Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2831; Foleni ya kushangaa.

By | October 1, 2022

2831; Foleni ya kushangaa. Siku iliyopita nikiwa barabarani nilikutana na foleni ndefu, ambayo ilituchukua muda. Kwa kuwa halikuwa eneo lililozoeleka kuwa na foleni, nilijiambia patakuwa na ajali mbele ambayo imeziba barabara. Foleni ikasogea, tulipofika sehemu inayosababisha foleni sikuamini macho yangu. Barabara ilikuwa nyeupe kabisa, ila kuna gari ilikuwa imeacha barabara (more…)

2830; Matokeo hayadanganyi.

By | September 30, 2022

2830; Matokeo hayadanganyi. Nimewahi kushirikisha huu mfano, ila nitaurudia tena kwa msisitizo zaidi. Wakati tupo sekondari, mwalimu wetu wa hesabu alikuwa anasahihisha mitihani kwenye majibu tu. Hakuwa anajisumbua kuangalia njia. Wanafunzi tukajadiliana na kuona hilo halipo sawa, hivyo tukamwuliza mwalimu kwa nini hasahihishi njia? Maana anatunyima maksi kwenye njia. Mwalimu (more…)

2829; Kuwaona huruma wasiojionea huruma.

By | September 29, 2022

2829; Kuwaona huruma wasiojionea huruma. Changamoto zetu kubwa kwenye maisha zinatokana na watu. Ni changamoto kubwa kwa sababu tunawahitaji sana watu, lakini ndiyo hivyo wanakuja na mambo yao ambayo yanatupa changamoto. Kwa kuwa tunawahitaji sana watu, kuna wakati tunakuwa hatutaki kuwapoteza, hivyo licha ya chagamoto wanazosababisha, tunaendelea kuwa nao. Na (more…)

2828; Mteja mpya rahisi kumpata.

By | September 28, 2022

2828; Mteja mpya rahisi kumpata. Hakuna kitu kigumu kwenye biashara kama kupata mteja mpya. Kutokana na kudanganywa na kuumizwa kwa muda mrefu, wateja wana wasiwasi sana na biashara mpya kwao. Ahadi nyingi unazowapa wanakuwa hawana uhakika kama kweli zitatimia. Hilo ndiyo limekuwa linasababisha wasiwe tayari kununua, licha ya kuwa kuwapa (more…)

2827; Ung’ang’anizi na upinzani.

By | September 27, 2022

2827; Ung’ang’anizi na upinzani. Hakuna chochote unachokitaka kwenye maisha yako ambacho utakipata kwa urahisi. Chochote kile unachokitaka, dunia itakuwekea upinzani mkali kwenye kukipata. Dunia itahakikisha inakuwekea kila aina ya kikwazo, mradi tu usipate unachotaka. Njia pekee ya kuvuka upinzani wa dunia ni kuwa na ung’ang’anizi usiokuwa na kikomo. Unapaswa kuwa (more…)

2826; Mkato mzuri.

By | September 26, 2022

2826; Mkato mzuri. Njia za mkato huwa siyo nzuri kwenye maisha. Kwani zimekuwa ndiyo chanzo cha wengi kukosa yale wanayotaka. Watu wamekuwa wanahangaika na njia nyingi za mkato, lakini wanaishia kupoteza muda, nguvu na hata fedha. Huwa kuna usemi lifti ya kuelekea kwenye mafanikio imeharibika, inabidi upande ngazi. Lakini kuna (more…)

2825; Unamtoa mtu.

By | September 25, 2022

2825; Unamtoa mtu. Kwenye maisha, kila mtu tayari ana mtu wake. Hivyo unapotaka kupata mtu, inabidi uwe tayari kumtoa aliyepo. Twende kwenye mfano ili tuelewane. Kama upo kwenye biashara, wateja unaowalenga tayari wana pengine wanaponunua hicho unachouza. Ili uwapate waje kununua kwako, lazima uwatoe kule walipo sasa. Siyo rahisi kumtoa (more…)

2824; Hakuna kushindwa.

By | September 24, 2022

2824; Hakuna kushindwa. Kitu kinachoitwa kwenye maisha hakipo kiuhalisia. Bali ni msamiati ulitengenezwa na jamii ili kuwadhibiti watu. Tunapoiangalia asili kwa namna inavyofanya kazi, tunaona wazi kabisa kushindwa hakupo. Kwenye eneo moja, panda mbegu za papai na embe. Siku chache mbegu za papai zitakuwa zimeota, ila mbegu za embe zitakuwa (more…)

2823; Tayari najua.

By | September 23, 2022

2823; Tayari najua. Hayo ni maneno ambayo yamewapoteza wengi sana na kuwazuia wasifanikiwe. Ni maneno ambayo yamewazuia wengi wasiendelee kujifunza na kuwa bora zaidi. Kila mtu hudhani tayari anajua mengi, lakini kiuhalisia hana uelewa kama anavyodhani anao. Kujifunza kitu chochote kile, kunahitaji marudio ya muda mrefu. Hata pale unapodhani tayari (more…)

2822; Umalaya wa fursa.

By | September 22, 2022

2822; Umalaya wa fursa. Richard Branson amewahi kunukuliwa akisema fursa za biashara ni kama daladala, ukikosa moja, kuna jingine linakuja. Kwa maana rahisi ni kwamba fursa ni nyingi na haziishi. Lakini wanachokifanya walio wengi ni kutaka kupanda kila daladala. Pata picha umeenda kituo cha daladala, ikaja daladala ukaipanda, lakini kabla (more…)