Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

Mawazo 10 Ya Kuingiza Fedha Kama Mwalimu.

By | May 26, 2021

Mawazo 10 Ya Kuingiza Fedha Kama Mwalimu. Kupitia taaluma ya ualimu, kuna njia nyingi za kuingiza kipato. Hapa ni njia kumi ambazo mtu anaweza kutumia kuingiza kipato kwa taaluma hiyo. Kuajiriwa kama mwalimu. Kufundisha wanafunzi masomo ya ziada (tuition). Kujiajiri kama mwalimu kwa kufungua shule au chuo chako. Kuandika kitabu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAISHA YA USHINDI….

By | May 26, 2021

Kupata ushindi kwenye maisha yako kazana kulata ushindi kwenye siku zako. Kazana kuiishi kila siku kwa ushindi kwa kuwa na vipaumbele sahihi na kuvifanyia kazi hivyo. Kila siku hakikisha kuna kitu unafanya ambacho ni cha ushindi na kumbukumbu yake itaendelea kuwepo. Huwezi kuwa na maisha ya ushindi kama unazipoteza siku (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia ulichosomea.

By | May 25, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia ulichosomea. Tatizo kubwa la mfumo wa elimu unaotumika sasa ni kuwaandaa wanafunzi kwa njia moja tu ya kuingiza kipato, kuajiriwa. Wanafunzi wanafanya vizuri na kuhitimu, lakini nafasi za ajira hakuna. Kinachotokea ni wengi kukata tamaa na kuona elimu waliyopata haina maana. Elimu yoyote uliyopata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USISUBIRI HAMASA…

By | May 25, 2021

Usisubiri mpaka upate hamasa ndiyo uanze kufanya kile unachotaka kufanya. Badala yake anza kukifanya na utatengeneza hamasa ya kuendelea kukifanya zaidi. Ukisubiri mpaka upate hamasa ndiyo uanze utajichelewesha. Ukianza kabla hata hujawa na hamasa unajenga hamasa ya kuendelea kufanya. Kama ilivyo kanuni ya sayansi, kilichosimama huendelea kusimama wakati kilicho kwenye (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia uandishi wa

By | May 24, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia uandishi wa vitabu. Huwa nasema kila mtu ni kitabu kinachotembea. Maisha uliyoishi mpaka sasa kuna mengi umejifunza na kupitia ambayo ukiweka kwenye maandishi wengine wanaweza kukifunza pia. Pamoja na uandishi kuwa njia ya kushirikisha uzoefu wako kwa wengine, pia ni njia ya kuingiza kipato. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KITABU CHA MAELEZO YA MATUMIZI…

By | May 24, 2021

Unapoenda kununua kifaa chochote kipya, huwa unapewa kitabu chenye maelezo ya uwezo wa kifaa hicho na jinsi ya kukitumia. Unaposoma kitabu hicho, unaweza kutumia kufaa hicho kwa uwezo wake. Kwa bahati mbaya binadamu huwa hatuzaliwi na vitabu vya maelezo ya uwezo wetu mkubwa na tunayoweza kufanya. Hicho ni kitu mtu (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kutumia blogu.

By | May 23, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kutumia blogu. Blogu ni kitu ambacho kila mtu anaweza kuanzisha na kuendesha kama una msukumo mkubwa ndani yako wa kushirikisha kile unachojua, unachojifunza au ulicho na uzoefu nacho. Hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza kipato kwa kutumia blogu. Kuweka matangazo ya adsense, hapa unaunganisha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; POTEZA ILI USHINDE…

By | May 23, 2021

Maisha ni kama ligi ya mpira, timu inayochukua kombe siyo inayoshinda michezo yake yote, bali inayoshinda michezo iliyo mingi, tena ile ya muhimu. Kwa kujua hilo, ili timu ishinde inapaswa kujipanga na kujua michezo ipi lazima ishinde na ipi hata ikishindwa siyo mbaya, hilo linasaidia timu ipangilie rasilimali zake vizuri. (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia mtandao wa

By | May 22, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia mtandao wa intaneti. Mtandao wa intaneti umeleta mapinduzi makubwa duniani, umerahisisha kila kitu ikiwepo kuingiza kipato. Hapa kuna mawazo kumi unayoweza kutumia kuingiza kipato kwa kutumia mtandao wa intaneti mara moja. Anzisha blog ambayo utaweka maudhui mbalimbali na kisha kuitumia kuweka matangazo au kuuza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; IPE AKILI MAZOEZI…

By | May 22, 2021

Moja ya nadharia ya mageuzi (evolution) ni kwamba kiungo cha mwili kinachotumiwa sana kinakuwa imara na kile kisichotumiwa kinakuwa dhoofu. Ndiyo maana kama unatumia sana mkono wa kulia, unakuwa na nguvu kuliko wa kushoto. Kadhalika ndivyo ilivyo kwenye akili, ukiitumia sana inakuwa imara, usipoitumia inakuwa dhoofu. Akili dhoofu haiwezi kufanya (more…)