Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2945; Mapigo ya moyo yapo, Anapumua.

By | January 23, 2023

2945; Mapigo ya moyo yapo, Anapumua. Rafiki yangu mpendwa, Kila mmoja analalamika sana kuhusu changamoto ya wafanyakazi.Imekuwa vigumu sana kupata wafanyakazi sahihi wa kutusaidia kwenye biashara zetu. Ni kweli hii ni changamoto kubwa na inayowaathiri watu wengi.Na pia ni kweli uwezo na umakini wa wengi wanaotafuta kazi upo chini. Lakini (more…)

2944; Usifanyie kazi ushauri huu, kwanza.

By | January 22, 2023

2944; Usifanyie kazi ushauri huu, kwanza. Rafiki yangu mpendwa, Kabla sijakushauri kitu chochote, huwa kwanza nakifanyia kazi ili kujua uwezekano wake na changamoto zake. Hivyo ninapokushauri ufanye au usifanye kitu fulani, nakuwa tayari najua nini unakwenda kukabiliana nacho. Sasa kuna kitu ambacho ndiyo nimeanza kukifanya na bado sijawa na matokeo (more…)

2943; Watakusumbua sana.

By | January 21, 2023

2943; Watakusumbua sana. Rafiki yangu mpendwa, Kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yako huwa unajiwekea vigezo vya watu wa aina gani ujihusishe nao. Vigezo hivyo huwa vinategemea kile unachofanya na watu sahihi wa kuwalenga. Mara kwa mara huwa unakutana na watu ambao hawakidhi vigezo ulivyoweka, lakini bado wanataka kushirikiana na wewe. (more…)

2940; Namba mbaya kwenye biashara.

By | January 18, 2023

2940; Namba mbaya kwenye biashara. Rafiki yangu mpendwa, Ipo namba ambayo ni mbaya sana kwenye biashara na ambayo unapaswa kuiepuka kama unataka kujenga biashara yenye mafanikio makubwa. Namba hiyo ni moja. Kuwa na kitu chochote kimoja kwenye biashara ni hatari kubwa. Inakuweka kwenye utegemezi mbaya na unaokuwa kikwazo kwa ukuaji. (more…)

2939; Mnatofautiana sana.

By | January 17, 2023

2939; Mnatofautiana sana. Rafiki yangu mpendwa, Wewe na wafanyakazi uliowaajiri kwenye biashara yako mnatofautiana sana. Mnatofautiana kimtazamo, wakati wewe unaangalia kujenga biashara ambayo itakuwa kubwa na yenye mafanikio, wao wanachoangalia ni kufanya kazi ya siku husika tu. Mnatofautiana kiajenda, wakati ajenda yako ni kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kwa malipo unayoweza (more…)

2938; Mfalme ni mmoja tu kwenye biashara.

By | January 16, 2023

2938; Mfalme ni mmoja tu kwenye biashara. Rafiki yangu mpendwa, Kila himaya huwa inakuwa na mfalme mmoja tu. Na neno la mfalme huwa ndiyo sheria, hufuatwa na kila mmoja. Kwenye biashara pia kuna mfalme mmoja anayepaswa kuheshimiwa na wote. Mfalme huyo ni MAUZO. Kwa kuwa mauzo ndiyo kitu pekee kinachoingiza (more…)

2937; Kinachohesabika kama kazi.

By | January 15, 2023

2937; Kinachohesabika kama kazi. Rafiki yangu mpendwa, Kwenye kurasa za nyuma tumeshirikishana dhana ya thamani ya muda wako na mpangilio wa masaa 16 ya kazi kwenye siku. Pamoja na watu kufanyia kazi hayo, bado kuna wengi ambao wanachanganya inapokuja kwenye swala la kazi. Wengi hudhani chochote wanachofanya kwenye muda wao (more…)

2936; Safisha kwanza.

By | January 14, 2023

2936; Safisha kwanza. Rafiki yangu mpendwa, Kama unataka kutumia kikokotozi kukokotoa hesabu fulani na ukakuta kikokotozi hicho tayari kina hesabu nyingine, unasafisha kwanza ndipo unaweka hesabu mpya. Kwa kuchanganya hesabu mpya na za zamani, unapata majibu yasiyo sahihi. Kabla hujapanda mazao kwenye shamba, unalisafisha kwanza kuondoa magugu. Ukipanda mazao kwenye (more…)