Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2782; Anaringa.

By | August 13, 2022

2782; Anaringa. Kwenye maisha, watu wanataka uwe vile wanavyotaka wao, ukiwa tofauti, watakupa kila aina ya shutuma. Lakini sasa, kwenye hii safari ya mafanikio, huwezi kuwa vile ambavyo kila mtu anataka uwe. Badala yake unapaswa kuwa na misingi ambayo unaisimamia wakati wote, hata kama haiwafurahishi wengine. Maana kama kuwafurahisha wengine (more…)

2781; Watu na matatizo yao.

By | August 12, 2022

2781; Watu na matatizo yao. Mtu mmoja alisikia mbwa wa jirani yake akilia kwa uchungu na kwa muda mrefu. Alishindwa kuvumilia na kuamua aende kuangalia nini kinaendelea. Alipofika kwa jirani yake, alimkuta amekaa kwenye bustani yake akisoma gazeti, huku pembeni yake mbwa wake akiwa amekalia msumari ambao unamuumiza ndiyo maana (more…)

2779; Kutokutaka kupitwa.

By | August 10, 2022

2779; Kutokutaka kupitwa. Habari, tv, umbeya, udaku, majungu na mitandao ya kijamii ni vitu ambavyo vimekuwa na nguvu kubwa kwa wengi kwa sababu vinatumia msingi mmoja muhimu; hofu ya kupitwa. Kwa Kiingereza wanaita FOMO (Fear Of Missing Out). Hebu fikiria, kila siku kuna habari mpasuko (breaking news). Unadhani zote hizo (more…)

2778; Itafanyika njia kwa ajili yako.

By | August 9, 2022

2778; Itafanyika njia kwa ajili yako. Ukweli mmoja ambao watu wengi wamekuwa hawaelewi kwenye maisha ni huu, kila mtu huwa anapata kile anachokitaka kweli kwenye maisha yake. Yaani kama kuna kitu ambacho unakitaka sana kwenye maisha yako, na hakuna namna unakubali kutokukipata, basi unakipata. Hata pale inapoonekana hakuna njia kabisa, (more…)

2777; Maji hufuata mkondo wake.

By | August 8, 2022

2777; Maji hufuata mkondo wake. Hii ni kauli rahisi sana ya Waswahili, lakini iliyobeba ujumbe mzito sana. Ni ujumbe ambao ukiweza kuuelewa utajitenganisha kabisa na mambo yanayokuzuia kufanikiwa. Kwenye kitabu cha The Richest Man In Babylon ipo hadithi ya bwana mmoja ambaye hakuwa makini na matumizi ya fedha zake. Alijikuta (more…)

2774; Wanajua usichojua.

By | August 5, 2022

2774; Wanajua usichojua. Watu wote ambao wamefanikiwa zaidi kwenye maisha, kuna vitu ambavyo wanavijua ambavyo wasiofanikiwa hawavijui. Kwa hao waliofanikiwa, wanaweza kuwa wanajua vitu hivyo kwa sababu ndivyo mtazamo wao ulivyo au kwa sababu wamepata nafasi ya kujifunza vitu vya tofauti. Hivi karibuni nimesoma mahojiano ya msanifu majengo mkubwa, Frank (more…)

2773; Usichokitaka.

By | August 4, 2022

2773; Usichokitaka. Kama kuna kitu ambacho hukitaki kwenye maisha yako, dawa yake ni kukipuuza. Hapaswi kupambana na chochote ambacho hukitaki. Kwa sababu kwenye kupambana na kitu, unakipa nguvu zaidi na hivyo kuishia kushindwa. Njia ya uhakika na ya ushindi ni kupuuza kile ambacho hukitaki. Kuchukulia kama vile hakipo na hukihitaji (more…)