Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2872; Tuongelee hili swala la uvivu.

By | November 11, 2022

2872; Tuongelee hili swala la uvivu. Kwako rafiki yangu unayedhani unaweka juhudi kubwa kwenye kazi, lakini hakuna matokeo mazuri unayoyapata. Watu wengi wamekuwa wakichanganya kushughulika na kuzalisha. Huwa wanadhani kwa kushughulika ndiyo wanajituma hasa. Lakini unapoyaangalia matokeo wanayozalisha, unaona kabisa kwamba hayaendani na kile wanachodai. Mtu anakuwa yupo bize kweli (more…)

2870; Haifanyi kazi.

By | November 9, 2022

2870; Haifanyi kazi. Kwako rafiki yangu mpendwa, ambaye umekuwa unatafuta njia ya uhakika na inayofanya kazi. Umekuwa unajaribu njia mbalimbali, lakini zote umekuwa unaishia njiani kwa sababu hazifanyi kazi. Wakati unaanza kutumia njia mpya, unakuwa na imani na matumaini makubwa kwamba italeta matokeo makubwa na mazuri. Ni pale unapoendelea kutumia (more…)

2868; Mwisho wa changamoto.

By | November 7, 2022

2868; Mwisho wa changamoto. Kwako rafiki yangu ambaye unatamani siku moja usingewe na changamoto kabisa. Umechoshwa na hali ya kila wakati kuwa na changamoto ambayo unakabiliana nayo. Ukitatua changamoto moja, inaibuka nyingine kubwa zaidi ya hiyo ya awali. Rafiki, unapaswa kujua kwamba mwisho wa changamoto ni kifo. Kama bado upo (more…)

2867; Asili ya binadamu.

By | November 6, 2022

2867; Asili ya binadamu. Kwako rafiki yangu ambaye umedhamiria kuwabadili watu. Nia yako ni njema kabisa, kwa sababu namna watu walivyo inaweza kuwa kikwazo kwao na hata kwako kufanikiwa. Lakini wajibu huo uliojipa ni mkubwa sana na ambao hauwezekani. Najua hili litakushangaza, hasa kwa kuwa nimekuwa nakuambia hakuna kisichowezekana. Lakini (more…)

2866; Kutokufanya maamuzi thabiti.

By | November 5, 2022

2866; Kutokufanya maamuzi thabiti. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye kila ukianzisha jambo linaishia njiani. Unaweza kujipa sababu nyingi zinazopelekea hilo kutokea. Na sababu hizo nyingi zitakuwa ni za nje. Lakini sababu moja kubwa hutaipa uzito, sababu ambayo inaanzia ndani yako mwenyewe. Sababu hiyo ni kutokufanya maamuzi thabiti. Neno maamuzi limekuwa (more…)

2865; Hupati matokeo.

By | November 4, 2022

2865; Hupati matokeo. Kwako rafiki yangu unayesema hupati matokeo licha ya kuweka juhudi kubwa sana. Unaona kabisa kwamba umeweka juhudi kubwa, lakini inapokuja kwenye matokeo, yanakuwa tofauti kabisa na ulivyotarajia. Unaweza kudhani labda huna bahati au una bahati mbaya. Unaweza kudhani labda juhudi unazoweka siyo sahihi. Hayo yote siyo kweli. (more…)

2864; Kama kweli unajua.

By | November 3, 2022

2864; Kama kweli unajua. Kwako rafiki yangu unayedhani tayari unajua kila kitu na huhitaji tena kujifunza. Ni kweli unaweza kuwa unajua mengi unayosema unayajua. Lakini je, matokeo unayozalisha yanaendana na hicho unachosema unajua? Maana kama unasema unajua, lakini matokeo unayozalisha ni tofauti na unachosema unajua, kuna tatizo mahali. Huenda hujui (more…)

2863; Kama huuzi unafanya nini?

By | November 2, 2022

2863; Kama huuzi unafanya nini? Kwako rafiki yangu mpendwa uliye kwenye biashara. Unajua kabisa kwamba mauzo ndiyo namba ya kwanza na muhimu kwenye biashara. Unajua bila mauzo hakuna fedha na bila fedha hakuna biashara. Haya yote unayajua bila ya shaka yoyote. Lakini bado huuzi. Je unategemea nini? Unajipa sababu mbalimbali. (more…)

2862; Lazima tuambiane ukweli.

By | November 1, 2022

2862; Lazima tuambiane ukweli. Kwako rafiki yangu unayeyataka mafanikio makubwa, Kuujua ukweli, ambao ni mchungu ni sehemu ya hii safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa. Sababu ya kwanza kwa wengi kushindwa kwenye hii safari ni kutokuukubali ukweli ambao ni mchungu. Mafanikio makubwa yanawezekana kabisa. Lakini yanakutaka ujitoe mzima mzima (more…)