Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

3084; Kila mtu anaongea, sisi tufanye.

By | June 11, 2023

3084; Kila mtu anaongea, sisi tufanye. Rafiki yangu mpendwa,Watu wanaongea sana,Wanaongea jinsi ambavyo wanataka kufanya makubwa.Wanaongea jinsi ambavyo wengi siyo waaminifu wala wachapa kazi.Wanaongea jinsi ambavyo mambo ni magumu na vikwazo vinavyowazuia.Wanaongea jinsi walivyoshindwa kutimiza yale waliyoahidi wao wenyewe. Lakini yote hayo wanayoongea hayana uzito kama ufanyaji.Kuongea kunafurahisha na kuridhisha, (more…)

3083; Piga kelele.

By | June 10, 2023

3083; Piga kelele. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye kitabu cha CHUO CHA MAUZO nimeandika; ustaarabu pekee kwenye biashara ni kuuza.Nimeandika hivyo kwa sababu kuna baadhi ya watu wanajiona ni wastaarabu sana hivyo kuna baadhi ya mambo hawawezi kufanya kwenye biashara.Halafu kwa bahati mbaya sana, wanakuwa hawauzi.Yaani mtu anajifanya mstaarabu, wakati hafanyi mauzo (more…)

3082; Siyo kupanga, ni kufanya.

By | June 9, 2023

3082; Siyo kupanga, ni kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye safari ya mafanikio, kila mtu huwa ana mipango mizuri ya jinsi ya kufikia mafanikio anayoyataka.Lakini licha ya hilo, bado ni watu wachache sana ambao wanayapata mafanikio wanayokuwa wanayataka. Hilo linaweza kukushangaza, iweje wengi wawe na malengo na mipango ya kufanikiwa, lakini wachache (more…)

3081; Mambo yasiwe mengi.

By | June 8, 2023

3081; Mambo yasiwe mengi. Rafiki yangu mpendwa,Kwa kuwa tunataka sana kufanikiwa kwenye maisha yetu, huwa hatuoni kama sisi wenyewe tunaweza kuwa kikwazo kwenye mafanikio yetu. Lakini ukweli ni kwamba sisi wenyewe huwa tunakuwa kikwazo kwa mafanikio makubwa tunayoyataka kwa sababu ya mambo kuwa mengi. Kadiri mtu anavyokuwa na orodha ndefu (more…)

3080; Mwili na mazingira.

By | June 7, 2023

3080; Mwili na mazingira. Rafiki yangu mpendwa,Tunaweza kuona tuna mambo mengi sana ambayo tunakabiliana nayo kwenye safari yetu ya mafanikio makubwa. Lakini kiuhalisia, mambo hayo yote yamegawanyika kwenye makundi makubwa mawili; mwili na mazingira. Mapambano ya kwanza kwetu ni ya kimwili.Miili yetu ni kikwazo cha kwanza kwetu kuyafikia mafanikio makubwa (more…)

3079; Hapana sahihi kwako.

By | June 6, 2023

3079; Hapana sahihi kwako. Rafiki yangu mpendwa,Kama ambavyo tunajua, tupo kwenye msimu wa kusema HAPANA.Ni msimu wa kupeleka umakini na juhudi zote kwenye vitu vichache na kuachana na vingine vyote. Watu hudhani kusema hapana ni rahisi sana, kwa sababu vitu unavyokataa ni ambavyo huvitaki.Lakini hilo siyo sahihi.Hapana sahihi kwako ni (more…)

3078; Maji yanayoizamisha meli.

By | June 5, 2023

3078; Maji yanayoizamisha meli. Rafiki yangu mpendwa,Sote tunajua ya kwamba meli huwa inaelea kwenye maji.Pamoja na uzito wake mkubwa, meli hiyo huwa inaendelea kuelea vizuri tu.Lakini hiyo yote ni kama maji yataendelea kubaki nje ya meli.Ni pale maji yanapoingia ndani ya meli ndiyo meli inapoanza kuzama. Kumbe basi, maji yanayoizamisha (more…)

3077; Kwa nini umekubali?

By | June 4, 2023

3077; Kwa nini umekubali? Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu tuna uwezo mkubwa sana wa kufanya chochote kile tunachotaka kufanya.Tunachohitaji tu ni sababu kubwa ya kwa nini tufanye kitu hicho.Tunapokuwa na sababu kubwa huwa tunaitimiza. Unapokuwa na msukumo mkubwa wa kufanya kitu, huwa unahakikisha unakifanya kweli.Na unapokosa msukumo mkubwa wa kufanya kitu, (more…)

3076; Kubadilika na kutokubadilika.

By | June 3, 2023

3076; Kubadilika na kutokubadilika. Rafiki yangu mpendwa,Hendry Ford, aliyekuwa mwanzilishi wa magari, alikuwa mtu mbishi sana kubadilika.Baada ya kuja na gari ambalo lilipendwa sana na watu, hakutaka kubadili chochote, badala yake aliendelea kuzalisha gari hilo hilo kwa muundo ule ule.Licha ya kushauriwa sana kubadilika, aliendelea kubaki kwenye kile alichoamini ndiyo (more…)

3075; Mapenzi na pesa.

By | June 2, 2023

3075; Mapenzi na pesa. Rafiki yangu mpendwa,Watu huwa wanasema kwamba pesa haiwezi kununua mapenzi,Sijui kuhusu hilo kwenye mahusiano, lakini kwenye biashara, mapenzi na pesa haviwezi kutenganishwa. Tukianzia kwenye msingi mkuu, utafanikiwa zaidi kwenye biashara ambayo unapenda kuifanya.Ile ambayo kwako siyo kazi, bali kama mchezo, ambayo inahusisha kusudi la maisha yako (more…)