Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia simu yako.

By | May 21, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia simu yako. Kama unatumia simu janja (smartphone) na una mtandao wa intanetu, una fursa nyingi za kuingiza kipato. Hapa kuna mawazo kumi unayoweza kutumia kuingiza fedha kwa simu yako. Fursa ya kujifunza zaidi. Kujifunza na kubobea kwenye chochote unachofanya ni njia ya uhakika ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUKUTANA NA BAHATI…

By | May 21, 2021

Kila anayefikia mafanikio makubwa kwenye maisha, huwa kuna bahati anakutana nazo kwenye safari yake ya mafanikio. Lakini bahati hizi haziendi kwa aliyelala, bali zinaenda kwa aliye kwenye mapambano. Kwa kuwa hujui lini bahati itakufikia, wajibu wako mkubwa ni kuhakikisha uko hai na uko kwenye mapambano ili bahati inapokuja ikukute. Ukikata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NI VIWANGO ULIVYOJIWEKEA…

By | May 20, 2021

Kile ambacho wengine wanakupa kwenye maisha yako, ni kulingana na viwango ulivyojiwekea wewe mwenyewe. Ukijiwekea viwango vya juu na kuvisimamia, watakupa kadiri ya viwango hivyo. Hakuna anayekudharau au kukutukana kama huvumilii vitu hivyo. Kupata kile unachotaka, jiwekee viwango vyako kisha kataa kabisa kupokea au kuvumilia chochote chini ya viwango hivyo. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA WEWE…

By | May 19, 2021

Huwezi kupata mafanikio makubwa kwa kuyaiga maisha ya wengine. Hata kama watu hao wamefanya vitu fulani au kuishi kwa namna fulani wakafanikiwa, haimaanishi na wewe utafanikiwa kwa kuiga jinsi walivyofanya. Badala yake unapaswa kujifunza kutoka kwao, kisha kuishi uhalisia wako ili uweze kufanikiwa sana. Kwa kuishi uhalisia wako, hakuna anayeweza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAOSTAHILI UNACHOLIPWA…

By | May 18, 2021

Watu wengi huwa wanalalamikia kipato wanachoingiza, wakisema ni kidogo sana na siyo sahihi kwao. Wanaona wanastahili kulipwa zaidi ya hapo. Kwenye uchumi wa soko huria, unastahili kile unacholipwa, hata kama ni kidogo kiasi gani, kwa sababu kinaendana na thamani unayozalisha. Hivyo kama unataka kulipwa zaidi, wajibu wako ni mmoja, zalisha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAUMIVU NA MATESO…

By | May 17, 2021

Maumivu ni sehemu ya kawaida kwenye maisha yetu hapa duniani. Mambo huwa hayaendi kama tunavyotaka sisi na hilo huleta maumivu. Lakini mateso kwenye maisha ni kitu ambacho mtu unakichagua mwenyewe. Unachagua mateso pale unapokataa kukubaliana na ilichotokea na ambacho kipo nje ya uwezo wako au unapolazimisha kitu kiende unavyotaka wewe. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MATANGAZO SIYO MASOKO…

By | May 16, 2021

Watu wengi hudhani kutangaza biashara ndiyo kufanya masoko. Matangazo ni sehemu ya masoko ila siyo sehemu pekee. Masoko ni mfumo wa kuifanya biashara ijulikane na wateja, washawishike kununua na waendelee kuiamini biashara hata baada ya kununua. Masoko yanahusisha kila eneo la biashara kuanzia kwenye kuandaa bidhaa au huduma, kutengeneza hadithi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; VIASHIRIA VIKO WAZI…

By | May 15, 2021

Huwa tunawalalamikia watu kwamba wamebadilika, wakati tunaanza nao mahusiano au ushirikiano walikuwa namna fulani ila baadaye tunaona wamebadilika na kuwa kikwazo. Ukweli ni kwamba watu siyo wamebadilika, bali wameonesha uhalisia wao, wamekuwa hawawezi tena kuendelea kuficha uhalisia wao. Lakini tangu awali, kuna viashiria ambavyo watu walikuwa wanatuonesha ambapo kama tungevizingatia, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; EPUKA HUU MTEGO…

By | May 14, 2021

Kuna watu falsafa yao ya kutafuta fedha ni wanachoangalia ni kama fursa inaingiza fedha, hawajali fedha hizo zinapatikanaje, wao kama kitu kina faida wanafanya. Watu hawa hujikuta wananasa kwenye fursa ambazo zinaingiza faida kubwa siyo kwa sababu zina thamani ambayo watu wananufaika nayo, bali kwa sababu zina uhaba. Kwa uhaba (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HUWEZI KUJISIFIA HEKIMA…

By | May 13, 2021

Unaweza ukawaambia watu kwamba umesoma vitabu vingi au unajua mambo mengi sana. Lakini huwezi kuwaambia watu kwamba una hekima kubwa. Hekima ni kitu ambacho watu wanakiona kwako, kutokana na jinsi unavyoyatumia maarifa ambayo umeyapata. Hivyo pata maarifa mengi uwezavyo, ila yatumie kujijengea hekima, kwa kuyaweka kwenye matendo yale uliyojifunza. Hakuna (more…)