Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

3074; Utekelezaji ni muhimu zaidi.

By | June 1, 2023

3074; Utekelezaji ni muhimu zaidi. Rafiki yangu mpendwa,Kuna watu wanadhani kwamba kinachowazuia wasifanikiwe ni hawajawa na wazo bora kabisa linaloweza kuwapa mafanikio makubwa. Wengine wengi wanadhani kinachowakwamisha ni hawajapata mtaji kwa ajili ya kuanzisha au kukuza biashara.Wengine ni ujuzi, koneksheni au kukosa rasilimali muhimu ambazo wanahitaji. Kuna mengi watu wanaweza (more…)

3073; Faida, Hasara au Mshahara?

By | May 31, 2023

3073; Faida, Hasara au Mshahara? Rafiki yangu mpendwa,Jim Rohn aliwahi kunukuliwa akisema; unalipwa kulingana na thamani unayoipeleka sokoni.Hiyo ina maana kwamba kiasi cha fedha unachopata, kinategemea sana kile unachofanya na jinsi unavyofanya vitu hivyo. Kanuni ya msingi ya uchumi pia inaeleza wazi juu ya mahitaji (demand) na upatikanaji (supply) wa (more…)

3072; Usilale.

By | May 30, 2023

3072; Usilale. Rafiki yangu mpendwa,Tuna maadui wengi sana ambao wanapambana kwa kila namna kutuzuia tusipate mafanikio makubwa tunayoyataka. Maadui wanaokuwa na nguvu sana siyo wa nje, bali wale wa ndani yetu.Hao ni maadui wanaokuwa na nguvu kwa sababu wanatujua kiundani. Uvivu, uzembe na mazoea ni maadui ambao wengi hawajui madhara (more…)

3071; Maamuzi na utekelezaji.

By | May 29, 2023

3071; Maamuzi na utekelezaji. Rafiki yangu mpendwa,Tunajua jinsi ambavyo wanaoyataka mafanikio ni wengi, lakini wanaoyapata wakiwa wachache sana. Tumeshajifunza sababu nyingi zinazowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa. Hapa tunakwenda kuangalia eneo moja ambalo siyo kwamba halifanyiki kabisa, bali halifanyiki kwa usahihi. Eneo hilo ni kufanya maamuzi na utekelezaji wa maamuzi hayo. Watu (more…)

3069; Kesho itakuwa ngumu zaidi.

By | May 27, 2023

3069; Kesho itakuwa ngumu zaidi. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu huwa tupo vizuri sana kwenye kujidanganya.Huwa tunapanga mambo yetu wenyewe, tukiwa na shauku kubwa.Lakini wakati wa kufanya mambo hayo unapofika, tunaahirisha.Tunajiambia tutafanya kesho. Kama kuna kaburi ambalo lina ndoto nyingi zilizoshindwa kutimia basi ni hiyo kesho.Hebu anza tu kwa kujiuliza wewe (more…)

3068; Kuweka na kutoa.

By | May 26, 2023

3068; Kuweka na kutoa. Rafiki yangu mpendwa,Kuna hadithi nyingi tulizokuwa tunafundishwa tulipokuwa watoto, ambazo zilikuwa na mafunzo makubwa sana kuhusu maisha.Nyingi zilikuwa na mafunzo ambayo yalikuwa nje ya uwezo wetu kuelewa kwenye hicho kipindi. Kwa mfano kuna hadithi ya kijana ambaye alipewa kazi ya kwenda kulisha mifugo nje kidogo ya (more…)

3067; Imani, Ujuzi, Kazi.

By | May 25, 2023

3067; Imani, Ujuzi, Kazi. Rafiki yangu mpendwa, Kuna kanuni chache sana za mafanikio.Lakini zimekuwa zikipinduliwa pinduliwa na kuishia kuonekana kama ni nyingi na ngumu.Hilo huwa linawakatisha tamaa wengi na kushindwa kufanikiwa. Maneno matatu yaliyopo hapo juu, siyo mageni kuyasikia.Na hata maana za maneno hayo unazijua vizuri kabisa. Lakini leo nataka (more…)

3065; Maumivu hayajatosha.

By | May 23, 2023

3065; Maumivu hayajatosha. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu ni viumbe wa tabia, huwa tunaanza kujenga tabia, kisha tabia zinatujenga.Asilimia kubwa ya yale tunayofanya kila siku, tunayafanya kwa tabia na mazoea na siyo kwa fikra. Hilo ndiyo huleta upinzani mkali sana kwenye mabadiliko.Watu huwa hawapo tayari kuachana na tabia na maumivu yao.Njia (more…)