Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2955; Kupendwa au kuheshimiwa?

By | February 2, 2023

2955; Kupendwa au kuheshimiwa? Rafiki yangu mpendwa,Wajibu wetu wa kwanza kama viongozi kwenye biashara zetu ni kuwafanya watu wafanye vitu ambavyo hawataki kufanya, lakini vyenye manufaa kwao. Na hilo halitakuweka kwenye nafasi ya kupendwa sana na watu hao unaowaongoza, kwa sababu utakuwa unawasukuma kuondoka kwenye mazoea.Hakuna kitu kinachowafanya watu wajisikie (more…)

2954; Biashara yenye mauzo ya faida.

By | February 1, 2023

2954; Biashara yenye mauzo ya faida. Rafiki yangu mpendwa,Takwimu za kibiashara kila mara huwa zinasikitisha sana. Kati ya biashara mpya zinazoanzishwa, asilimia 80 huwa zinakufa ndani ya miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. Haijalishi ni biashara ya aina gani na inafanywa na nani, hatari ya biashara mpya huwa ni kubwa sana. (more…)

2953; Fanya machache kufanya makubwa.

By | January 31, 2023

2953; Fanya machache kufanya makubwa. Rafiki yangu mpendwa,Huwa tunadhani ili tuweze kufanya makubwa, basi tunahitaji kufanya mambo mengi sana.Hilo linapelekea tujihangaishe na mambo mengi na mapya kila wakati. Lakini cha kushangaza, hata baada ya kuhangaika na mengi, bado matokeo tunayoishia kupata ni ya kawaida sana. Tunahangaika na mengi, tunachoka sana (more…)

2952; Hili basi linaenda wapi?

By | January 30, 2023

2952; Hili basi linaenda wapi? Rafiki yangu mpendwa,Pata picha una safari yako ya kwenda eneo fulani.Unafika stendi ya mabasi na kukata tiketi ya safari yako na kuelekezwa basi unalopaswa kupanda.Unakwenda kwenye basi na muda siyo mrefu dereva anawasha gari kuondoka.Kujihakikishia safari yako, unamuuliza dereva swali; “hili basi linaenda wapi?”Dereva anakuangalia (more…)

2951; Njia yangu au njia kuu.

By | January 29, 2023

2951; Njia yangu au njia kuu. Rafiki yangu mpendwa, Zipo njia nyingi sana za kuweza kumfikisha mtu kwenye mafanikio anayoyataka. Uwepo wa njia hizo nyingi ulipaswa uwe ni uhuru mkubwa kwa wengi, kwa kuwaonyesha wanaweza kupata wanachotaka. Lakini badala yake njia hizo nyingi zimegeuka kuwa usumbufu mkubwa kwa wengi.Kwani watu (more…)

2950; Yule kuku aliyekuwa anataga sana.

By | January 28, 2023

2950; Yule kuku aliyekuwa anataga sana. Rafiki yangu mpendwa,Kila kitu kwenye maisha huwa kinakuja na tarehe ya mwisho wa matumizi.Kwa Kiingereza wanaita expire date.Kila kitu, ikiwepo mimi na wewe.Na hiyo haimaanishi tu kifo, bali mwisho wa matumizi ya uzalishaji mkubwa. Kama umewahi kufuga, unakumbuka kuku uliyekuwa naye, ambaye alikuwa anataga (more…)

2949; Upendeleo.

By | January 27, 2023

2949; Upendeleo. Rafiki yangu mpendwa, Miaka ya nyuma niliwahi kuongea na rafiki yangu ambaye alikuwa ameomba kazi ya udaktari kwenye shirika fulani kubwa. Alikuwa ananishirikisha baadhi ya maswali aliyoulizwa wakati wa usaili.Moja ya maswali aliyoulizwa ni iwapo kuna foleni ya watu wanasubiria kuingia kwa daktari na kuna mtu wa kawaida (more…)

2948; Itakugharimu kabla haijakunufaisha.

By | January 26, 2023

2948; Itakugharimu kabla haijakunufaisha. Rafiki yangu mpendwa,Moja ya vitu ambavyo vinawazuia watu wengi wasipate mafanikio makubwa ni kukosa msimamo.Wanapanga vitu ambavyo watafanya, lakini wanapoanza kufanya na vikawagharimu, huwa wanaacha mara moja. Kitu ambacho wengi wamekuwa hawajui ni kwamba kila kitu kwenye maisha huwa kina gharama yake.Kila maamuzi unayofanya kwenye eneo (more…)

2946; Wasaidie kufanya maamuzi.

By | January 24, 2023

2946; Wasaidie kufanya maamuzi. Rafiki yangu mpendwa,Kama ulikuwa hujui, moja ya wajibu wako mkubwa ni kuwasaidia watu kufanya maamuzi.Kwa sababu watu wengi hawana ujasiri wa kutosha kufanya maamuzi yao wenyewe. Siyo kwamba hawajui wanachotaka, wanajua sana, ila uthubutu wa kuamua ndiyo wamekosa. Kama wewe unataka mambo yako yaende na usikwamishwe (more…)