Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; INUKA UENDELEE…

By | February 27, 2021

Unapoanguka, hupaswi kubaki pale ulipoangukia, badala yake unapaswa kuinuka na kuendelea na safari yako. Kila mtu kwenye maisha huwa anaanguka, wanaobaki walipoanguka wanashindwa na wanaoinuka na kuendelea wanafanikiwa. Na hilo halitatokea mara moja, bali litajitokeza mara nyingi, hata ukianguka mara 10 amka mara ya 11 na uendelee na safari. Kama (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUPATA MUDA ZAIDI…

By | February 26, 2021

Unaweza kupata muda zaidi kwenye siku yako kama utaacha kuhangaika na yale yasiyo muhimu kwako. Kuna mengi unajihangaisha nayo sasa ambayo hayana mchango wowote kwako, mfano kufuatilia maisha ya wengine. Mstoa Marcus Aurelius amewahi kusema yule asiyehangaika na wengine wanafikiri, kusema au kufanya nini, ana muda mwingi wa kuhangaika na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JICHELEWESHE UNAPOKUWA KWENYE HALI HII.

By | February 25, 2021

Unapogundua kwamba upo kwenye hali ya kusukumwa na husia zaidi kuliko fikra, basi jicheleweshe. Hisia zina tabia ya kukufanya uone unapaswa kuchukua hatua mara moja, ila hatua unazochukua ukiwa kwenye hali hiyo huwa siyo nzuri kwako. Ukiwa kwenye hasira chelewa sana kuchukua hatua yoyote ile, jipe muda zaidi. Hasira zitakaposhuka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KITU CHA THAMANI ZAIDI…

By | February 24, 2021

Huwa tunashangaza, vitu vya thamani tunavichukulia poa, ila visivyo vya thamani tunahangaika navyo kweli. Fikiria muda unaotumia kwenye mambo yasiyo na manufaa yoyote kwako, kuanzia kufuatilia habari, maisha ya wengine, mabishano na ushabiki wa kila aina. Unayapa mambo hayo muda kuliko unavyoweka kwenye vitu vyenye tija kama kujifunza au kufanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SIYO KUFANYA MENGI…

By | February 23, 2021

Wengi hufikiri ili kufanikiwa lazima mtu afanye mambo mengi, ahangaike na kila linalopita mbele yake. Lakini huo siyo ukweli, wale wanaohangaika na mengi huwa hawafanikiwi, kwa sababu wanatawanya sana nguvu zao. Ili ufanikiwe unapaswa kufanya mambo machache kwa kina na siyo kufanya mengi kwa juu juu. Kufanya hayo machache kunakuweka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TUNZA UTULIVU WAKO…

By | February 22, 2021

Unaweka mipango yako vizuri, unafanya kila unachopaswa kufanya lakini matokeo yanakuja tofauti na ulivyotegemea. Hapo ndipo wengi huvurugwa na kukata tamaa, kwa kuona mambo hayawezekani. Unapaswa kujua hiyo ni hali ya kawaida, inayomkumba kila mtu. Hata unaoona wamefanikiwa sana, siyo kwamba hawakutani na hali hiyo, wanakutana nayo sana, ila wanaikabili (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KABLA JAMBO HALIJAKUSUMBUA…

By | February 21, 2021

Kabla hujaruhusu jambo lolote likusumbue au kukupa wasiwasi, jua kwanza kama lipo ndani au nje ya uwezo wako. Lililo ndani ya uwezo wako ni lile unaloweza kuchukua hatua na ukalibadili na lililo nje ya uwezo wako ni lile ambalo hakuna hatua unaweza kuchukua. Mfano umetoka nyumbani kuna mahali unataka kuwahi, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MUDA HAUKUSUBIRI….

By | February 20, 2021

Dunia haikusubiri wewe mpaka uwe tayari kuanza. Kila siku jua linachomoza na kuzama, miaka inayoyoma na muda wako hapa duniani unazidi kupungua. Wakati unapanga kusubiri au kuahirisha chochote, jikumbushe hili. Unaweza kufa muda wowote, jua hilo na likusaidie kwenye kuyaishi maisha yako ya kila siku, ndivyo alivyosema na kuishi Mstoa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNATUMA UJUMBE GANI?

By | February 19, 2021

Sisi binadamu tuna uwezo mkubwa wa kumsoma mtu kupitia anachosema, jinsi anavyokisema na kile anachofanya. Hivyo kila unachofanya na kusema, kuna ujumbe unatuma kwa wengine, ambao wanausoma vizuri na kuamua wewe ni mtu wa aina gani. Mtu anapokuhudumia unajua kabisa kama mtu huyo anakujali au la, kama anapenda anachofanya au (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUKOSEA NA KUPATIA…

By | February 18, 2021

Hakuna yeyote anayeweza kukosea mara zote au kupatia mara zote. Kila mmoja wetu kuna mambo anakosea na mengine anapatia. Tunapaswa kuwa wanyenyekevu ili kujua wakati tunapokosea na pia kuweza kujifunza kwa wengine. Kama unadhani wewe unapatia tu na wengine wanakosea tu, hutaweza kujifunza na mara zote utafanya makosa zaidi. Hata (more…)