Category Archives: NENO LA LEO

Jifunze kila siku kupitia usemi mbalimbali.

Tulikuona Wakati Unakuja Mjini…

By | December 7, 2014

Tulikuona wakati unakuja mjini, usijione mjanja leo… Ulikuja umevaa yeboyebo na nguo umebeba kwenye mfuko wa rambo, leo unajiona unajua sana… Hayo ni maneno ya hovyo sana yanayotolewa na watu walioshindwa. Watu ambao wamepoteza muda wao kwa kufikiri wao ni wakongwe na anakuja mtu na kuwaacha wakishangaa. Ili kujifariji kwamba (more…)

NENO LA LEO; Hapa Ndio Unapoweza Kuanzia Na Hiki Ndio Unachoweza Kufanya.

By | December 7, 2014

Start where you are. Use what you have. Do what you can. –Arthur Ashe Anzia hapo ulipo. Tumia hiko ulicho nacho. Fanya unachoweza. Usipoteze tena muda kufikiri ni wapi pa kuanzia, uanze na nini au ufanye nini. Unachohitaji ni kuanza kupiga hatua na mambo mengine yote yatakwenda vizuri. Nakutakia siku (more…)

NENO LA LEO; Chochote Unachotaka Kuwa Kipo Huku

By | December 6, 2014

Everything you’ve ever wanted is on the other side of fear. –George Addair Chochote ambacho umewahi kutaka kipo upande wa pili wa hofu. Acha sasa kuwa na hofu na chukua hatua kupata kile unachotaka. Kumbuka hakuna kingine zaidi ya kuchukua hatua. Nakutakia siku njema. (more…)

NENO LA LEO; Umepangiwa Kuwa Mtu huyu…

By | December 5, 2014

The only person you are destined to become is the person you decide to be. –Ralph Waldo Emerson Mtu pekee uliyepangiwa kuwa ni yule unayeamua kuwa. Kama unaamua kuwa na mafanikio utakuwa nayo kweli na kama unaamua kuwa wa hovyo utakuwa wa hovyo. Maamuzi ni yako, uchaguzi ni wako. Nakutakia (more…)

NENO LA LEO; Maana Halisi Ya Vikwazo.

By | December 4, 2014

Obstacles are those frightful things you see when you take your eyes off the goal. –Henry Ford Vikwazo ni yale mambo ya kutisha unayoyaona pale unapoondoa macho yako kwenye malengo yako makubwa. Ukishaweka malengo na mipango yako usiangalie tena pembeni, utaona mambo mengi ambayo yatakukatisha tamaa. Nakutakia siku njema. (more…)

NENO LA LEO; Njia Moja Ya Uhakika Ya Kuepuka Kupingwa.

By | December 3, 2014

There is only one way to avoid criticism: do nothing, say nothing, and be nothing. –Aristotle Kuna njia moja pekee ya kuepuka kupingwa; usifanye chochote, usiseme chochote na usiwe chochote. Vinginevyo chochote utakachofanya lazima kuna mtu atakupinga au kukukosoa. Fanya kile unachoona ni sahihi kufanya na komaa nacho mapaka ufikie (more…)

NENO LA LEO; Jinsi Ya Kuua Hofu

By | December 2, 2014

If you hear a voice within you say “you cannot paint,” then by all means paint and that voice will be silenced. –Vincent Van Gogh Kama unasikia sauti ndani yako inayokuambia huwezi kuchora basi kwa njia yoyote ile hakikisha unachora na sauti hiyo itanyamazishwa. Usikubali kukatishwa tamaa na nafsi yako (more…)

NENO LA LEO; Uwekezaji Unaolipa Riba Kubwa Sana

By | November 30, 2014

An investment in knowledge pays the best interest. –Benjamin Franklin Uwekezaji kwenye elimu/ujuzi ndio uwekezaji unaolipa riba kubwa sana. Anza sasa kuwekeza kwenye ujuzi na elimu yako, jifunze mambo mapya na yafanyie kazi. Jinsi unavyojifunza zaidi ndivyo unavyoongeza thamani yako na hivyo kuongeza kipato chako. Nakutakia siku njema. (more…)

NENO LA LEO; Siku Mbili Muhimu Sana Kwenye Maisha Yako.

By | November 29, 2014

The two most important days in your life are the day you are born and the day you find out why. –Mark Twain Siku mbili muhimu sana kwenye maisha yako ni siku uliyozaliwa na siku uliyojua kwa nini ulizaliwa. Najua wengi tunajua siku tulizozaliwa ila ni wachache sana wanaojua kwa (more…)