Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2747; Hawaoni unachoona.

By | July 4, 2022

2742; Hawaoni unachoona. Kuna mahali unayaona maisha yako yakiwa yamefika. Hakuna mwingine yeyote mwenye maono ya aina hiyo. Watu wengine wanapokushauri, hawakushauri kulingana n maono makubwa uliyonayo ndani yako. Bali wanakushauri kwa vile wanavyoona itakupendeza zaidi. Lakini siyo kinachokupendeza ndiyo chenye manufaa kwako. Bali kile kinachoendana na maono makubwa uliyonayo (more…)

2740; Wanataka kukutumia.

By | July 2, 2022

2740; Wanataka kukutumia. Baadhi ya mambo ambayo tumekuwa tunajifunza kuhusu binadamu ni ubinafsi na maslahi. Huwa tuna ubinafsi mkubwa na kujali zaidi maslahi yetu wenyewe. Na hilo ndiyo linawafanya watu kuwa tayari kuwatumia wengine pale wanapoona kuna maslahi mazuri kwa ajili yao. Hivyo lazima ujue kwenye mahusiano yako mengi na (more…)

2738; Siyo lazima ufanye.

By | June 30, 2022

2738; Siyo lazima ufanye. Sehemu kubwa ya msongo tunaokuwa nao kwenye maisha huwa ni wa kujitakia. Tunakuwa na msongo pale tunapoona kwamba ni lazima tufanye vitu fulani ambavyo tumejiambia tunapaswa kufanya. Ukweli ni kwamba hulazimiki kufanya kitu chochote kile. Mahangaiko unayokuwa nayo kwenye kujilazimisha kufanya vitu, ni kujipa tu umaarufu (more…)

2737; Hakuna ambacho umewahi kufanya mara moja ukawa umemaliza.

By | June 29, 2022

2737; Hakuna ambacho umewahi kufanya mara moja ukawa umemaliza. Unakula chakula kila siku, Hakuna kitu unaweza kula mara moja na kuwa umeshiba milele. Unasafisha mwili wako kila siku. Hakuna namna ya kuusafisha mara moja na ukawa msafi milele. Ukitaka kupungua uzito unafanya mazoezi kila siku. Ukitaka kupata utajiri unaongeza kipato (more…)

2736; Kujitoa nusu haisaidii.

By | June 28, 2022

2736; Kujitoa nusu haisaidii. Maandiko ya dini yanaeleza wazi kwamba ni bora kuwa moto au baridi, lakini siyo kuwa vuguvugu. Kuwa vugu vugu hakukuweki kwenye upande wowote wa uhakika hivyo hunufaiki kwa namna yoyote ile. Utanufaika zaidi kwa kujitoa kweli kweli kwenye upande mmoja, kuliko kujaribu kuwa kwenye kila upande. (more…)

2735; Maana halisi ya kufokasi.

By | June 27, 2022

2735; Maana halisi ya kufokasi. Steve Jobs aliwahi kutoa hotuba iliyopendwa na wengi sana ambapo alieleza kwa ufupi sana kwamba maana halisi ya kufokasi ni kusema HAPANA. Haijalishi unafanya nini, kila mara utakuwa na machaguo mengi mbele yako. Kila mara kuna vitu vizuri vitakuja. Kuna fursa ambazo utaona hazipaswi kukupita. (more…)

2734; Kama ungekuwa huogopi chochote.

By | June 26, 2022

2734; Kama ungekuwa huogopi chochote. Sehemu kubwa ya kikwazo cha watu kufanikiwa inatokana na woga ambao watu wanao. Watu wanaogopa sana kushindwa, wanaogopa kukataliwa na wanaogopa wengine watawachukuliaje. Kinachotokea ni watu kufanya mambo ambayo ni ya kawaida na yanayoficha woga wao. Na hilo linapelekea washindwe kupata mafanikio makubwa. Ili uweze (more…)

2733; Hakuna kukosea.

By | June 25, 2022

2733; Hakuna kukosea. Kipindi cha nyuma kidogo palikuwa na kichekesho kwamba kulikuwa na bendi ya waimbaji ambao walikuwa wanasafiri kwenda kutoa burudani. Mmoja wa wanamuziki akawa amechomwa na msumari ndani ya gari waliyokuwa wanasafiria. Kwa kuwa aliyechomwa alikuwa muimbaji, aliamua kumwambia dereva kwamba amechomwa na msumari, lakini akamwambia kama vile (more…)