Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2722; Wanadanganya, lakini tunawakubali.

By | June 14, 2022

2722; Wanadanganya, lakini tunawakubali. Umewahi kuangalia maigizo au tamthilia mbalimbali. Na katika hizo, kuna ambazo zilinasa hisia zako, ukajikuta ukifurahi na kucheka au kuhuzunika na kulia. Ulijua kabisa kila kilichokuwa kinaonyeshwa kwenye maigizo au tamthilia siyo ukweli. Kama ni mtu amekufa kwenye igizo au tamthilia unajua kabisa kwamba hajafa kweli. (more…)

2720; Unataka au hutaki?

By | June 12, 2022

2720; Unataka au hutaki? Hadithi tulizokuwa tunajifunza utotoni zilikuwa na mafunzo makubwa sana, japo siyo mara zote tuliweza kuyang’amua. Chukua mfano wa hadithi ya sungura na ndizi. Sungura anapita zake, anaziona ndizi, anaona ni nzuri na kujiambia anazitaka. Anaanza kurukia ndizi zile. Anaruka na kuruka tena, Lakini hazifikii ndizi. Anaruka (more…)

2717; Nusu muda, muda kamili na muda wote (au safari ya kuelekea kwenye ubilionea).

By | June 9, 2022

2717; Nusu muda, muda kamili na muda wote (au safari ya kuelekea kwenye ubilionea). Siku chache zilizopita nilikuwa naangalia video kwenye mtandao wa youtube. Nilikutana na video moja ya Patrick Bet David ambapo alikuwa anaelezea hatua nne za kupata utajiri mkubwa. Kitu kipya nilichojifunza kwenye video hiyo ni dhana ya (more…)

2716; Nataka nikuoe/unioe.

By | June 8, 2022

2716; Nataka nikuoe/unioe. Pata picha, umekutana na mtu mahali kwa mara ya kwanza, humjui hakujui na hapo hapo akakuambia anataka akuoe/umuoe. Ni jambo ambalo litakushtua na kukushangaza. Iweje mtu akutake ufanye maamuzi makubwa hivyo wakati hata bado hamjajuana? Maamuzi ya kuoa/kuolewa na mtu huwa yanajengeka taratibu baada ya watu kuwa (more…)

2713; Matamanio makubwa zaidi.

By | June 5, 2022

2713; Matamanio makubwa zaidi. Hakuna ubaya wowote kwenye kuridhika haraka na kile ambacho mtu umekipata. Lakini ili uweze kupata mafanikio makubwa zaidi, lazima mtu uwe na matamanio makubwa zaidi. Ni matamanio makubwa ndiyo yaliyoisukuma dunia na kuifanya kuwa bora zaidi ya ilivyokuwa huko nyuma. Ni watu ambao hawakuridhika na kile (more…)