Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2985; Usipoteze hiyo kazi ambayo umeshaweka.

By | March 4, 2023

2985; Usipoteze hiyo kazi ambayo umeshaweka. Rafiki yangu mpendwa,Tofauti ya kufanikiwa na kushindwa siyo akili wala juhudi zinazowekwa. Wanaofanikiwa na wanaoshindwa hawatofautiani sana kiakili.Na juhudi wanazokuwa nazo pia hazitofautiani sana. Tofauti kubwa ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa inaanzia kwenye msimamo.Wanaofanikiwa wanapeleka juhudi zao kwenye jambo moja kwa muda mrefu.Wakati wanaoshindwa wanahamisha (more…)

2983; Ongeza kasi ili kuwa imara.

By | March 2, 2023

2983; Ongeza kasi ili kuwa imara. Rafiki yangu mpendwa,Kama umewahi kuendesha baiskeli unajua kitu kimoja, kama inayumba yumba, ili kuifanya iwe na mwendo imara na wa utulivu, unapaswa kuongeza kasi zaidi.Ndiyo kwa kuiweka baiskeli kwenye mwendo wa kasi kubwa, unaipa utulivu na uimara mkubwa kwenye mwendo wake. Hivyo pia ndivyo (more…)

2982; Kupangiwa cha kufanya.

By | March 1, 2023

2982; Kupangiwa cha kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Tunajua maisha ni magumu na yana changamoto za kila aina.Lakini sehemu kubwa ya ugumu wa maisha huwa tunaisababisha sisi wenyewe.Hasa kutokana na matarajio tunayokuwa nayo kwenye yale tunayofanya. Kwenye kila eneo la maisha, ugumu na urahisi huwa vinapishana.Chochote ambacho tunakifanya kwa urahisi huwa kinakuwa (more…)

2981; Fanya kinachopaswa kufanyika.

By | February 28, 2023

2981; Fanya kinachopaswa kufanyika. Rafiki yangu mpendwa,Ili uweze kupata matokeo makubwa unayoyataka, lazima ufanye mambo mapya, makubwa na magumu.Na ili uweze kufanya mambo hayo magumu, lazima ujitoe kafara. Unapaswa kufanya kinachopaswa kufanyika na siyo unachotaka kufanya au unachoweza kufanya.Unapaswa ujitoe kupitiliza na siyo kujiwekea ukomo wa nini unaweza na nini (more…)

2980; Kubali kupitwa.

By | February 27, 2023

2980; Kubali kupitwa. Rafiki yangu mpendwa,Inapokuja kwenye swala la mafanikio, wengi huwa na mtazamo wa kutokukubali kupitwa na chochote.Lakini huo ni mtazamo ambao unakuwa kikwazo kikubwa kwa wengi kupata mafanikio makubwa. Tamaa huwafanya wengi kuhangaika na mengi wakidhani watairahisisha safari ya mafanikio, lakini kwa uhalisia wanaishia kuwa wameirefusha safari hiyo. (more…)

2979; Hofu ya mafanikio.

By | February 26, 2023

2979; Hofu ya mafanikio. Rafiki yangu mpendwa,Kwa kipindi kirefu ambacho nimekuwa najifunza kuhusu mafanikio, nimekuwa na kutana na sababu mbalimbali zinazowazuia watu kufanikiwa.Moja ya sababu hizo ni hofu ya mafanikio. Nilikuwa sielewi iweje mtu anayeyataka mafanikio awe pia anayahofia mafanikio?Sikuwa nalipa sana uzito hilo kwenye sababu za watu kutokufanikiwa. Ni (more…)

2978; Biashara rahisi kufanya.

By | February 25, 2023

2978; Biashara rahisi kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Swali la ni biashara gani rahisi kwa mtu kufanya ni swali ambalo nimekuwa naulizwa kila mara na watu.Kipindi cha nyuma nilikuwa nakazana kuwaelewesha watu ni biashara gani zinaweza kuwafaa watu kulingana na hali wanazokuwa nazo. Lakini kwa uzoefu ambao nimeshajijengea mpaka sasa kwenye biashara, (more…)

2977; Furahia kushindwa.

By | February 24, 2023

2977; Furahia kushindwa. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye safari ya mafanikio ambayo tupo, hakuna kitu kizuri ambacho kila mmoja anakitaka kama ushindi. Tunapenda sana ushindi, uwe ni mdogo mdogo au mkubwa, kwa sababu ni kiashiria kizuri kwamba tunaelekea kule tunakotaka kufika. Japokuwa kushinda kunaleta hali ya kujisikia vizuri wakati huo wa ushindi, (more…)

2976; Muda na usumbufu.

By | February 23, 2023

2976; Muda na usumbufu. Rafiki yangu mpendwa,Inapokuja kwenye muda, msimamo wangu uko wazi mara zote, tatizo letu siyo muda, bali kile tunachofanya na muda tulionao.Ninaamini, bila ya shaka yoyote kwamba muda tunao mwingi, ila tu tunautumia vibaya.Kwamba tatizo kubwa la muda tulilonalo, siyo kwamba muda ni wa uhaba, bali tunao (more…)