Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; VUNJA MAZOEA…

By | April 23, 2021

Chochote unachorudia kufanya kwa muda mrefu, huwa unakijengea tabia na kuanza kukifanya kwa mazoea. Inafika wakati unakifanya bila hata ya kufikiria kabisa. Ni vizuri kwa akili yako maana inapunguza mengi ya kufanya, lakini ni mbaya kwa ubunifu na ufanisi. Ukishafanya kwa mazoea huwezi kuja na ubunifu mpya. Kwa kuwa mazoea (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIJIDANGANYE MWENYEWE…

By | April 22, 2021

Ni rahisi kuwadanganya wengine kwa sababu hawajui kilicho ndani yako. Lakini unapoanza kuwadanganya wengine, inakuwa rahisi kujidanganya wewe mwenyewe pia. Unaweza kuwa na sababu nzuri ya kuwapa wengine ili wasikusumbue, lakini kamwe usije ukaisaha sababu ya kweli ya wewe kufanya unachofanya. Maana ukishaanza kujidanganya mwenyewe, unakuwa kwenye njia mbaya. Ukurasa (more…)

Thamini kinachopotea…

By | April 21, 2021

“Mostly it is loss which teaches us about the worth of things.” – Arthur Schopenhauer Kwenye maisha ya kawaida huwa tunathamini zaidi vitu ambavyo kuna hatari ya kuvipoteza. Mfano ukiambiwa ofa ya kitu inaisha, unakithamini zaidi na kuhakikisha unakipata. Lakini inapokuja kwenye maisha yako mwenyewe, mbona hutumii hilo? Mbona upoteze (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WAELEWE WATU KAMA UNAVYOIELEWA ASILI…

By | April 21, 2021

Huwa unaielewa asili na kwenda nayo kama inavyoenda. Hung’ang’ani kuilazimisha ibadilike na kwenda kama unavyotaka wewe. Kama ulitaka sana jua liwake, lakini mvua ndiyo ikanyesha, huhangaiki kulazimisha jua liwake, bali unaenda na vile mvua inavyonyesha. Lakini inapokuja kwa binadamu hufanyi hivyo, unataka wawe vile unavyotaka wewe, na kulazimisha kwa namna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KILA MAISHA YANA GHARAMA…

By | April 20, 2021

Ukiwa masikini unaweza kuona matajiri wana maisha rahisi kuliko wewe, kwa kuwa wanaweza kupata chochote wanachotaka. Ukiwa tajiri unaweza kuona masikini wana maisha rahisi kuliko yako, kwa sababu hawasumbuki na mambo mengi. Ukweli ni kwamba kila maisha yana gharama ambayo lazima ilipiwe, hakuna maisha ya bure. Hivyo usihangaike kutafuta maisha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USHAURI USIO SAHIHI…

By | April 19, 2021

Watu watajitolea kukupa ushauri mbalimbali ambao hata hujawaomba. Wataona wanajua jinsi unavyopaswa kuyaishi maisha yako kuliko wewe unavyojua. Chunga sana usishawishiwe na kila ushauri watu wanakupa. Kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako ni kupata kile unachotaka na hivyo ushauri unaohitaji ni wa kukusaidia kufika huko. Kama bado hujapata unachotaka, ushauri (more…)