Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya

By | June 14, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya nguo. Hakuna siku watu watatembea uchi duniani, hivyo mavazi yanabaki kuwa hitaji la msingi kabisa kwa wanadamu. Japo ni biashara yenye changamoto kubwa ya ushindani, maana wengi huona ndiyo biashara rahisi kwao kuingia na kufanya. Hapa kuna mawazo 10 ya kuingiza fedha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TUMIA AU POTEZA…

By | June 14, 2021

Kuna mambo mengi umewahi kujifunza kwenye maisha yako na kujiambia siku moja utayatumia, lakini umeshayasahau kabisa.Kuna mawazo mazuri yamewahi kukujia na ukajiambia utakuja kuyafanyia kazi ila umeyasahau kabisa.Kama hutatumia mawazo au maarifa unayoyapata wakati bado ni ya moto kabisa, nafasi ya kuyapoteza ni kubwa.Kila unapojifunza kitu, jiulize hapo hapo unawezaje (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya

By | June 13, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya mbao. Samani mbalimbali zinatengenezwa kwa kutumia mbao. Hilo linafanya uhitaji wa mbao kuwa mkubwa na kutoa fursa ya kibiashara kwa wale wanaoweza kushughulika na upatikanaji wa mbao. Hapa ni mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia biashara ya mbao. Kununua na kuuza mbao (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UKIINGIZA UCHAFU UTATOA UCHAFU…

By | June 13, 2021

Akili yako ni kompyuta yenye uwezo wa hali ya juu mno. Huwa inachakata chochote kinachoingia na kuzalisha matokeo. Kama uchafu unaingia kwenye akili, akili inauchakata na kutoa uchafu zaidi. Vile ulivyo sasa kwenye maisha yako ni matokeo ya kile ulichoruhusu kiingie kwenye akili yako. Kama unataka kuyabadili maisha yako, anza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; PAMBANA MPAKA UFIKIE LENGO…

By | June 12, 2021

Ukishajiwekea lengo, kinachofuata ni wewe kupambana mpaka ulifikie lengo hilo. Usipoteze nguvu zako kwenye kujishawishi kulibadili lengo kwa sababu unaona huwezi kulifikia. Badili mikakati na njia unazotumia, lakini usibadili lengo. Hata kama huoni namna ya kulifikia lengo, wewe amini kwenye lengo lako na kaa kwenye mchakato. Tathmini kila hatua unazochukua (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAKUNA MAISHA YA MAJARIBIO….

By | June 11, 2021

Watu wengi huendesha maisha yao kama vile bado wapo kwenye majaribio au mazoezi ya kuja kuishi maisha yenyewe. Kila wakati wanaahirisha kuishi, wakiwa shule wanajiambia wataanza kuishi wakihitimu na kupata kazi. Wakipata kazi wanajiambia wataanza kuishi wakistaafu. Wakistaafu wanajikuta wameshachelewa na wanakufa. Maisha yako ndiyo hayo unayoyaishi sasa, hakuna siku (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WANAPOKUKOSOA FURAHI…

By | June 10, 2021

Kwa sababu ni kiashiria kwamba unafanya kitu kikubwa na cha tofauti. Pia ukosoaji wao unakupima kama kweli unakiamini na kukisimamia kile unachofanya. Ukosoaji, upingaji na ukatishaji tamaa wa wengine, ni vitu vyenye manufaa kwako, maana ukiweza kuvivuka, utakuwa imara kupata chochote unachotaka. Ukurasa wa kusoma ni wanaokukosoa wanakusaidia; www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/09/2352 #NidhamuUadilifuKujituma (more…)

#TAFAKARI YA LEO; VIKUFANYE KUWA IMARA ZAIDI…

By | June 9, 2021

Hakuna siku maisha yako yatakosa vikwazo na changamoto mbalimbali. Hivyo ni vitu vitakuandama katika kipindi cha uhai wako. Hivyo njia pekee ya kuwa na maisha ya mafanikio na yenye utulivu, ni kutumia kila kikwazo na changamoto kuwa imara zaidi, kuwa bora zaidi baada ya changamoto kuliko ulivyokuwa kabla. Usizikimbie changamoto (more…)