Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2851; Uwezo tayari upo, tofauti ni matumizi.

By | October 21, 2022

2851; Uwezo tayari upo, tofauti ni matumizi. Unga wa ngano, unaweza kutengeneza mandazi, chapati, mkate, keki na vingine vingi. Uwezo wote huo tayari upo ndani ya unga, ila matokeo ya mwisho yanategemea jinsi ambacho uwezo huo umetumiwa. Kadhalika kwetu binadamu, chochote ambacho wanadamu wengine wameshaweza kufanya, hata wewe una uwezo (more…)

2850; Ushindi kila siku.

By | October 20, 2022

2850; Ushindi kila siku. Sisi binadamu huwa tunapenda sana ushindi. Ndiyo maana huwa tupo tayari kushindana hata kwenye mambo yasiyokuwa na tija. Ile hali ya kushinda tu inatufanya tujisikie vizuri. Lakini sasa, maisha huwa hayatupi ushindi kirahisi. Huwa yanatupa kila aina ya vikwazo na changamoto ili tu tusipate ushindi. Na (more…)

2849; Watu na matokeo.

By | October 19, 2022

2849; Watu na matokeo. Kama kiongozi, una mambo hayo makubwa mawili ya kuzingatia. Una watu unaowaongoza na kuwasimamia na una matokeo ambayo unapaswa kuyazalisha. Haya mawili yanakwenda pamoja kwa sababu ni watu ndiyo wanaozalisha matokeo unayoyataka. Na hapo ndipo penye mtego mkubwa kwenye uongozi, kwa sababu unahitaji mlinganyo mzuri sana (more…)

2848; Lengo, Sifa, Maboresho.

By | October 18, 2022

2848; Lengo, Sifa, Maboresho. Hivyo ni vitu vitatu vinavyoweza kukufanya kuwa kiongozi bora kabisa kutokea. Ni vitu unavyopaswa kuvifanya kwako na kwa wote unaowaongoza. Kwanza unaanza na lengo, nini hasa unachotaka kupata? Au matokeo gani yanapaswa kupatikana? Lengo lazima liwe wazi na kueleweka na wote wanaohusika. Na liweze kuelezewa kwa (more…)

2847; Kukaa kati.

By | October 17, 2022

2847; Kukaa kati. Dunia inaendeshwa kwa upacha, pande mbili zinazotofautiana. Usiku na mchana. Jinsia ya kike na ya kiume. Juu na chini. Hizo hali zinaeleweka na kutengana wazi. Huwa hazina katikati. Changamoto nyingi kwenye maisha yetu huwa zinatokana na kujaribu kukaa kati. Kushindwa kujitoa kweli kwenye upande mmoja wa kitu. (more…)

2846; Cheza kamari kwako mwenyewe.

By | October 16, 2022

2846; Cheza kamari kwako mwenyewe. ‘Kila kitu kwenye maisha ni kamari….’ Ni kauli wanayopenda kuitumia wale wanaocheza kamari mbalimbali kwa kutegemea kupata matokeo makubwa bila kufanya kazi. Ni kweli kwamba kila kitu kwenye maisha ni kamari, kwa sababu hakuna kitu chochote ambacho kina uhakika wa asilimia 100. Kwa chochote tunachofanya (more…)

2845; Ni kufanya.

By | October 15, 2022

2845; Ni kufanya. Matokeo ni zao la kufanya. Haijalishi una mawazo na nia nzuri kiasi gani, kama hutafanya, hakuna matokeo utakayoyapata. Kuwa chanya au hasi haina maana kama hutafanya. Kipaumbele chako cha kwanza kinapaswa kuwa ni kufanya. Kufanya na kelele huwa haviendi pamoja. Wasiofanya watakuwa na maoni mengi kwako, jinsi (more…)

2844; Shtuka ni mtego.

By | October 14, 2022

2844; Shtuka ni mtego. Huwa kuna kichekesho kinasema ukiona choo kwenye ndoto usikitumie, ni mtego huo. Huenda unakumbuka hili vizuri utotoni, unaota unacheza, unaufurahia mchezo, halafu mkojo unakubana, unaenda kukojoa, unashtuka umekojoa kitandani. Kwenye maisha kuna mitego mingi inayowanasa watu kwa kukosa umakini wa kujua ni mitego. Moja wapo ni (more…)

2843; Kuweka matumaini yako kwa wengine.

By | October 13, 2022

2843; Kuweka matumaini yako kwa wengine. Kuweka matumaini yako kwa wengine ndiyo kitu ambacho kimekuwa kinakuangusha kila mara. Huwa kuna usemi kwamba ndege anapotua kwenye tawi la mti, siyo kwa sababu anaamini tawi hilo ni imara, bali kwa sababu anaamini mabawa yake yanaweza kumrusha. Kama ndege angetua kwenye tawi kwa (more…)

2842; Usitapeliwe tena.

By | October 12, 2022

2842; Usitapeliwe tena. Utapeli hautakuja kuisha duniani kwa sababu tatu; Moja, watu siyo waaminifu. Huwa wapo tayari kutumia njia yoyote hata isiyokuwa halali ili tu kupata wanachotaka. Mbili, watu hawapendi kufanya kazi. Hivyo hutafuta njia ya mkato ya kupata wanachotaka bila kuweka kazi. Tatu, watu wanapenda kufuata mkumbo. Wakiona wengi (more…)