Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2811; Kinachohitajika ni furaha.

By | September 11, 2022

2811; Kinachohitajika ni furaha. Tunahangaika na mambo mengi kwenye maisha yetu. Lakini mwisho wa siku kinachohitajika ni furaha. Huenda hatujui moja kwa moja, lakini kila tunachofanya, msingi wake ni furaha. Sasa kwa kutokujua chanzo sahihi cha furaha, tunajikuta tunajaribu kila aina ya kutu kuona kama kitatupa furaha. Kubahatisha furaha imekuwa (more…)

2810; Usitengeneze majuto.

By | September 10, 2022

2810; Usitengeneze majuto. Unakumbuka ukiwa shuleni, kuna wakati ulikuwa husomi sana na pale matokeo yalipokuwa yanatoka ukawa unajiambia kama ungeweka juhudi zaidi, ungeweza kupata matokeo zaidi? Hiyo ni dhana ambayo wengi wanaondoka nayo shuleni na kwenda nayo kwenye maisha, kitu kinachowazuia wasipate mafanikio makubwa. Kufanya vitu nusu nusu ili ukishindwa (more…)

2809; Rahisi kufanya.

By | September 9, 2022

2809; Rahisi kufanya. Ukichunguza kwa makini, utagundua kwamba matatizo yote ambayo umewahi kuwa nayo kwenye maisha, chanzo chake ni kukimbilia vitu rahisi kufanya. Hii ni asili yetu binadamu, huwa hatupendi vitu vigumu. Hivyo kila mara tunatafuta kilicho rahisi. Na huko pia ndipo tunapotengeneza matatizo mengi tunayokuwa nayo kwenye maksha. Hata (more…)

2808; Kujua hujui.

By | September 8, 2022

2808; Kujua hujui. Kujua hujui ndiyo ujuzi muhimu ambao utakusaidia sana kwenye maisha yako. Utakufanya uwe mnyenyekevu na tayari kujifunza ili kuwa bora zaidi na kuweza kupiga hatua kubwa. Na hili siyo rahisi kukubali na hata kulifanya. Huwa tuna ufahari wa kutaka kuwaonyesha wengine kwamba tunajua. Huwa tunaona kuonekana hatujui (more…)

2807; Unahangaika na mambo mengi sana.

By | September 7, 2022

2807; Unahangaika na mambo mengi sana. Mwanga wa jua, ukitawanyika, unaishia kuangaza tu. Lakini mwanga huo huo ukikusanywa sehemu moja, unakuwa na nguvu ya kuchoma. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye nguvu zetu binafsi, tukizitawanya kwenye mambo mengi, tunaishia kupata matokeo ya kawaida. Lakini tukikusanya nguvu hizo kwenye jambo moja au (more…)

2805; Kujifunza na kazi.

By | September 5, 2022

2805; Kujifunza na kazi. Kama mtu yeyote akiniuliza ni vitu gani afanye ambavyo vitampa mafanikio kwa uhakika, bila ya kusita hata sekunde moja nitamjibu kujifunza na kazi. Kujifunza kwa kina na endelevu kwenye kile ambacho mtu unafanya ni hitaji muhimu sana ili kufanikiwa. Unapaswa kukijua kweli chochote unachofanya, maana hivyo (more…)

2804; Hakuna kushindwa.

By | September 4, 2022

2804; Hakuna kushindwa. Watu wengi hudhani pale wanapokutana na changamoto na vikwazo mbalimbali basi wameshindwa. Kwenye safari ya mafanikio, kushindwa ni pale unapokuwa umekata tamaa na kuacha kufanya. Hapo ndiyo unakuwa umeshindwa kwa sababu kama umeacha kufanya, umeondoa nafasi zote za kuweza kupata matokeo mazuri. Lakini kama unaendelea kufanya licha (more…)

2803; Usitafute fursa, jitafute wewe.

By | September 3, 2022

2803; Usitafute fursa, jitafute wewe. Kama bado unatafuta fursa, tatizo siyo fursa hazipatikani, tatizo ni wewe bado hujajijua vizuri. Na kama umeshajijua basi hujajitumia ipasavyo. Fursa hazitafutwi, maana hazijawahi kupotea, wala hazijajificha. Fursa zinajidhihirisha, pale unapokuwa mtu sahihi, kwenye eneo sahihi na wakati sahihi. Hivyo kama bado hujapata fursa nzuri (more…)

2802; Wape wanachotaka.

By | September 2, 2022

2802; Wape wanachotaka. Naweza kusema kwenye haya maisha kama hujafanikiwa, chanzo kikubwa ni ubinafsi. Kwenye maisha unashindwa pale unapojiangalia wewe mwenyewe zaidi ya unavyowaangalia wengine. Pale unapoweka maslahi yako mbele na kupuuza ya wengine. Utakazana sana kupata unachotaka, lakini hutakipata. Kwa sababu kanuni za asili haziendi hivyo. Huwezi kuziambia kuni (more…)