Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2732; Kukosa kwako umakini kunakuumiza.

By | June 24, 2022

2732; Kukosa kwako umakini kunakuumiza. Kiwango chako cha kukosa umakini, kinaiumiza sana biashara yako. Huo ni ujumbe nilioutuma kwa mmoja wetu baada ya kuona kuna mambo ya msingi kabisa yanamsumbua. Nilipozungumza naye, nikagundua tatizo ni kubwa kuliko nilivyokuwa nadhani awali. Na maumivu kwenye biashara yanayosababishwa na kukosekana kwa umakini yalikuwa (more…)

2731; Fanya kazi kwa juhudi na utafanikiwa.

By | June 23, 2022

2731; Fanya kazi kwa juhudi na utafanikiwa. Ipo nukuu moja ya Kiingereza ambayo ilikuwa ikitumiwa na moja ya familia tajiri sana dunian. Nukuu hiyo kwa Kiingereza inasema; Work hard and you will succeed. Ikimaanisha; Fanya kazi kwa juhudi na utafanikiwa. Iko wazi na inaeleweka kabisa, kwamba ukifanya kazi kwa juhudi, (more…)

2730; Sumu inayoua taratibu.

By | June 22, 2022

2730; Sumu inayoua taratibu. Nikikuambia sasa hivi unywe sumu ambayo itakatisha maisha yako mara moja utanishangaa sana. Utaniambia huwezi kufanya hivyo, kwa sababu bado unataka kuishi. Lakini tukikuchunguza kwa kina, kwa namna unavyofanya mambo yako, tunaweza kuona huna tofauti sana na anayetumia sumu. Tofauti pekee ni sumu unayotumia wewe inaua (more…)

2728; Ni wewe umewafundisha.

By | June 20, 2022

2728; Ni wewe umewafundisha. Kwa namna yoyote ile ambayo watu wanakuchukulia, ni wewe mwenyewe umewafundisha wakuchukulie hivyo. Umewapa ruhusa kwamba wanaweza kukuchukulia kwa namna wanavyokuchukulia. Kama watu wanakudharau maana yake umewafundisha wakudharau. Kuna namna umejiweka ambayo inawafanya watu waone ni sawa kukudharau. Kadhalika kama watu wanakuheshimu maana yake umewafundisha hivyo. (more…)

2727; Tengeneza wasiwasi wenye manufaa.

By | June 19, 2022

2727; Tengeneza wasiwasi wenye manufaa. Sisi binadamu mara zote huwa tunakuwa na wasiwasi. Hata kama mambo yako sawa kabisa, huwa hatukosi kitu kinachotupa wasiwasi. Tena pale mambo yanapokuwa sawa ndiyo tunakuwa na wasiwasi mkubwa zaidi. Tukifikiria vipi mambo hayo yakiharibika. Hata kama hakuna tatizo lolote, huwa tunatengeneza matatizo ya kufikirika (more…)

2726; Huhitaji kuvumbua kitu kipya.

By | June 18, 2022

2726; Huhitaji kuvumbua kitu kipya. Kama unatengeneza chombo cha mwendo, tairi inabaki kuwa tairi. Huhitaji kuja na aina mpya ya uvumbuzi wa tairi. Hata utengeneze tairi kwa upya kiasi gani, itabaki kuwa ya duara. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mambo mengi ya maisha yako. Mengi unayopitia kama changamoto au mkwamo (more…)

2725; Una moto kiasi gani?

By | June 17, 2022

2725; Una moto kiasi gani? Dunia inaendeshwa na moto. Mwanga wa jua, ambao ndiyo unafanya maisha yote yawezekane hapa duniani unatokana na moto unaoendelea ndani ya jua. Nyota mbalimbali tunazoziona angani, ni mawe yenye moto na ambayo yapo kwenye kasi kubwa. Moto unasafisha kila kitu. Moto unaimarisha vitu. Moto unateketeza (more…)

2724; Siyo kuanza, bali mwendelezo.

By | June 16, 2022

2724; Siyo kuanza, bali mwendelezo. Ingekuwa kuanza kitu ndiyo mafanikio, kila mtu angekuwa amefanikiwa. Maana karibu kila mtu alishaanza kitu fulani kwenye maisha yake. Na watu wengi huwa na shauku na hamasa kubwa pale wanapoanza. Lakini haichukui muda mrefu shauku na hamasa hiyo vinayeyuka na wanakosa msukumo wa kuendelea. Huwezi (more…)

2723; Ukishapanda mbegu.

By | June 15, 2022

2723; Ukishapanda mbegu. Kila mmoja hapa anajua kitu kuhusu kilimo, maana tumepita mazingira ambayo kilimo ni jambo la msingi. Katika kilimo kuna kupanda, kupalilia na kuvuna. Huwezi kuvuna kama hujapanda, hivyo cha msingi kabisa ni kuhakikisha unapanda. Lakini pia unapopanda, huwezi kutegemea kuvuna hapo hapo. Lazima ujipe muda, uwe na (more…)