Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; HESHIMA NI BORA KULIKO KIKI…

By | April 8, 2021

Watu wanaotaka mafanikio kwa njia za mkato, huwa wanakimbilia kutumia kiki. Kufanya mambo ya kijinga ambayo yanawapa umaarufu wa haraka, lakini usio na heshima. Umaarufu wa aina hiyo huwa haudumu muda mrefu na huacha madhara makubwa. Wewe jenga mafanikio na umaarufu wako kupitia heshima na heshima inajengwa kupitia kutoa thamani (more…)

#TAFAKARI YA LEO; RAHA IPO KWENYE KUFANYA…

By | April 7, 2021

Watu wengi hutegemea kupata raha au furaha baada ya kukamilisha kufanya kitu. Lakini ukweli ni kwamba raha inapatikana wakati wa kukifanya kitu, siyo baada ya kumaliza kukifanya. Na ili uipate raha hiyo, lazima uwe umechagua na kuridhia kukifanya na wakati wa kukifanya unaweka umakini wako wote hapo. Usihangaike kutafuta raha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAJUTO HAYAKWEPEKI….

By | April 6, 2021

Majuto ni kitu kisichokwepeka kwenye maisha yako. Kwa kila jambo utakalofanya, kuna majuto utakuwa nayo. Hasa pale unapokuwa na machaguo mbalimbali na inabidi uchague moja, haijalishi utachagua lililo bora kiasi gani, kuna wakati utaona bora ungechagua kingine. Hivyo usiangalie kutokuwa na majuto kabisa, bali angalia maamuzi ambayo yatakupa majuto madogo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UMEWAFUNDISHA MWENYEWE…

By | April 5, 2021

Jinsi watu wanavyokuchukulia, ni wewe mwenyewe umewafundisha. Wanaiga kile unachojifanyia mwenyewe na ndiyo wanakufanyia. Kama unajiheshimu, watu lazima wakuheshimu, ukijidharau wanakudharau. Kama unajithamini na watu pia watalazimika kukuthamini. Ndiyo maana ni muhimu sana kujiwekea viwango vyako vya kimaisha na kuviishi, maana bila hivyo watu watakuwekea viwango vya chini ili wakutumie (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KIPIMO CHA UIMARA…

By | April 4, 2021

Uimara wa kitu huwa unapimwa kwa kukipitisha kitu hicho kwenye mazingira magumu kabisa. Mazingira ambayo kitu kisichokuwa imara hakiwezi kuyastahimili. Hivyo pia ndivyo uimara wa watu unavyopimwa, kwa kuwapitisha kwenye mazingira magumu. Unapopitia magumu yoyote, jua hicho ni kipimo cha uimara wako. Unapoamua kufanikiwa, uimara wako utapimwa kwa viwango vya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UTAWARIDHISHA WANGAPI?

By | April 3, 2021

Sisi binadamu kama viumbe wa kijamii, tumejengewa mazoea ya kutaka kuwaridhisha wengine ili watukubali. Hili lilikuwa muhimu kipindi cha kale ambapo watu walikuwa kwenye makundi madogo na hali ilikuwa hatari. Lakini sasa mambo yamenadilika, hatupo tena kwenye makundi madogo na hatari siyo kubwa. Hivyo unapokazana kuwaridhisha wengine, haina msaada wowote (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TEGEMEA UWEZO NA SIYO HURUMA…

By | April 1, 2021

Wafanye watu wakuchague wewe kutokana na uwezo ulionao katika kufanya vizuri kile wanachohitaji na siyo kwa kukuonea huruma. Wakikuchagua kwa huruma wanakuwa wametumia hisia, ambazo huwa hazidumu. Lakini wakikuchagua kwa uwezo, wanakuwa wametumia mantiki, ambayo hudumu wakati wote. Badala ya kutaka uonewe huruma au upendelewe, kazana kujijengea uwezo wako kwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HUDUMA…

By | March 31, 2021

Chochote tunachotaka kwenye maisha yetu, ni wengine wanacho. Hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tubaweza kuwashawishi wengine kutupa tunachotaka. Na njia ya uhakika ya kufanya hivyo ni kutoa huduma kwa wengine. Chochote unachofanya, hakikisha kina manufaa kwa wengine, kinaongeza thamani kubwa kwao na kuyafanya maisha yao kuwa bora. Hakikisha unayagusa maisha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UPENDO…

By | March 30, 2021

Falsafa kuu ya mafanikio inayotuongoza kwenye safari nzima ni upendo. Kwa kujipenda sisi wenyewe tunajikubali tulivyo na kuwa sisi, badala ya kutaka kuwa kama wengine. Kwa kuwapenda wengine tunawakubali na kuwapokea walivyo na kuona njia bora ya kushirikiana nao, bila kutaka wawe tofauti. Kwa kupenda kile tunachofanya hakiwi tena kazi (more…)