Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

3045; Afya yako ya akili.

By | May 3, 2023

3045; Afya yako ya akili. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye safari ya mafanikio, afya yako ya akili ni rasilimali muhimu sana unayopaswa kuilinda. Safari ya mafanikio imejaa vikwazo na changamoto za kila aina.Usipokuwa imara kuvuka hayo, yatakuchosha haraka sana na kujikuta ukikata tamaa. Ili kuimarisha afya yako ya akili, zingatia mambo haya (more…)

3044; Hofu na majuto.

By | May 2, 2023

3044; Hofu na majuto. Rafiki yangu mpendwa,Mafanikio yoyote yale kwenye maisha yanaanzia kwenye misingi fulani ambayo huwa inajengwa na kila mtu anayehusika kwenye eneo hilo. Mafanikio pia huwa yanahusisha kufanya mambo mapya ambayo ni tofauti kabisa na mazoea yaliyopo kwenye ebeo husika. Inapokuja kwenye ufanyaji wa mambo hayo mapya, huwa (more…)

3043; Roho mbaya.

By | May 1, 2023

3043; Roho mbaya. Rafiki yangu mpendwa,Moja ya vikwazo vikubwa kwenye safari ya mafanikio ya wengi ni jamii inayokuwa inamzunguka.Jamii hiyo inapokuwa na watu ambao hawana mafanikio wala hawapo kwenye safari ya mafanikio makubwa, inazuia watu wengine wasiyapambanie mafanikio. Kwa kuwa safari ya mafanikio inamtaka mtu ajitoe sana na kusema HAPANA (more…)

3042; Ipende kazi.

By | April 30, 2023

3042; Ipende kazi. Rafiki yangu mpendwa,Tunaishi kwenye zama ambazo kila mtu anatafuta njia ya mkato na ya haraka ya kufanikiwa isiyohusisha ufanyaji wa kazi. Kazi imekuwa inachukuliwa kama kitu cha mateso na kinachofanywa na wale wasiojielewa.Lakini licha ya watu kutafuta njia za kukwepa kazi, hakuna ambaye amewahi kufanikiwa bila kuipenda (more…)

3041; Kazi yako kuu.

By | April 29, 2023

3041; Kazi yako kuu. Rafiki yangu mpendwa,Ni rahisi na watu wanapenda sana kujipa vyeo vikubwa kwenye biashara zao.Kuna wanaojiita waanzilishi, wengine wamilili na wengine wakurugenzi wakuu wa biashara zao. Vyeo hivyo vinaweza kuwa sahihi na vinavyomfanya mtu ajisikie sana vizuri, lakini ni vyeo ambavyo vinaweza visiwe na wajibu wa kutekeleza (more…)

3040; Raha ya mchezo.

By | April 28, 2023

3040; Raha ya mchezo. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi huwa wanapenda kufuatilia michezo mbalimbali.Japokuwa hakuna mtu anapenda kuona timu anayoshabikia ikifungwa, kama timu hiyo inaweza kushinda mara zote bila ya kusumbuka, mchezo hauwi na raha ya kuangalia. Kadhalika sinema na maigizo mbalimbali.Kama mhusika mkuu hakutani na changamoto mbalimbali kwenye safari yake, (more…)

3039; Gharama ya kulipa.

By | April 27, 2023

3039; Gharama ya kulipa. Rafiki yangu mpendwa,Kila kitu kwenye maisha huwa kina gharama ambayo mtu anapaswa kulipa ili kukipata.Gharama hiyo siyo tu kwenye fedha, bali pia kwenye kazi, muda, nguvu n.k. Thamani ambayo watu wanakipa kitu, inaendana na gharama ambayo wamelipa kukipata.Kama kitu kinapatikana kirahisi, watu wanakipa thamani ndogo na (more…)

3038; Kuamua unachotaka.

By | April 26, 2023

3038; Kuamua unachotaka. Rafiki yangu mpendwa,Hatua ya kwanza muhimu ya kufanikiwa kwenye maisha ni kuamua nini hasa unachotaka.Hayo ni maelezo mafupi na rahisi kueleza, lakini ambayo utekelezaji wake ni mgumu sana. Kuna kutaka na kuna kuamua.Kila mtu kuna vitu vingi anavyokuwa anataka, vitu anavyotamani awe navyo au kuvifikia.Halafu kuna kuamua (more…)

3037; Uwajibikaji haukwepeki.

By | April 25, 2023

3037; Uwajibikaji haukwepeki. Rafiki yangu mpendwa,Mafanikio ya aina yoyote ile kwenye maisha huwa yanaambatana na uwajibikaji.Ni uwajibikaji wa hali ya juu sana ndiyo unaozalisha mafanikio makubwa ambayo watu wanayapata kwenye maisha yao. Mafanikio pia yanategemea sana watu ambao mtu anaambatana nao.Kwa sababu hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu peke yake, (more…)

3036; Ndiyo ni Hapana kubwa.

By | April 24, 2023

3036; Ndiyo ni Hapana kubwa. Rafiki yangu mpendwa,Wakati tupo kwenye msimu wa HAPANA, tukumbushane jambo muhimu sana kuhusu NDIYO na HAPANA. Unaposema HAPANA kwenye kitu kimoja, unakuwa umekikataa kitu hicho kimoja tu.Hilo linakupa fursa ya kuweza kuangalia mambo mengine mazuri yanayoendana na kile unachofanya na kuweza kuyasemea NDIYO.Kwa maana hiyo (more…)