Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

3064; Usawa usiowezekana.

By | May 22, 2023

3064; Usawa usiowezekana. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu huwa tunapenda sana usawa kwenye kila eneo la maisha.Tunapenda vitu vyote viende sawa ili tuyafurahie maisha yetu.Lakini ukweli mchungu ni kwamba, hakuna usawa kwenye mambo yote na wala hautakuja kuwepo. Mambo yote kwenye maisha huwa yanakwenda kwa kanuni za asili, ambazo haziangalii usawa (more…)

3063; Kataa kushindwa.

By | May 21, 2023

3063; Kataa kushindwa. Rafiki yangu mpendwa,Kitu kimoja ambacho nimekuwa narudia sana kukisema ni kwamba watu huwa hatupati kile tunachotaka, bali kile tunachokubali, tunachokivumilia. Na nimekuwa nikitumia mifano rahisi ya miji mikubwa.Ni vigumu sana ukasikia mtu amekufa kwa njaa kwenye mji wowote mkubwa.Lakini ndani ya miji hiyo, kuna wengi ambao hawana (more…)

3062; Hakuna mjadala.

By | May 20, 2023

3062; Hakuna mjadala. Rafiki yangu mpendwa,Fikiria kuna kitu muhimu sana ambacho unataka kununua.Unaongea na muuzaji wa kitu hicho na anakupa bei.Mnajadiliana kwenye bei na kufikia muafaka kati yako na muuzaji. Unaondoka kwenda kuchukua fedha za kulipia kama mlivyokubaliana.Unarudi ukiwa na kiasi cha fedha kilichokamilika kulingana na makubaliano.Lakini muuzaji anakuambia hataweza (more…)

3061; Kuaminiana.

By | May 19, 2023

3061; Kuaminiana. Rafiki yangu mpendwa,Dunia inaendeshwa kwa msingi mkuu wa kuaminiana.Bila ya kuaminiana, dunia haiwezi kwenda. Tunaweza kufanya yote tunayoyafanya kwenye maisha, kwa sababu tunaweza kuwaamini wengine bila hata ya sababu yoyote. Tunakuwa tayari kuyaweka maisha yetu kwenye hatari kubwa kwa kuwaamini wengine kwamba watafanya kile kilicho sahihi. Fikiria unaenda (more…)

3060; Kuna vitu unafanya kwa usahihi.

By | May 18, 2023

3060; Kuna vitu unafanya kwa usahihi. Rafiki yangu mpendwa,Takwimu nyingi za kibiashara zimekuwa zinasikitisha sana.Biashara nyingi zinazoanzishwa huwa zinakufa ndani ya mwaka mmoja au miwili. Vifo vya biashara hizo nyingi huwa vinatokana na changamoto mbalimbali ambazo waanzilishi hawakujua na kujiandaa nazo.Lakini pia makosa, uvivu na uzembe vimekuwa vinachangia sana vifo (more…)

3059; Ahadi yangu kwako.

By | May 17, 2023

3059; Ahadi yangu kwako. Rafiki yangu mpendwa,Tangu nilipoanzisha huduma ya ukocha ya KISIMA CHA MAARIFA mwaka 2014, sikuwa naichukulia huduma hii kama biashara, kwa maana ya kuwaangalia washiriki kama wateja. Badala yake nimekuwa naichukulia kama huduma ninayoijenga na washiriki nimekuwa nawachukulia kama bidhaa ambayo ipo ndani ya huduma.Ndiyo maana gharama (more…)

3058; Wote tupo chini ya misingi hii.

By | May 16, 2023

3058; Wote tupo chini ya misingi hii. Rafiki yangu mpendwa,Tawala nyingi za kidikteta huwa zinaanza vizuri sana.Kiongozi ambaye ni dikteta, anaanza akiwa na nia njema kabisa ya kufanya maisha ya watu kuwa bora. Anapata imani kubwa ya watu mwanzoni na mambo yanaenda vizuri sana.Mabadiliko mazuri yanaonekana mwanzoni na watu kunufaika. (more…)

3057; Kwa nini nataka uuze.

By | May 15, 2023

3057; Kwa nini nataka uuze. Rafiki yangu mpendwa,Kama ambavyo nimeshakuandikia mara kwa mara, una malengo makubwa matatu kwenye biashara yako.Malengo hayo ni kujenga mfumo wa kuiendesha biashara, kujenga timu imara na kujenga wateja waaminifu. Ili uweze kutekeleza malengo hayo, kuna majukumu makuu mawili ambayo unapaswa kuyatekeleza. Na majukumu hayo yanakutaka (more…)

3056; Unajivuruga mwenyewe.

By | May 14, 2023

3056; Unajivuruga mwenyewe. Rafiki yangu mpendwa,Kutokana na ugumu na changamoto za safari ya mafanikio, watu wengi huwa wanatafuta watu wa kuwapelekea lawama pale mambo yao yanavyokwenda tofauti na matarajio. Hapo watu huona wazi kwamba wamevurugwa na wengine ambao wamefanya tofauti na walivyotarajia. Lakini huo siyo ukweli, hakuna mtu yeyote yule (more…)

3055; Usijipe kazi usizoziweza.

By | May 13, 2023

3055; Usijipe kazi usizoziweza. Rafiki yangu mpendwa,Safari ya mafanikio ambayo tupo ni safari ngumu na ndefu.Ugumu wa safari hii ni kazi kubwa tunayopaswa kuweka ili kupata matokeo makubwa tunayotaka kuyapata. Wengi huwa wanashindwa kazi hiyo, siyo kwa sababu haiwezekani, bali kwa sababu wanachoka kwa kazi nyingine wanazokuwa wamejipa. Yaani wanakuwa (more…)