Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; KAZI…

By | March 29, 2021

Kama kuna rafiki mmoja unayemhitaji sana kwenye maisha yako basi ni kazi. Kazi haijawahi kumtupa yeyote anayeipenda na kuiheshimu. Kazi imekuwa inalipa sawasawa na mtu anavyoweka juhudi. Chochote unachotaka kwenye maisha yako, utakipata kupitia kuweka kazi kwa juhudi kubwa. Kuanzia fedha, mafanikio, heshima, afya na hata mahusiano bora. Kila chenye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HEKIMA…

By | March 28, 2021

Kujua pekee haitoshi, bali kufanyia kazi kile unachojua ndiko kunakoweza kukufikisha kwenye mafanikio. Hekima ni kujua na kufanyia kazi kile unachojua. Kwa zama tunazoishi sasa, hakuna uhaba wa maarifa, lakini kuna uhaba mkubwa wa hekima. Watu wamekuwa wanapata maarifa mengi, lakini hawawezi kuyachambua na kujua yaliyo muhimu na kisha kuyatumia (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UTAJIRI…

By | March 27, 2021

Kuna watu wakisikia neno utajiri wanajisikia vibaya, kama vile ni neno baya ambalo ni mwiko kulisema hadharani. Hivyo ndivyo jamii ilivyowatengeneza watu, kuhakikisha hawafikii utajiri ili waendelee kuwa watumwa wa jamii husika. Utajiri ni kitu cha asili, asili huwa haipendi utupu, hivyo hujaza kila aina ya utupu. Fikiria madini ambayo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; AFYA…

By | March 26, 2021

Safari ya mafanikio siyo rahisi, inahitaji mapambano makubwa. Hivyo hitaji la kwanza muhimu kwenye safari hii ni mtu kuwa na afya imara. Afya hiyo inahusisha mwili, akili na roho. Akili inafanya maamuzi, roho inakupa msukumo na mwili unayekeleza. Kwenye afya ya akili unapaswa kuilisha maarifa sahihi, roho inahitaji utulivu mkubwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UADILIFU…

By | March 24, 2021

Uadilifu ni moja ya misingi muhimu sana kwenye mafanikio yako. Ili ufanikiwe, lazima watu wakuamini na watu watakuamini kupitia uadilifu wako. Huwezi kuaminika kama unayosema na unayofanya yanatofautiana. Huwezi kuaminika kama unaahidi vitu na hutekelezi. Huwezi kuaminika kama ukiwa faragha unafanya mambo mengine na ukiwa kwenye hadhara unafanya mambo mengine. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NIDHAMU…

By | March 23, 2021

Nidhamu ni moja ya misingi muhimu sana ya mafanikio. Ni nidhamu inayokuwezesha kupanga na kutekeleza ili kufanikiwa. Nidhamu binafsi ni kujiheshimu mwenyewe na kutekeleza unayopanga. Nidhamu ya kazi ni kujiwekea viwango vya ufanyaji kazi na kuvifuata kila wakati. Nidhamu ya fedha ni kuongeza kipato, kuweka akiba na kuwekeza. Nidhamu ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNACHOJUA NA UNACHOFANYA…

By | March 22, 2021

Matokeo unayopata sasa kwenye maisha yako, siyo ajali wala bahati, bali ni wewe mwenyewe umeyatengeneza. Umeyatengeneza kutokana na kile unachojua na hatua ambazo umekuwa unachukua. Kama unataka kupata matokeo ya tofauti na unayopata sasa, kwanza jifunze vitu vya tofauti na kisha chukua hatua za tofauti. Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIHANGAIKE NA MENGI…

By | March 21, 2021

Mambo ya kufanya ni mengi ma mengi mno yanawinda umakini wako. Lakini huna muda wala nguvu za kuweza kufanya yote yanayokutaka uyafanye. Kama unataka matokeo mazuri, lazima uweke vipaumbele vyako vizuri, uhangaike na yale ambayo ni muhimu zaidi, ambayo wewe tu ndiye unaweza kuyafanya kwa namna bora unayotaka. Mengine ambayo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TUMIA FIKRA ZAKO VIZURI…

By | March 20, 2021

Fikra zako zina nguvu ya kuumba chochote kile, kiwe kizuri au kibaya. Ni wajibu wako kutumia nguvu hiyo ya fikra kutengeneza ndoto kubwa na nzuri kwako na kuziamini kisha kuzifanyia kazi. Hata kama umefungwa kimwili au mwili unateswa, usiruhusu akili na fikra zako zifungwe au kuteswa. Hata kama unapitia magumu (more…)