Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; LINDA UTULIVU WA AKILI YAKO…

By | March 9, 2021

Watu wakitaka kuyavuruga maisha yako, wanaanza kwa kuvuruga akili yako. Watu wakitaka kukuibia au kukutapeli, wanaanza kwa kuivuruga akili yako. Na hata wale wanaotaka kukutumia kwa manufaa yao, wanahakikisha wamevuruga akili yako kwanza. Akili yako ni rasilimali muhimu na yenye nguvu kubwa ndiyo maana ni kitu cha kwanza kushambuliwa. Kila (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUJIANDAA KUISHI…

By | March 8, 2021

Sehemu ambayo wengi wanayapoteza maisha yao ni kwenye kujiandaa kuishi. Kila wakati mtu anajiambia hajawa tayari, hivyo hafanyi kile anachotaka. Ukiwa shule unasema ukihitimu utaanza kuishi maisha yako. Ukihitimu unasema ukipata kazi utaanza. Ukipata kazi unasema ukimaliza kulea utaanza. Ukimaliza kulea unasema ukistaafu utaanza. Ukistaafu unakuta muda umeshakuacha. Seneca amewahi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NA KWAKO YANAWEZA KUTOKEA…

By | March 7, 2021

Yale unayoona yakitokea kwenye maisha ya wengine, jua na kwako pia yanaweza kutokea. Iwe ni mazuri au mabaya, yana nafasi ya kuja kwako pia. Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi sahihi ya kukabiliana na lolote linalokuja kwako, ili lisikujie kwa mshangazo. Mstoa Seneca alishauri mtu uishi kwenye ile hali unayoihofia kutokea (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HESHIMU THAMANI YAKO…

By | March 6, 2021

Unapaswa kuijua thamani yako na kisha kuiheshimu na kuisimamia, bils kujali wengine wanafanya nini au kukucgukuliaje. Hupaswi kuyumbishwa na maoni ya wengine kuhusu wewe, ijue thamani yako na kuisimamia. Kama ambavyo dhahabu itabaki kuwa dhahabu, hata kama itawekwa kwenye tope au kudharauliwa na wengine. Na kama ambavyo noti ya elfu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NI MSIMAMO…

By | March 5, 2021

Kama unayataka mafanikio makubwa, lazima ujijengee msimamo kwenye kile unachofanya. Hakuna utakachofanya mara moja ukafanikiwa, ila kile unachofanya kwa kurudia rudia ndiyo utafanikiwa. Kuandika makala moja siyo jambo la kishujaa, ila kuandika kila siku kwa muda mrefu kutakufanya mwandishi bora. Kila mtu anaweza kufanya kitu mara moja, ila wanaofanikiwa wanajijengea (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MWILI USITAWALE AKILI…

By | March 4, 2021

Mwili wako huwa haupendi kuchoka wala kuumia, hivyo hutafuta kila mbinu kukwepa kufanya mambo magumu. Hufanya hivyo kwa kuishawishi akili kwamba mambo ni magumu na hayawezekani. Iwapo akili itautii mwili wako, hutaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako. Badala yake akili inapaswa kuusukuma mwili uende zaidi, akili inapaswa kuupa mwili nguvu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UTULIVU UPO KWENYE KUFANYA MACHACHE…

By | March 3, 2021

Dunia inatuhadaa na kutuonesha kwamba tunapaswa kufanya kila kinachokuja mbele yetu. Kwa kuwa ya kufanya ni mengi lakini muda wetu ni mchache, hilo huleta msongo. Kadiri unavyokazana kufanya mengi zaidi kwenye muda mchache ulionao, ndivyo unavyopatwa na msongo. Ili kupata utulivu, unapaswa kufanya machache. Katika mengi yanayokusonga, chagua machache muhimu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FUTA MSAMIATI WA KUSHINDWA…

By | March 2, 2021

Hofu ya kushindwa ni moja ya vikwazo vinavyowazuia wengi kuchukua hatua na hata kuwakatisha tamaa wanapokutana na magumu. Wewe usijiulize unawezaje kuvuka magumu unayokutana nayo, bali jiulize magumu yanawezaje kukushinda. Kwa kubadili mtazamo wako kwa namna hiyo, unabadili kabisa mwelekeo wa maisha yako. Kushinda kunakuwa hakuna nafasi kwako, haijalishi unakabiliana (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAPATA UNACHOLENGA…

By | March 1, 2021

Wachezaji wa mpira wa miguu, huwa wanaelekeza mpira kwenye goli la timu pinzani. Siyo mipira yote inaingia na kufunga goli, lakini mara chache mpira utaingia golini na kuwa wamefunga goli, kitu kinachowaweka kwenye nafasi ya kupata ushindi. Kama wataelekeza mipira sehemu nyingine ambayo siyo goli la timu pinzani, hawawezi kushinda (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUPOTEZA UNACHOHITAJI…

By | February 28, 2021

Watu wengi wamekuwa wanapoteza kile wanachokihitaji, ili kupata wasichohitaji na mwisho kujikuta wameanguka vibaya. Hiyo yote husababishwa na tamaa ya kutaka kupata zaidi au kutokutaka kupitwa na kile ambacho wengine wananufaika nacho. Warren Buffett anaita huu ni upumbavu wa kiwango cha juu na ndiyo unapelekea wengi kuanguka kwenye biashara na (more…)