Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

3252; Kabla ya kujifunza kushinda.

By | November 26, 2023

3252; Kabla ya kujifunza kushinda. Rafiki yangu mpendwa,Kila mtu anataka kupata ushindi mkubwa kwenye maisha yake.Lakini wanaopata ushindi huo mkubwa na unaodumu huwa ni wachache.Wengi huwa wanapata ushindi ambao huwa unawapoteza kabisa. Ukweli ni kwamba kabla mtu hajajifunza kushinda, lazima kwanza ashindwe.Ni kupitia kushindwa ndiyo mtu anajifunza mambo mengi ya (more…)

3251; Unaowahofia siyo sahihi.

By | November 25, 2023

3251; Unaowahofia siyo sahihi. Rafiki yangu mpendwa,Kila tunapofanya jambo jipya na kubwa huwa unapatwa na hali ya hofu. Hofu ni kiashiria kwamba unafanya kitu kikubwa au kipya kuliko ulivyozoea.Wengi wamekuwa wanatumia hofu wanazokutana nazo kama sababu ya kuacha. Lakini hilo halipaswi kuwa hivyo.Hofu haipaswi kutufanya tuache.Bali inapaswa kuwa kichocheo cha (more…)

3250; Tayari unalipa hiyo gharama.

By | November 24, 2023

3250; Tayari unalipa hiyo gharama. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye uzalishaji huwa kuna dhana kwamba kama kampuni inahitaji kupata zana fulani ambayo itaongeza uzalishaji, lakini ikawa haiwezi kumudu gharama za zana hiyo, tayari inakuwa inalipa hiyo gharama.Hiyo ni kwa sababu kwa kampuni kukosa hiyo zana, inakuwa na uzalishaji mdogo na hivyo kukosa (more…)

3249; Maarifa pekee hayatoshi.

By | November 23, 2023

3249; Maarifa pekee hayatoshi. Rafiki yangu mpendwa,Moja ya mapingamizi ya watu wasiopenda kusoma vitabu ni kwamba hata waandishi na wauzaji wa vitabu hivyo hawajaweza kunufaika na kile kilichoandikwa kwenye vitabu hivyo. Huwa kuna utani kwamba mtu aliandika kitabu cha jinsi ya kupata mtaji wa kuanza biashara. Lakini akashindwa kuchapa kitabu (more…)

3248; Endelea na huo mpango.

By | November 22, 2023

3248; Endelea na huo mpango. Rafiki yangu mpendwa,Huwa tunakuwa na malengo makubwa, ambayo tunayawekea mipango ya kuyatekeleza malengo hayo na kuyafikia. Tukishaweka mipango huwa tunakuwa na shauku kubwa ya kuitekeleza, tukiona jinsi ilivyo rahisi na uhakika kufikia malengo hayo.Yote hiyo ni mipango, ambayo bado tunakuwa hatujaanza utekelezaji wake. Ni pale (more…)

3247; Kama ungeanza upya.

By | November 21, 2023

3247; Kama ungeanza upya. Rafiki yangu mpendwa,Moja ya vikwazo vinavyowazuia watu kufanikiwa ni mwili na roho kutokuwa sehemu moja.Unakuta kile ambacho mtu anafanya na kile ambacho angependa kufanya ni tofauti kabisa. Mtu anakuwa anafanya kitu ambacho kama angekuwa anaanza upya kufanya, asingekifanya.Kinachomfanya aendelee kuwa kwenye kitu hicho ni kwa sababu (more…)

3246; Ushindi unaotaka.

By | November 20, 2023

3246; Ushindi unaotaka. Rafiki yangu mpendwa,Ushindi wowote unaoutaka kwenye maisha yako, unawezekana kama tu utaacha kuwa na mashaka na kukataa kushindwa.Hivyo ndivyo vitu viwili ambavyo vimekuwa vinawakwamisha watu wengi kupata ushindi. Mashaka hayapaswi kupewa nafasi kama mtu unataka kupata ushindi mkubwa.Ukishakuwa tu na mashaka, unakuwa umeshikilia breki na hivyo huwezi (more…)

3245; Kabla ya kuhangaika na magumu.

By | November 19, 2023

3245; Kabla ya kuhangaika na magumu. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye safari ya mafanikio, watu huwa wanapenda kuhangaika na mambo makubwa na magumu.Lakini unakuta watu hao hao bado hawajaweza kufanya yale ya msingi kabisa kwenye eneo husika. Yale ya msingi huwa yanaoneka ni rahisi na yasiyo na mchango mkubwa.Lakini ndiyo mambo magumu (more…)

3244; Mara moja moja na kila mara.

By | November 18, 2023

3244; Mara moja moja na kila mara. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye maisha kuna mambo ambayo mtu unaweza kujikusanya na kuyafanya mara moja moja.Yanaweza kuwa mambo makubwa na ya kishujaa, ambayo wengi hawawezi kuyafanya. Lakini bado ni mambo ambayo hayawezi kumpa mtu mafanikio makubwa.Hiyo ni kwa sababu mafanikio siyo zao la kufanya (more…)

3243; Vitu vinavyokupa ushindi.

By | November 17, 2023

3243; Vitu vinavyokupa ushindi. Rafiki yangu mpendwa,Msukumo wa kwanza kwetu kwenye chochote tunachofanya ni kupata ushindi.Kila mtu anapenda ushindi, ni kiashiria kwamba mambo yamefanyika kwa usahihi. Lakini watu ambao wamekuwa wanapata ushindi mzuri na unaodumu wamekuwa ni wachache sana.Zipo sababu nyingi ambazo zimekuwa zinawakwamisha wengi wasipate ushindi mkubwa wanaoutaka. Moja (more…)