Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2861; Nguvu kubwa kuliko wewe.

By | October 31, 2022

2861; Nguvu kubwa kuliko wewe. Ipo nguvu kubwa kuliko wewe ambayo inauendesha huu ulimwengu. Bado hatuielewi vizuri nguvu hii, hivyi tumekuwa tunaipa majina mbalimbali. Wapo wanaoiita Mungu, wengine wanaiita Asili na mengine. Lakini wote tunakubaliana kwamba ipo nguvu kubwa inayofanya ulimwengu mzima uende unavyoenda. Kuchomoza na kuzama kwa jua, kuonekana (more…)

2859; Zidisha thamani yako.

By | October 29, 2022

2859; Zidisha thamani yako. Zamani watu walikuwa wanalipwa kulingana na muda wanaofanya kazi, hivyo wengi walitengeneza mazingira ya kuonekana wanafanya kazi muda mrefu hata kama haina tija. Siku hizi watu wanalipwa kulingana na thamani wanayoizalisha. Hivyo kama unataka ukipwe zaidi, toa thamani zaidi. Ukizidisha thamani unayoitoa mara 10, utaweza kuongeza (more…)

2858; Icheke dunia.

By | October 28, 2022

2858; Icheke dunia. Katika viumbe wote waliopo hapa duniani, sisi binadamu pekee ndiyo wenye uwezo wa kucheka. Viumbe wote wana uwezo wa kulia, hasa pale wanapokuwa na maumivu mbalimbali. Lakini inapokuja kwenye kucheka, ni sisi binadamu pekee tunaoweza kufanya hivyo. Tumia uwezo huo wa kucheka kuweza kufanya makubwa kwenye maisha (more…)

2857; Tawala hisia zako.

By | October 27, 2022

2857; Tawala hisia zako. Sisi binadamu ni viumbe wa kihisia. Huwa tunafanya maamuzi yetu kwa hisia, kisha tunayahalisha kwa mantiki. Tatizo la hisia huwa hazina msimamo, ni kitu cha kupita kama mawimbi. Pia hisia zinaathiriwa na mambo mbalimbali. Ukiwa mtu unayetawaliwa na hisia, hutaweza kufanya chochote kikubwa kwenye maisha yako. (more…)

2856; Ishi kila siku kama ndiyo siku yako ya mwisho.

By | October 26, 2022

2856; Ishi kila siku kama ndiyo siku yako ya mwisho. Huwa tunaona tuna muda mwingi, mpaka pale tunapokuja kugundua muda wetu umeisha. Ni rahisi kujiambia utafanya kesho, kwa kuwa umezoea kuziona kesho nyingi. Lakini ipo siku ambayo hutaiona kesho uliyopanga. Ubaya ni huwezi kuijua siku hiyo ni ipi. Lakini uhakika (more…)

2855; Wewe ni miujiza.

By | October 25, 2022

2855; Wewe ni miujiza. Kupatikana kwako ni tukio la miujiza mikubwa. Kukutana kwa wazazi wako, lilikuwa tukio ambalo hakuna aliyelitegemea. Wazazi wako kuamua kufanya mapenzi siku ambayo mimba yako ilitungwa pia ni tukio ambalo huenda lisingetokea. Kama mmoja wao angekuwa amesafiri au kuumwa, siku hiyo zoezi hilo lisingefanyika. Katika mbegu (more…)

2854; Ng’ang’ana mpaka ufanikiwe.

By | October 24, 2022

2854; Ng’ang’ana mpaka ufanikiwe. Wanaofanikiwa na wanaoshindwa wote huanza sawa. Huwa wanaanza na ndoto kubwa walizonazo. Kisha wanachukua hatua kwenye ndoto hizo. Katika kuchukua huko hatua huwa wanakutana na changamoto na vikwazo mbalimbali. Na hapa ndipo wanaofanikiwa na wanaoshindwa wanapotofautiana. Wanaoshindwa huwa wanakata tamaa haraka pale wanapokutana na vikwazo na (more…)

2853; Ipokee kila siku kwa upendo.

By | October 23, 2022

2853; Ipokee kila siku kwa upendo. Upendo ndiyo nguvu kuu inayoiendesha dunia. Upendo ndiyo imani kuu inayowaleta watu wote pamoja. Upendo una nguvu kubwa ya kuleta mapinduzi kwenye maisha ya kila mtu. Ili kufanikiwa, unapaswa kuipokea kila siku kwa upendo mkuu. Unapaswa kuongozwa na upendo kila siku. Upendo unapaswa kuanzia (more…)

2852; Kuwa mtumwa wa tabia nzuri.

By | October 22, 2022

2852; Kuwa mtumwa wa tabia nzuri. Tulipokuwa watoto, tulikuwa watumwa wa hisia. Tuliendeshwa na hisia na kila mara kufanya yale tuliyojisikia kufanya. Tumekuwa watu wazima na sasa tumekuwa watumwa wa tabia. Tumejenga tabia na sasa tabia zinatujenga. Mambo mengi tunayofanya tunayafanya kwa tabia, kwa jinsi ambavyo tumezoea kufanya. Ubaya wa (more…)