Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2841; Uchawi na ushirikina.

By | October 11, 2022

2841; Uchawi na ushirikina. Hadithi tulizokuwa tunajifunza utotoni zilikuwa na maana kubwa ambayo haikuwa rahisi kwa akili zetu za utoto kung’amua. Moja ya hadithi hizo ni SIZITAKI MBICHI HIZI. Kama unakumbuka, sungura aliona ndizi na kuzipenda. Akaanza kuzirukia, lakini hakuzifikia. Akaruka na kuruka tena, lakini wapi. Baada ya kuhangaika sana (more…)

2840; Hatupendi mambo magumu.

By | October 10, 2022

2840; Hatupendi mambo magumu. Kitu kimoja kuhusu sisi binadamu ni hiki, huwa hatupendi mambo magumu. Huwa tunapenda mambo rahisi kuyaelewa na kufanyia kazi. Na ndiyo maana matapeli huwa wana ushawishi mkubwa kwa watu. Kwa sababu huwa wanaelezea mambo kwa urahisi kabisa ambao mtu anaelewa. Ndiyo maana pia mambo yanayohusu burudani (more…)

2839; Kukosa cha kufanya.

By | October 9, 2022

2839; Kukosa cha kufanya. Watu huwa wanapoteza muda kwa sababu wanakuwa hawana kitu kingine cha kufanya. Wengine wanatengeneza hata matatizo kwa sababu tu hawana cha kufanya. Kikubwa ambacho naendelea kujifunza kwenye maisha yetu wanadamu ni kwamba muda hauwezi kukaa mtupu, lazima kuna kitu kitajipenyeza tu. Hivyo basi, kama kweli unataka (more…)

2838; Ukishapotea, ni vigumu sana kurudi.

By | October 8, 2022

2838; Ukishapotea, ni vigumu sana kurudi. Kama umeshawahi kwenda mahali usipopajua kwa kufuata ramani ya kwenye simu (google map), unajua jinsi ambavyo unaweza kuwa unazunguka mahali pamoja kwa muda mrefu bila kujua. Hiyo ni kwa sababu ramani hizo zina udhaifu mmoja, kama imekuelekeza ukifika mbele kata kulia, halafu hukukata hapo (more…)

2837; Siyo kwa ajili yako, bali wao.

By | October 7, 2022

2837; Siyo kwa ajili yako, bali wao. Kitu kikubwa ninachoendelea kujifunza kwa kina kabisa kwenye safari ya mafanikio ni kwamba ili ufanikiwe, unapaswa kwenda kinyume kabisa na tabia zetu za asili kama binadamu. Tabia kama uvivu, wivu, chuki, ubinafsi na nyingine, ni sehemu ya asili yetu binadamu. Lakini ukiziendekeza hizo, (more…)

2836; Udhaifu ndiyo uimara.

By | October 6, 2022

2836; Udhaifu ndiyo uimara. Kwa maisha yetu yote tumekuwa tukidanganywa. Tumekuwa tunaambiwa tuyafanyie kazi madhaifu yetu kwa kuyaondoa ili tuwe imara. Hilo linafanyika kwa nia nzuri, ila matokeo yake huwa siyo mazuri. Pale mtu anapohangaika kuondoa madhaifu yake na kuyageuza kuwa uimara, kinachotokea ni madhaifu hayo yanakuwa makubwa na yenye (more…)

2835; TUTATUA TATIZO HILI KWANZA.

By | October 5, 2022

2835; TUTATUA TATIZO HILI KWANZA. ASILIMIA 90 YA MATATIZO ULIYONAYO, YANAWEZA KUTATULIWA NA FEDHA. NA HIYO ASILIMIA 10 AMBAYO HAIWEZI KUTATULIWA NA FEDHA, HUNA CHA KUFANYA. KWA HIYO BASI, TATIZO LAKO KUBWA SIYO MATATIZO ULIYONAYO, BALI NI FEDHA. HIVYO UNA TATIZO MOJA KUBWA LA KUTATUA MBELE YAKO, FEDHA. KAMA BADO (more…)

2834; Mwache akuambie mwenyewe.

By | October 4, 2022

2834; Mwache akuambie mwenyewe. Huwa tunajikatalia mambo mengi sisi wenyewe kuliko tunavyokataliwa na wengine. Ninachoweza kusema kwa uhakika ni kwamba yale hapana za watu ambazo umekuwa unajipa wewe mwenyewe ni nyingi kuliko hapana unazosikia kweli kutoka kwa watu. Yaani majibu unayojipa kwamba watu watakataa kitu fulani kama utawaambia ni mengi (more…)

2832; Gharama ya kuepuka watu wa kawaida.

By | October 2, 2022

2832; Gharama ya kuepuka watu wa kawaida. Ili ufanikiwe, unawahitaji sana watu. Lakini watu hawalingani. Kuna watu wa kawaida, ambao ndiyo wengi. Hawa pia ni rahisi kuwapata. Halafu kuna watu wasio wa kawaida, ambao ni wachache na wagumu kuwapata. Ili upate mafanikio makubwa, unahitaji kuwaepuka watu wa kawaida na kuwapata (more…)