Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2965; Siamini.

By | February 12, 2023

2965; Siamini. Rafiki yangu mpendwa,Kumekuwa na sababu moja pendwa kwa watu wengi wanaoshindwa kufanya yale wanayopaswa kufanya. Sababu hiyo ni; “SIna muda.”Karibu kila mtu anatumia kauli hiyo kama sababu ya kushindwa kufanya makubwa. Lakini niseme ukweli kabisa, mimi siamini kabisa kwamba hakuna muda.Naamini bila ya shaka yoyote kwamba muda tayari (more…)

2964; Onyesha kazi yako.

By | February 11, 2023

2964; Onyesha kazi yako. Rafiki yangu mpendwa,Wakati upo shuleni, ulifundishwa namna sahihi ya kufanya hisabati.Kila swali la hisabati lilikuwa na sehemu tatu.Sehemu hizo ni swali, kazi, jibu.Katika kujibu maswali hayo ya hisabati hukutakiwa tu kutoa jibu sahihi, bali ulitakiwa kuonyesha njia uliyotumia kupata jibu hilo.Mara nyingi, hata kama ulikosa jibu, (more…)

2963; Imani na matamanio makubwa.

By | February 10, 2023

2963; Imani na matamanio makubwa. Rafiki yangu mpendwa,Ili uweze kufikia mafanikio makubwa unayoyataka kwenye maisha yako, unapaswa kuchukua hatua kubwa pia.Hatua ambazo siyo za kawaida na wengi hawawezi kuzichukua. Unapaswa kuchukua hatua kubwa kwa namna ambayo wengine wanakushangaa, ya kwamba unawezaje kuchukua hatua za aina hiyo. Unapaswa kufanya kazi kwa (more…)

2962; Weka dau lako hapa.

By | February 9, 2023

2962; Weka dau lako hapa. Rafiki yangu mpendwa, Huwa sishauri mtu yeyote mwenye akili timamu acheze kamari au michezo mingine ya kubahatisha, ambayo kwangu yote hayo ni kitu kimoja. Lakini mcheza kamari au michezo hiyo ya kubahatisha akisikia hayo, anakimbilia kukuambia kwenye maisha kila kitu ni kamari. Hapo akimaanisha hakuna (more…)

2961; Uza maziwa, siyo ng’ombe.

By | February 8, 2023

2961; Uza maziwa, siyo ng’ombe. Rafiki yangu mpendwa,Ukiwa na ng’ombe, ambaye unamkamua maziwa, halafu akajitokeza mtu na kukuambia ng’ombe wako anatoa maziwa vizuri, niuzie maana nina uhitaji sana wa maziwa.Kama ndiye ng’ombe pekee uliyenaye na ndiye tegemeo kwako, unajua vyema kwamba hutakubali kumuuza ng’ombe huyo, bali utamwambia umuuzie maziwa. Kadhalika (more…)

2960; Usiwauzie, wafundishe.

By | February 7, 2023

2960; Usiwauzie, wafundishe. Rafiki yangu mpendwa,Mauzo yanakuwa magumu kwa wengi kwa sababu wamekuwa wakikazana kuwalazimisha watu kununua.Wanachosahau watu hao ni kwamba hakuna mteja anayependa kuona amelazimishwa kununua. Kuuza ni kufundisha na kufundisha ni kuuza.Wauzaji ambao wamekuwa wanaweka mbele kipaumbele cha kufundisha badala ya kuuza, wamekuwa wanaingiza kipato kikubwa sana. Wafundishe (more…)

2959; Kisima kitupu.

By | February 6, 2023

2959; Kisima kitupu. Rafiki yangu mpendwa,Kama una bomba la maji ambalo linatokea kwenye kisima, lakini halitoi maji, siyo kwamba maji hakuna kabisa, bali ni kisima ndiyo kitupu.Kama kisima kingekuwa na maji, ni dhahiri bomba lingetoa maji. Unaweza kulalamika hakuna wateja kwenye biashara yako, lakini huo siyo ukweli. Wateja wapo na (more…)

2958; Abiria ambao hawaendi Arusha washuke.

By | February 5, 2023

2958; Abiria ambao hawaendi Arusha washuke. Rafiki yangu mpendwa,Pata picha wewe ni dereva wa basi ambalo linafanya safari zake kutoka Dar kwenda Arusha. Basi imepaki kwenye stendi kuu ya mabasi ya Dar na kupakia abiria.Basi inajaa kisha unaanza safari. Ile unatoka tu kwenye stendi na kuelekea kibaha, kundi la abiria (more…)

2957; Utatu wa umasikini.

By | February 4, 2023

2957; Utatu wa umasikini. Rafiki yangu mpendwa,Umasikini ni mbaya sana.Kuna vitu vingi sana tunavyokutana navyo ambavyo vinadhihirisha umasikini na madhara yake kwetu. Aliyekuwa raisi wa kwanza wa Tanzania, Mwl. J. K. Nyerere alichagua maadui wakubwa watatu ambao alishawishi kila mwananchi kupambana nao.Maadui hao walikuwa ni Ujinga, Maradhi na Umasikini.Pamoja na (more…)

2956; Viwango, Fokasi na Kasi.

By | February 3, 2023

2956; Viwango, Fokasi na Kasi. Rafiki yangu mpendwa,Kama unataka kujenga biashara yenye mafanikio makubwa sana, unapaswa kufanyia kazi kwa uhakika maeneo hayo matatu. Unapaswa kuweka viwango vya juu sana kisha kuhakikisha watu wote wanafikia viwango hivyo.Biashara nyingi hazifanikiwi kwa sababu hakuna viwango vilivyowekwa.Biashara inakuwa haina msimamo wowote.Kila wakati inabadilika ili (more…)