Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; USHAWISHI WA WENGINE…

By | April 18, 2021

Kila unachosikia, kuona au kusoma, kuna ushawishi kinasababisha ndani yako. Hakuna kinachoingia kwenye akili yako bila kuacha madhara fulani. Hivyo unapaswa kuwa makini sana na watu unaowasikiliza, unaowaangalia na unaowasoma. Wale wenye ushawishi usio mzuri kwako, kaa nao mbali sana. Pia kuwa na msingi wako imara unaoufuata ambao mara zote (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUTAKA KUBEMBELEZWA…

By | April 17, 2021

Kama unachotaka ni kubembelezwa, umeshapishana na mafanikio. Kama hutaki kabisa kuumia, huwezi kuyafikia mafanikio makubwa. Hatua ya kwanza ya kufanikiwa ni kusimama kwenye ukweli na ukweli huwa unaumiza. Uongo unaweza kukubembeleza, ila ni kwa muda tu, ukweli utakuumiza, lakini utakuweka huru. Mara zote simama kwenye ukweli, ndiyo njia pekee ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SIYO RAHISI LAKINI INAWEZEKANA…

By | April 16, 2021

Kufikia mafanikio makubwa siyo kazi rahisi, lakini ni kitu kinachowezekana kwa sababu wapo ambao wameweza kuyafikia. Hivyo wajibu wetu kama tunataka kuyafikia, ni kujitoa kweli kweli na kuwa tayari kupambana kwa kila namna ili kuyapata. Tunapotaka kukata tamaa tujikumbushe haya mawili, kwamba wapo walioweza kufikia mafanikio hayo makubwa na wapo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HUWEZI KUELEWEKA NA WOTE…

By | April 15, 2021

Kueleweka au kukubalika na watu wote ni kitu ambacho hakiwezi kutokea. Hata kama unafanya jambo lenye manufaa kiasi gani, kuna ambao wataona ni bora ungefanya jambo jingine wanaloona lina manufaa zaidi. Hivyo msingi wako kwenye yale unayofanya haupaswi kuwa kukubalika na kila mtu, badala yake unapaswa kuwa ni kufanya kilicho (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIDHARAU HATUA NDOGO NDOGO…

By | April 14, 2021

Hakuna kitu unachofanya kisiache madhara kwenye maisha yako. Kila hatua unayochukua, hata kama ni ndogo kiasi gani, inaacha alama kwenye maisha yako na unavyorudia kufanya inajenga au kubomoa tabia fulani ndani yako. Pia kile unachofanya, kinageuka kuwa mazoea na baadaye unajikuta unafanya bila hata ya kufikiri. Kuwa makini sana na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WINGI HAUBADILI USAHIHI…

By | April 13, 2021

Huwa tunapenda kupima usahihi wa kitu kwa kuangalia wingi wa wanaokifanya. Kama wengi wanafanya au kukubaliana na kitu, tunaamini kitu hicho ni sahihi na hata kama siyo sahihi basi tunaamini kifo cha wengi ni harusi. Tatizo ni huwezi kufanikiwa kwa kuhangaika na yasiyo sahihi na kama unapima usahihi wa kitu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; EPUKA KAULI HII YA KITAPELI…

By | April 12, 2021

Utapeli huwa hautofautiani sana, ukiwa na akili kidogo tu na ukaitumia, utaona wazi viashiria vya utapeli. Na matapeli wanajua kuna viashiria vilivyo wazi na pale unapouliza kuhusu hilo tayari wana majibu. Watakuambia hii ni tofauti na nyingine ambazo utakuwa umefananisha nazo. Na kama utaendelea kuuliza zaidi watakuonesha wengine ambao tayari (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KIPIMO NI WINGI WA WANAOFANYA…

By | April 11, 2021

Kipimo rahisi kabisa unachoweza kutumia kuamua kitu gani ufanye ni kuangalia wingi wa wale wanaokifanya kitu hicho. Ukiona kitu kinafanywa na watu wengi, jua hicho siyo sahihi kwako kufanya. Kwa sababu watu wengi wanapenda kufanya vitu rahisi na vilivyo rahisi huwa havina thamani kubwa. Wewe unapaswa kufanya vitu vyenye thamani (more…)

#TAFAKARI YA LEO, HAKUNA KINACHOPOTEA…

By | April 10, 2021

Kuna wakati utaweka juhudi na muda kwenye kile unachofanyia kazi, lakini matokeo unayopata yasiwe sahihi. Ni rahisi kuona juhudi na muda ulioweka vimepotea. Kama upo kwenye mchakato sahihi, basi jua hakuna kinachopotea, hata kama matokeo unayopata siyo uliyotaka, jua juhudi na muda ulioweka havijapotea, badala yake ni uwekezaji ambao baadaye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TOA ILI UPATE…

By | April 9, 2021

Watu wengi wanakwama kwenye maisha kwa sababu wanataka kupata kwanza kabla hawajatoa. Mtu anataka kazi imlipe vizuri ndiyo aweke juhudi au biashara impe faida kubwa ndiyo aweke umakini wake mkubwa. Kinachotokea ni hawapati kile wanachotaka. Ili kupata unachotaka, anza kutoa kwanza. Anza kuweka juhudi kubwa kwenye kazi na biashara yako (more…)