Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; KAMA WEWE YAMEKUSHINDA, UNADHANI WENGINE WATAWEZA?

By | June 21, 2021

Wajibu wako wa kwanza kwenye maisha yako ni wewe mwenyewe. Hilo ndiyo jukumu lako kubwa unalopaswa kulipa kipaumbele kikubwa. Kitu chochote ambacho unataka watu wakupe, lazima uanze kujipa wewe mwenyewe. Ukitaka wakupende, jipende. Ukitaka wakukubali, jikubali. Na ukitaka wakuheshimu, jiheshimu. Kama wewe mwenyewe unashindwa kujipa vitu hivyo, unadhani wengine watawezaje (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FURAHIA CHANGAMOTO…

By | June 20, 2021

Wakati wengine wanazichukoa na kuzikimbia changamoto, wewe unapaswa kuzifurahia na kuzikaribisha, kwa sababu ndani yake huwa zina fursa nzuri za ukuaji zaidi kwako. Hutaweza kuziona fursa hizo nzuri kama utaona changamoto ni mbaya. Hivyo anza na mtazamo kwamba changamoto ni nzuri kisha jiulize ni fursa zipi nzuri zilizo ndani ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UKIWA NACHO UTAJUA…

By | June 19, 2021

Ukiwa na furaha utajua, huhitaji kujiuliza mara mbilimbili kama una furaha au la. Ukifanikiwa utajua, huhitaji kujihoji kama umefanikiwa. Mambo yote muhimu kwenye maisha, unayajua wazi kama unayo au la na kama bado unajiuliza, basi jibu ni huna. Tafakari ni maswali gani umekuwa unajiuliza mara kwa mara, jua nini unakosa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIHARAKISHE PASIPO NA UMUHIMU…

By | June 18, 2021

Huwa tunafikiri tutayafurahia maisha baada ya kupata vitu fulani au kufika hatua fulani. Tunaharakisha kufika huko na hatuipati hiyo furaha. Furaha haipo kwenye matokeo, bali kwenye mchakato. Hivyo unapaswa kuweka umakini wako kwenye kile unachofanya, kiwe ndiyo muhimu kabisa na kukipa muda wa kutosha. Kila unapochagua kufanya kitu, kinapaswa kuwa (more…)

Photo from Kocha Dr Makirita Amani

By | June 17, 2021

Hakuna kitu chenye gharama kubwa kwako kama usumbufu unaokuzunguka. Huwezi kuona gharama hiyo haraka kwa sababu akili yako inapata raha kirahisi. Ni baada ya muda mrefu ndiyo unakuja kugundua umekuwa unafanya kazi za kawaida na zisizo na ubunifu. Kutaka kwako kujua kila kinachoendelea kumepunguza umakini wako kwenye yale unayofanya na (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia ufundi wa

By | June 16, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia ufundi wa simu. Karibu kila mtu sasa anatumia simu ya mkononi. Kwa mazingira ya wengi, simu zao zimekuwa zinaharibika mara kwa mara na kuhitaji matengenezo. Hilo linatoa fursa mbalimbali za kuingiza kipato kupitia ufundi wa simu. Hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza kipato kupitia (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JINSI UNAVYOYAHARIBU MAISHA YAKO…

By | June 16, 2021

Unachagua mwenyewe kuyaharibu maisha yako kwa namna unavyochagua kuyaishi. Kila unachofanya kwenye eneo lolote la maisha yako, kinaathiri kila eneo la maisha yako. Ukifanya kazi yako hovyo, maisha yako yanakuwa hovyo. Ukiwa na mahusiano yasiyo mazuri, maisha yako yanaathirika pia. Unapaswa kujiwekea viwango vya juu kabisa kwenye kila unachofanya na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WANAKUKWEPA KIRAHISI…

By | June 15, 2021

Watu huwa siyo wepesi kusema hapana, wanajua wakikuambia hapana watakuumiza. Hivyo wanatafuta kauli ya kukuambia hapana bila kukuumiza. Na kauli rahisi huwa wanakuambia watakutafuta wakiwa tayari. Ukikubaliana na kauli hiyo na kusubiri wakutafute, utasubiri sana na hawatakutafuta. Badala ya kukubaliana nao tu kirahisi, waombe wakuambie lini watakuwa tayari, wakupe tarehe (more…)