Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2752; Niseme vibaya kwenye mengine yote, lakini siyo kwenye hiki kimoja.

By | July 14, 2022

2752; Niseme vibaya kwenye mengine yote, lakini siyo kwenye hiki kimoja. Kama binadamu, najua sijakamilika. Nina maeneo ambayo nina uimara mkubwa. Na maeneo ambayo nina udhaifu mkubwa. Najua kuna watu wananisema vibaya kwenye mambo mbalimbali, mengine ya kweli na mengine siyo ya kweli. Wapo wanaoweza kuwa wanasema sijali, nina roho (more…)

2751; Kujua, kuweza na kufanya.

By | July 13, 2022

2751; Kujua, kuweza na kufanya. Kama leo hii, utaacha kabisa kujifunza vitu vipya, yaani usijifunze chochote kipya, ila ukafanyia kazi yale ambayo tayari unayajua, bado utapata mafanikio makubwa sana. Kwa mfano ukaweka juhudi kubwa kwenye kazi/biashara yako kila mara. Ukawa na matumizi madogo kuliko kipato chako na hivyo kuweka akiba (more…)

2750; Siyo pale unapojisikia.

By | July 12, 2022

2750; Siyo pale unapojisikia. Huwezi kufanikiwa kama unafanya vitu pale unapojisikia kufanya. Mafanikio yanataka nidhamu kubwa sana ya kupanga na kufanya iwe unajisikia au la. Na hiyo ndiyo tofauti kuu kati ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa. Wote wanakuwa na ndoto kubwa. Na wote wanaweka mipango ya kufikia ndoto hizo. Ila tofauti (more…)

2749; Kama inabidi ulazimishwe, kuna tatizo.

By | July 11, 2022

2749; Kama inabidi ulazimishwe, kuna tatizo. Siku za karibuni nilikuwa naangalia mahojiano ya aliyekuwa mchezaji bora kabisa wa mpira wa kikapu Kobe Brayant. Aliulizwa yeye kama kiongozi alikuwa anawasukumaje wachezaji wenzake ili waweze kufanya vizuri kama timu. Jibu ambalo Kobe alitoa lilinifikirisha sana na nikaona siyo tu kwenye michezo, bali (more…)

2746; Kutamani, kupanga na kufanya.

By | July 8, 2022

2746; Kutamani, kupanga na kufanya. Matamanio ni bure kabisa, kila mtu huwa anatamani kuwa na vitu vizuri. Ni matamanio ya kila binadamu kupata mafanikio makubwa. Kupanga ni rahisi, watu wengi huwa wanaweka mipango mizuri kabisa ya kupata kile wanachotamani. Wanakuwa wanajua nini wanapaswa kufanya ili kupata wanachotaka. Tatizo kubwa lipo (more…)

2745; Atatenganishwa na fedha zake.

By | July 7, 2022

2745; Atatenganishwa na fedha zake. Mteja yeyote yule, huwa anakutana na watu wa mauzo ambao hufanikiwa kumtenganisha na fedha zake. Mteja akiwa na fedha, kuna namna ambavyo atashawishika na watu wa mauzo na kununua vitu ambavyo hata hakuwa na uhitaji navyo. Ndiyo maana wengi wakiwa hawana fedha wanakuwa na mawazo (more…)

2744; Usichoambiwa kuhusu mauzo.

By | July 6, 2022

2744; Usichoambiwa kuhusu mauzo. Kitu kimoja ambacho watu wengi huwa hawaelewi kwa uhalisia kwenye mauzo ni kwamba mara nyingi wateja huwa wanakudanganya. Na wanafanya hivyo kwa nia njema kabisa ya kutokutaka kukuumiza. Lakini wanaishia kukuumiza zaidi kwa kutokununua kwako. Mapingamizi mengi ambayo mteja anakupa siyo halisi, hasa kwenye pingamizi la (more…)