Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

Mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia ukalimani wa

By | June 8, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia ukalimani wa lugha. Kadiri dunia inavyoungana na kushirikiana, watu wanahitaji kushirikiana kwenye shughuli mbalimbali. Lakini lugha huwa ni kikwazo katika ushirikiano huo. Hapo inajitokeza fursa ya ukalimani, ambapo mtu anayezielewa vizuri lugha mbili, anaweza kusaidia kwenye mawasiliano. Hapa ni njia kumi za kuingiza kipato (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAYEPASWA KUMHOFIA ZAIDI…

By | June 7, 2021

Siyo yule anayeongea sana, bali yule anayekaa kimya. Anayeongea sana anaweka kila kitu wazi kuhusu yeye, hivyo unaweza kujua mipango yake na kujiandaa mapema. Anayekaa kimya hujui anapanga nini na huwezi kujiandaa kwa ajili yake. Hivyo hofia zaidi wale wanaokaa kimya kuliko wanaoongea sana. Lakini pia wapo wanaoongea sana kama (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USHAURI WAKO NI MZURI KWAKO…

By | June 6, 2021

Unaweza kuona una ushauri mzuri sana kwa wengine, lakini tambua siyo wote watakaoona uzuri wa ushauri huo kama unavyouona wewe. Na hata kama watauona huo uzuri, bado siyo wote watakaofanyia kazi ushauri wako. Na kama unawashauri bila ya wao kuomba, ndiyo kabisa hawatajihangaisha na ushauri wako. Watu huwa hawathamini ushauri (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAPATA UNACHOTAFUTA…

By | June 5, 2021

Kama unatafuta sababu za kutokufanya kitu, utazipata nyingi tu. Na kama unatafuta njia ya kufanya kitu, utazipata za kutosha. Akili yako ina uwezo mkubwa wa kuvuta kwako kile unachotaka. Hivyo kama hujapata unachotaka, hebu anza kwa kuangalia akili yako inatafuta nini zaidi na utagundua kila ulichonacho sasa ndiyo akili yako (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIYAPOTEZE MAISHA KWA YASIYO NA TIJA…

By | June 4, 2021

Maisha tayari ni mafupi, mambo ya kufanya ni mengi na muda ulionao ni mchache. Usikubali kuyapoteza maisha yako kwa kuhangaika na mambo yasiyo na tija kwako kama kubishana. Usihangaike na kila anayekupinga au kuamini tofauti na wewe. Hata ukihangaika kuwabadili, bado hawatabadilika. Lakini kama jambo ni muhimu kweli, kama inabidi (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha ushonaji wa nguo.

By | June 3, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha ushonaji wa nguo. Ufundi wa kushona nguo huwa unaonekana ni kitu ambacho kila mtu anaweza kujifunza na kufanya. Na hivyo wengi wamekuwa hawalipi uzito hilo, wale wanaofanya hubaki wakifanya kwa mazoea na kulalamika hawawezi kuingiza kipato kwa njia hiyo. Hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIKUBALI MSONGO HUU…

By | June 3, 2021

Msongo wa mawazo unaosababishwa na matumizi ya mitandao ya kijamii ni wa kujitakia. Unajiweka mwenyewe kwenye mazingira ambayo watu wengi unaojihusisha nao huwajui halafu unakazana kujilinganisha nao wakati kila mmoja anaishi maisha ya maigizo huko mitandaoni. Unaweza kujionea mwenyewe kwa nini lazima upate msongo kwenye mitandao hiyo usipokuwa makini. Ni (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kutumia pikipiki.

By | June 2, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kutumia pikipiki. Kila mtu anapofikiria kuingiza kipato kwa pikipiki anafikiria njia moja iliyozoeleka ambayo ni bodaboda. Hilo limepelekea bodaboda kuwa nyingi mitaani na ushindani kuwa mkali. Kuna njia nyingine nyingi za kuingiza kipato kwa kutumia pikipiki. Hapa ni 10 katika njia hizo. Njia iliyo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WENYE CHUKI WAPUUZE…

By | June 2, 2021

Huwa tunapenda kupendwa na kukubalika na kila mtu. Lakini hata tufanyenye, kuna watu wanachagua tu kutuchukia. Hasa pale unapochagua kuyaishi maisha yako na kufanya makubwa, wengi hawatafurahishwa na hilo. Lakini wajibu wako siyo kumfurahisha kila mtu, bali kuyaishi maisha yako. Chagua kuyaishi maisha yako na wapuuze wale wanaokuchukua kwa wewe (more…)