Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2821; Kila mtu anafanya.

By | September 21, 2022

2821; Kila mtu anafanya. Sababu ya hovyo kabisa ya kufanya kitu ni kila mtu kuwa anakifanya. Sisi binadamu kama viumbe wa kimamii huwa tunapenda sana kufuata mkumbo. Lakini tuanze tu kwa kuuangalia ukweli ulivyo. Watu wengi kwenye jamii hawafanikiwi. Kwa kuwa wale tunaojihusisha nao wana ushawishi mkubwa kwetu, tunapaswa kuwaepuka (more…)

2819; Umechagua mwenyewe.

By | September 19, 2022

2819; Umechagua mwenyewe. Hakuna jambo linaloshangaza kwenye maisha kama hili, watu kulalamikia na kulaumu wengine kwa machaguo yao wenyewe. Kwa zama tunazoishi sasa, hakuna yeyote anayekulazimisha kufanya chochote. Ni wewe mwenyewe umechagua. Chukua mfano wa mtu anayefanya kazi na analipwa mshahara kidogo. Anaweza kumlaumu mwajiri wake kwa kutokumjali, lakini hayo (more…)

2818; Mwenza, roho mbaya au utegemezi.

By | September 18, 2022

2818; Mwenza, roho mbaya au utegemezi. Kuanzisha biashara na kuikuza mpaka ifikie mafanikio makubwa ni kitu kigumu sana kufanya, lakini ambacho kinawezekana kwa uhakika. Hatari kubwa na ya kwanza kwenye biashara ni kufa. Takwimu zinaonyesha biashara nyingi sana huwa zinakufa kwenye hatua ya uchanga. Zaidi ya asilimia 80 ya biashara (more…)

2817; Uwajibikaji na Mchakato.

By | September 17, 2022

2817; Uwajibikaji na Mchakato. Unataka kufanikiwa? 1. Jua unachotaka. 2. Panga jinsi ya kukipata. 3. Chukua hatua. 4. Kaa kwenye mchakato. 5. Wajibika. Unaanza kwa kujua nini unachotaka kwa uhakika kabisa. Mafanikio kwako yana maana gani? Hili lazima lianzie ndani yako, kwa kujisikiliza wewe mwenyewe. Unaweza kushangaa, lakini ukweli ni (more…)

2816; Kuhimili mikiki mikiki.

By | September 16, 2022

2816; Kuhimili mikiki mikiki. Huwa kuna kichekesho ambapo mtu anasema kila akipata ufunguo wa mafanikio, anakuta kitasa kimebadilishwa. Hivyo inabidi aanze kutafuta tena ufunguo mwingine. Na akiupata tu, vitasa vinabadilishwa tena. Sijui kama umeipata picha hapo, maana huo ndiyo uhalisia kamili wa maisha yetu. Tunaweza kupambana sana ili kupata kitu (more…)

2814; Acha kujikwamisha.

By | September 14, 2022

2814; Acha kujikwamisha. Ni jambo la kushangaza, lakini ndivyo uhalisia ulivyo, umekuwa unajikwamisha sana wewe mwenyewe. Pale mambo yanapokwenda vizuri kabisa kwa upande wako, unayaingilia na kuyavuruga. Unaharibu kile ambacho tayari kilishakuwa cha uhakika kwa kushindwa tu kuwa na utulivu na msimamo. Kutaka kwako vitu vipya na vinavyosisimua kunakufanya uharibu (more…)

2813; Kwanza umefanya?

By | September 13, 2022

2813; Kwanza umefanya? Huwa ni rahisi kuyaangalia matokeo na kukatishwa nayo tamaa pale yanapokuwa tofauti na mategemeo. Lakini mtu unasahau kwamba matokeo yoyote yale huwa hayaji kimiujiza. Bali yanaathiriwa na kile ambacho mtu amefanya. Hivyo kabla hujaumizwa na matokeo, kwanza jiulize umefanya? Je umefanya kile unachopaswa kufanya? Kama jibu ni (more…)

2812; Kwanza umefanya?

By | September 12, 2022

2812; Kwanza umefanya? Hakuna kitu kinashangaza kama pale mtu anajua anachopaswa kufanya, ila hakifanyi, halafu analalamika kwa kukosa matokeo aliyotegemea. Hakuna namna matokeo yoyote yatakuja kimiujiza kwako bila ya kuchukua hatua na kufanya. Ukiangalia kila matokeo ambayo unayapata kwenye maisha yako, yanaendana kabisa na hatua ambazo ulichukua huko nyuma. Kama (more…)