Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2772; Uzuri wa ukweli.

By | August 3, 2022

2772; Uzuri wa ukweli. Uzuri wa kusema ukweli ni kwamba huhitaji kuweka kumbukumbu yoyote ile kwenye yale unayoongea. Kwa sababu ukweli hubaki hivyo daima, huhitaji kujiuliza mara mbili mbili kabla ya kusema kitu. Unaposema uongo inabidi uwe na kumbukumbu nzuri ili kukumbuka yote ambayo umeshayadanganya kuepuka kusema kitu cha tofauti. (more…)

2770; Lazima uwaamini watu.

By | August 1, 2022

2770; Lazima uwaamini watu. Jamii zote zimejengwa kwenye msingi wa kuaminiana. Ni pale watu wanapoaminiana ndiyo jamii inakuwa imara na watu kufanikiwa. Na pale imani baina ya watu inapokosekana, jamii inakuwa dhaifu na watu kushindwa. Ni imani kwa wengine kwamba wanajua wanachofanya na wana nia njema ndiyo inafanya kila jamii (more…)

2769; Mtego wa mafanikio.

By | July 31, 2022

2769; Mtego wa mafanikio. Watu wengi huwa wanashangazwa na hili; kuna watu wanaanzia chini kabisa, wanapambana kweli kweli na kuyapata mafanikio makubwa, kisha wanaanguka. Hilo limekuwa linaonekana kwa wengi wanaoanzia chini, kupanda juu, kisha kushuka tena chini. Hali hiyo imekuwa ikisababishwa na mtego wa mafanikio ambao wengi wamekuwa hawauelewi. Mtego (more…)

2767; Wanaheshimu unachokagua.

By | July 29, 2022

2767; Wanaheshimu unachokagua. Umewahi kukubaliana kitu na mtu, kuhusu mambo anayopaswa kubadili. Anakubali kabisa na anaanza kubadilika. Lakini baada ya muda mfupi anarudi kule kule alikotoka. Anayaacha mabadiliko na kurudi kwenye mazoea. Unaweza kushangazwa na kuumizwa na hali ya aina hiyo. Iweje mtu akubali kitu halafu baadaye abadilike? Ambacho huelewi (more…)

2766; Watu wasiokuheshimu.

By | July 28, 2022

2766; Watu wasiokuheshimu. Mtu mmoja amewahi kusema kwamba watu wengi kwenye maisha wanatumia fedha ambazo hawana, kununua vitu ambavyo hawavihitaji ili kuwaridhisha watu ambao hawajali. Fikiria mtu anayekopa fedha, ili kununua gari ya kifahari kwa sababu anataka aonekane na wengine. Naweza kwenda mbali zaidi na kusema matatizo mengi kwenye maisha (more…)

2764; Wimbo unaoupenda sana.

By | July 26, 2022

2764; Wimbo unaoupenda sana. Rafiki, hebu fikiria wimbo mmoja ambao unaupenda sana. Tena hebu uimbe kidogo wimbo huo. Unaujua kwa hakika mashairi yake yote. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa baadhi ya matangazo ya biashara. Kuna baadhi ya matangazo ambayo umekuwa unayapenda sana na unayajua maelezo yake yote. Sasa nina swali (more…)

2763; Hakuna anayekuangusha.

By | July 25, 2022

2763; Hakuna anayekuangusha. Ni rahisi sana kulaumu wengine kwamba wanakuangusha au kukukwamisha. Lakini nataka nikuhakikishie kitu kimoja, hakuna yeyote anayekukwamisha au kukuangusha. Bali hayo yote unajifanyia wewe mwenyewe. Kama hujapata au kufika kule unakotaka kufika, hakuna mwingine yeyote ambaye anakuzuia isipokuwa wewe mwenyewe. Siyo wazazi, mwenza, serikali, uchumi au mazingira (more…)