Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2935; Somo kutoka makaburini.

By | January 13, 2023

2935; Somo kutoka makaburini. Rafiki yangu mpendwa, Watu wengi huwa na hofu ya makaburi kulingana na mitazamo na imani ambazo tumejengewa kwenye jamii zetu. Kuna hadithi nyingi juu ya yanayoendelea kwenye makaburi ambazo siyo sahihi. Lakini pia kuna mengi ya kujifunza kwenye makaburi, ambayo tukiyaelewa na kuyafanyia kazi, tutaweza kupiga (more…)

2934; Akili za mkulima.

By | January 12, 2023

2934; Akili za mkulima. Rafiki yangu mpendwa, Wengi wetu tumepitia familia ambazo zilikuwa zinajihusisha na kilimo. Hivyo tuna uelewa fulani juu ya kilimo. Tunajua kabisa kwamba mkulima hapaswi kula mbegu. Hata njaa ikimkamata kiasi gani, mkulima makini anajua mbegu hailiwi, maana ndiyo kitu cha kumvusha kipindi kijacho. Lakini pia mkulima (more…)

2933; Hatari ya saratani.

By | January 11, 2023

2933; Hatari ya saratani. Rafiki yangu mpendwa, Saratani huwa ni ukuaji wa eneo fulani la mwili usio na udhibiti wala ukomo. Hatari kubwa ya saratani ni pale inapoachwa ikaendelea kukua. Kadiri saratani inavyochelewa kuondolewa, ndivyo inavyokuwa na hatari kubwa. Na ubaya wake ni inavyokua haibaki tu pale inapokuwa imeanzia, badala (more…)

2932; Ndiyo maana unapaswa kufanya.

By | January 10, 2023

2932; Ndiyo maana unapaswa kufanya. Rafiki yangu mpendwa, Pata picha umemwajiri mtu afanye kazi fulani. Baada ya kumpa majukumu hayo ya kazi, anakuambia hii kazi ni ngumu sana. Hiyo ni kweli, kazi hiyo itakuwa ngumu ndiyo maana ukatafuta mtu wa kuifanya. Maana kama ingekuwa rahisi, ungeifanya wewe mwenyewe. Upande wa (more…)

2931; Utupu hujazwa.

By | January 9, 2023

2931; Utupu hujazwa. Rafiki yangu mpendwa, Asili huwa haipendi utupu. Popote panapokuwa na utupu, asili huwa inakazana kupajaza kwa haraka sana. Kama umewahi kupangilia eneo fulani vizuri na ukabaki na nafasi, haikuchukua muda nafasi iliyobaki inajaa kwa vitu mbalimbali. Kama umelima shamba na hukupanda chochote, magugu hupanda kwa wingi bila (more…)

2930; Kokotoa thamani ya muda wako.

By | January 8, 2023

2930; Kokotoa thamani ya muda wako. Rafiki yangu mpendwa, Kupitia kurasa hizi nilikushirikisha dhana ya kuwa na thamani ya muda wako ili uweze kuutumia vyema. Dhana hiyo ilihusisha kuupa muda thamani ya kifedha ili kutokuupoteza kwa mambo yasiyo na tija. Wengi hawakuelewa jinsi ya kuweza kukokotoa thamani ya muda wao. (more…)

2928; Asiwepo wa kuizidi biashara.

By | January 6, 2023

2928; Asiwepo wa kuizidi biashara. Rafiki yangu mpendwa, Matatizo mengi ya kibiashara yamekuwa yanaanzia pale mfanyabiashara anaposhindwa kujitofautisha yeye na biashara yake. Waanzilishi wengi wa biashara huwa wanadhani wao na biashara zao ni kitu kimoja. Na hilo limekuwa linapelekea wafanye maamuzi ambayo yanaiathiri sana biashara. Kosa kubwa wanalofanya ni kuifanya (more…)

2927; Nitavumilia matokeo, siyo mchakato.

By | January 5, 2023

2927; Nitavumilia matokeo, siyo mchakato. Rafiki yangu mpendwa, Kwenye maisha kuna mambo mawili makubwa; mchakato na matokeo. Mchakato ni yale unayofanya, hatua unazochukua kwenye kila jambo. Matokeo ni kile kinachokuja kupatikana kutokana na hatua zinazokuwa zimechukuliwa. Mchakato upo ndani ya uwezo wa mtu. Mtu ana uwezo wa kuamua nini afanye (more…)

2926; Nipe masaa yangu 16.

By | January 4, 2023

2926; Nipe masaa yangu 16. Rafiki yangu mpendwa, Utakumbuka kwenye ukurasa wa 2926 nilikueleza kwa kina uhusiano wangu mimi na wewe na namna tunavyokwenda. Kwenye vipengele 10 nilivyoeleza, kipengele namba 7 kilieleza kwamba mimi ni meneja wako. Meneja wako kwenye masomo, mauzo na mafunzo. Wajibu wa meneja ni kuhakikisha mambo (more…)