Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2792; Umewafundisha?

By | August 23, 2022

2792; Umewafundisha? Kama watu hawafanyi kitu, kuna sababu mbili tu; HAWAWEZI au HAWATAKI. Wanakuwa hawawezi pale wanapokuwa hawajui jinsi ya kufanya kitu hicho. Hilo linakuwa gumu kwao kufanya. Na mbaya zaidi, watu huwa hawapendi kukiri kwamba hawajui. Hivyo hujifanya wanajua, lakini kutokujua kwao kunakuwa kikwazo kwenye ufanyaji. Hapo hujaweka hali (more…)

2791; Uwanja wa nyumbani.

By | August 22, 2022

2791; Uwanja wa nyumbani. Kwenye michezo yote, huwa kuna dhana ya uwanja wa nyumbani. Kwamba timu inakuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda inapokuwa inacheza kwenye uwanja wa nyumbani. Hivyo timu inapokuwa inacheza uwanja wa ugenini, huko hucheza kwa kujilinda zaidi ili isifungwe. Timu ikiwa ugenini haiangalii sana kusinda, bali inakazana (more…)

2790; Kuna anayeweza kununua kwako?

By | August 21, 2022

2790; Kuna anayeweza kununua kwako? Hivi karibuni nilikutana na ujumbe unaozunguka mtandaoni unaosema kampuni ya magari ya Lamboghini (moja ya magari ya bei ghali zaidi) huwa haijitangazi kwenye tv kwa sababu watu wanaoweza kumudu kununua aina hiyo ya magari, hutawakuta wamekaa wanaangalia tv. Ujumbe huo unaweza kuchukuliwa kama kichekesho, lakini (more…)

2788; Usiage mashindano.

By | August 19, 2022

2788; Usiage mashindano. Fikiria timu yako unayoipenda ya mpira wa miguu. Imeingia uwanjani kushindana na timu nyingine. Dakika tano tu za kwanza za mchezo, timu yako inafungwa goli moja. Cha kushangaza sasa, baada ya kufungwa goli hilo moja, wachezaji wote wanaamu kuondoka uwanjani. Wanajiona hawafai kabisa, wamefungwa haraka na hawana (more…)

2787; Jipe uhakika mwenyewe.

By | August 18, 2022

2787; Jipe uhakika mwenyewe. Kitu kimoja kinachotukwamisha sana kwenye maisha ni kukosa uhakika. Hilo ndiyo limekuwa linatuzuia kufanya maamuzi na hata tukifanya maamuzi tunashindwa kuyasimamia. Kwa mfano nikikupa wateja 10 ambao kwa uhakika watanunua kwako, ila wanachosubiri ni wewe uwatembelee, utafanya kila namna kuwatembelea. Hutakuwa na sababu yoyote ya kukuzuia, (more…)

2786; Hujashindwa, ni uvivu tu.

By | August 17, 2022

2786; Hujashindwa, ni uvivu tu. Rafiki, kama kuna kitu chochote unachojiambia umeshindwa, siyo kweli. Kama bado upo hai, hakuna chochote unachokuwa umeshindwa. Bali unakuwa tu na uvivu wa kuendelea. Kila hadithi ya watu waliofanikiwa ina somo moja kubwa, kufanya kitu mara nyingi na kwa muda mrefu bila kupata matokeo mazuri. (more…)

2785; Kuanza na kuendelea.

By | August 16, 2022

2785; Kuanza na kuendelea. Mashine yoyote ile, huwa inatumia nishati kubwa zaidi kwenye kuanza kuwaka kuliko kuendelea kuwaka. Chukua mfano wa injini ya gari au ndege, inapowashwa na kuanza safari inatumia mafuta mengi. Lakini baada ya kuwaka na kuwa kwenye mwendo, mafuta yanayohitajika ili kuendelea na mwendo yanakuwa madogo kuliko (more…)

2784; Tatizo ni kujidanganya.

By | August 15, 2022

2784; Tatizo ni kujidanganya. Mwanafizikia Richard Feynman aliwahi kunukuliwa akisema jukumu lako la kwanza kwenye maisha ni kutokujidanganya wewe mwenyewe. Na hakuna mtu rahisi kumdanganya kama wewe mwenyewe. Kauli hiyo ina ukweli mkubwa sana ambao ukiuelewa na kuufanyia kazi hakuna kitu kitakachokushinda kwenye maisha yako. Kitu cha kwanza kabisa unachopaswa (more…)

2783; Haina matumizi.

By | August 14, 2022

2783; Haina matumizi. Kitu chochote kikishakosa matumizi, kinaanza kuharibika. Angalia majengo mazuri ambayo hayatumiki, huwa yanaanza kuharibika vibaya. Kadhalika kwenye vifaa mbalimbali tunavyotumia, kama kifaa hakitumiki kinaanza kuharibika. Tunapata funzo kubwa sana hapa kuhusu maisha ya mafanikio. Kama kuna kitu tunakosa au kushindwa kutumia, inasababishwa na sisi kukosa matumizi na (more…)