Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2762; Kujiandaa kuishi.

By | July 24, 2022

2762; Kujiandaa kuishi. Watu wengi huwa wanayamaliza maisha yao hapa duniani kabla hata hawajaanza kuishi. Kila wakati wanakuwa wanajiandaa kuanza kuishi. Hatimaye mauti yanawafika kabla hata hawajawa tayari kuishi. Ukifuatilia maisha ya wengi, na huenda hata ya kwako binafsi, hilo lipo dhahiri kabisa. Wakati mtu akiwa mtoto, anaenda shule kujiandaa (more…)

2761; Unajitofautishaje na wengine?

By | July 23, 2022

2761; Unajitofautishaje na wengine? Unajua ninj rafiki yangu, Neno siri za mafanikio limewanufaisha sana wengi. Kuna wengi ambao wameweza kuingiza kipato kikubwa kwa kuwaambia wengine kwamba wanazo siri za mafanikio. Sasa kwa sababu jamii kwa ujumla haiyaelewi mafanikio, hunasa kwenye huo mtego. Kwa kuamini kutakuwa na siri za mafanikio ndiyo (more…)

2760; Mipango haifanyiki uwanjani.

By | July 22, 2022

2760; Mipango haifanyiki uwanjani. Hebu fikiria timu ya mpira imeingia uwanjani kwa ajili ya mchezo wa fainali. Wakati mashabiki wanaishangilia timu hiyo na kutegemea makubwa, kocha ndiyo anawakusanya wachezaji na kuwauliza tutumie mbinu gani kushinda? Unajua kabisa timu ya aina hiyo itakuwa kwenye matatizo makubwa. Kwani wakati wa mapambano siyo (more…)

2759; Ninakuhitahu zaidi wakati una matatizo.

By | July 21, 2022

2759; Ninakuhitahu zaidi wakati una matatizo. Kitu kimoja ambacho nimeendelea kujifunza kwenye huduma ya ukocha ninayotoa ni pale ambapo watu wanaihitaji zaidi huduma yangu ndipo wanaikimbia. Pale mtu anapojikuta kwenye matatizo na changamoto kubwa, ndiyo unapaswa kuwa wakati mzuri kwake kutumia huduma ya ukocha kuvuka hilo. Lakini badala yake wengi (more…)

2757; Kuwepo na kutumika.

By | July 19, 2022

2757; Kuwepo na kutumika. Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa siyo kuwepo au kutokuwepo kwa vitu fulani, bali kutumika au kutokutumika kwa vitu hivyo. Kwa mfano wale waliofanikiwa huwa wanatumia uwezo mkubwa ulio ndani yao. Hiyo haimaanishi kwamba wanaoshindwa hawana uwezo mkubwa ndani yao. Wanao sana, ila kinachowakwamisha ni kutokuutumia. Na mara (more…)

2756; Unakulaje chakula kitamu?

By | July 18, 2022

2756; Unakulaje chakula kitamu? Rafiki, kipi huwa ni chakula kitamu kwako na unachokipenda sana? Je wakati wa kula chakula hicho huwa unaharakisha ukimalize haraka? Upi ni mchezo au burudani unayopenda kufuatilia sana? Je wakati unafuatilia mchezo au burudani hiyo huwa unataka kuharakisha ili kumaliza haraka? Na je ni watu gani (more…)

2755; Unakimbilia wapi?

By | July 17, 2022

2755; Unakimbilia wapi? Hebu pata picha unapita njiani na kukutana na mtu unayemfahamu, anatembea kwa haraka sana. Unamsimamisha ili kumsalimia anakujibu kwa haraka na kuendelea na kasi yako, anakuambia anataka kuwahi. Unamuuliza kwani unawahi wapi? Anakujibu hata sijui, ila nataka tu kuwahi. Je utamwelewaje mtu wa aina hii? Ni dhahiri (more…)

2754; Muda wa kazi na muda unaofanya kazi.

By | July 16, 2022

2754; Muda wa kazi na muda unaofanya kazi. Hakuna eneo ambalo watu wengi huwa wanajidanganya kama kwenye muda. Na usipokuwa mkweli kwenye muda wako mwenyewe, hakuna namna unaweza kufanikiwa. Watu wawili, wanaweza kufanya kitu cha aina moja na kuonekana wakiwa na muda unaolingana. Bado mmoja akafanikiwa zaidi ya mwingine. Tofauti (more…)