Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

Barua ya II; Usumbufu Kwenye Usomaji.

By | May 12, 2023

Barua ya II; Usumbufu Kwenye Usomaji. Rafiki yangu Mstoa,Maisha ni darasa ambalo halina kuhitimu. Hiyo ina maana kwamba kila wakati mtu unapaswa kuwa unajifunza. Zipo njia nyingi za kujifunza, na moja iliyo kuu na ambayo imedumu kwa miaka mingi zaidi ni kusoma vitabu. Tangu enzi na enzi, maarifa yamekuwa yanashirikishwa (more…)

3054; Uhakika wa ushindi.

By | May 12, 2023

3054; Uhakika wa ushindi. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye safari ya maisha ya mafanikio, ushindi ndiyo kitu ambacho kila mtu anakitaka.Lakini pia kimekuwa ndiyo kitu adimu sana. Ni watu wachache mno ndiyo wamekuwa wanapata mafanikio wanayoyataka. Kwa jinsi ambavyo mafanikio yamekuwa adimu, yanaonekana kama ni kitu cha kubahatisha, ambacho mtu hawezi kuwa (more…)

3053; Turudi kwenye misingi.

By | May 11, 2023

3053; Turudi kwenye misingi. Rafiki yangu mpendwa,Iwapo unajenga nyumba ya ghorofa, lakini kila unapojaribu kwenda ngazi za juu zaidi unakwama, hapo inabidi urudi kwenye msingi.Unapaswa kuangalia msingi mzima ambapo ghorofa hiyo imejengwa na kama utagundua msingi siyo sahihi basi unapaswa kuuboresha kwanza kabla hujaendelea. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye kila (more…)

3052; Siyo unachotaka, bali unachotoa.

By | May 10, 2023

3052; Siyo unachotaka, bali unachotoa. Rafiki yangu mpendwa,Karibu kila mtu kwenye maisha anataka kupata mafanikio makubwa.Lakini kwenye uhalisia ni watu wachache sana wanaopata mafanikio makubwa wanayoyataka. Tafiti nyingi zimefanywa ili kujua nini kinawatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.Vitu vingi vya nje ambavyo wengi walidhani ndiyo vinawatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa, vimeonekana kutokuwa na (more…)

3051; Kupanda na kushuka.

By | May 9, 2023

3051; Kupanda na kushuka. Rafiki yangu mpendwa, Safari ya mafanikio huwa ina kupanda na kushuka.Hizo ni pande mbili za safari hiyo, ambazo huwa hazifanani.Upande mmoja unahitaji kazi kubwa wakati upande mwingine hauhitaji kazi yoyote. Kupanda kunahitaji kazi, kunahitaji juhudi kubwa kuwekwa ili kuvuka nguvu kubwa ya mvutano inayofanya vitu vibaki (more…)

3050; Wateke.

By | May 8, 2023

3050; Wateke. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye malengo makubwa matatu tunayoyafanyia kazi kwenye kujenga biashara, yaani MFUMO, TIMU na WATEJA, lengo la TIMU ndiyo limekuwa gumu zaidi. Kila ambaye ameshachukua hatua kwenye kujenga timu, amekutana na changamoto nyingi sana.Changamoto ya kwanza ni kukosekana kwa watu sahihi ambao wanaweza kutekeleza majukumu yaliyopo.Changamoto ya (more…)

3049; Mambo ambayo huhitaji kukumbusha, lakini inabidi.

By | May 7, 2023

3049; Mambo ambayo huhitaji kukumbusha, lakini inabidi. Rafiki yangu mpendwa,Kuna mambo ya msingi kabisa kwenye safari ya maisha na mafanikio ambayo huhitaji kuwa unakumbushwa kila mara.Haya ni mambo ambayo unapaswa kuwa unayaelewa kutoka ndani kabisa ya moyo wako. Lakini kwa sababu binadamu tuna tabia ya kusahau mambo, hata yale ya (more…)

3048; Usinipange.

By | May 6, 2023

3048; Usinipange. Rafiki yangu mpendwa,Kuna mwenendo fulani ninaouona kwa watu wanaokuwa wananiomba ushauri kwenye mambo mbalimbali.Mtu anaelezea jambo lake jinsi lilivyo na kuomba ushauri wa hatua gani za kuchukua. Tunajadiliana namna bora ya kulikabili jambo linalokuwa mbele ya mtu na kufikia tamati ya hatua sahihi za kwenda kuchukua.Lakini sasa cha (more…)

3047; Ni bora uache mapema.

By | May 5, 2023

3047; Ni bora uache mapema. Rafiki yangu mpendwa,Kuna sababu kuu mbili kwa nini watu hawapati kile wanachotaka kwenye maisha yao.Moja ni hawajui kwa hakika nini hasa wanachotaka.Na mbili ni hawajajitoa kweli kweli kupata kile wanachotaka. Pamoja na mahangaiko makubwa ambayo unaona watu wengi wanayo, sehemu kubwa ya watu hao hawajui (more…)

3046; Wapambanie kombe.

By | May 4, 2023

3046; Wapambanie kombe. Rafiki yangu mpendwa,Kadiri chochote kile unachofanya kinavyokuwa rahisi kupatikana, ndivyo wengine wanavyokidharau na kukipuuza. Kama muda wako unapatikana kwa urahisi, watu watautumia hovyo kwa mambo yasiyokuwa na tija.Watakuzamisha kwenye mambo ya hovyo, yanayokula muda wako na yasiyokuwa na tija yoyote kwenye yale unayofanya au unayotaka kufikia. Kadhalika (more…)