Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; ANZA NA ULICHONACHO…

By | February 17, 2021

Kwa malengo na mipango uliyonayo, hapo ulipo tayari una vitu vingi unavyoweza kuanza kufanya. Lakini wengi huwa hawaanzi, badala yake wanatafuta sababu za kwa nini hawawezi kuanza. Kila mtu huwa anapata kile anachotafuta, anayetafuta sababu za kutokufanya kitu anazipata na anayetafuta mahali pa kuanzia anapapata. Wewe unataka nini, kama ni (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAAMUZI MAKUBWA YANAFANYWA NA WACHACHE…

By | February 16, 2021

Maamuzi yoyote makubwa na muhimu huwa yanafanywa na watu wawili mpaka watatu wenye ushawishi mkubwa na kisha kusukumwa kwa wengine wakubaliane nayo na kuonekana ni maamuzi ya wengi. Ni vigumu kwa watu wengi kufikia maamuzi kwa pamoja kwa sababu kila mtu anakuwa na mtazamo wake ambao unatofautiana na wa wengine. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TATIZO SIYO SABABU…

By | February 15, 2021

Huwa unapanga kufanya kitu, halafu sababu zinaingilia na wewe unaruhusu sababu hizo ziwe kikwazo. Tatizo kubwa zaidi linakuja pale sababu inapokuwa hiyo hiyo kila siku, miaka nenda miaka rudi, sababu ni ile ile. Mfano husomi vitabu kwa sababu huna muda, miezi inakwenda, husomi na sababu ni hiyo hiyo kwamba huna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; PESA, MUDA NA NGUVU…

By | February 14, 2021

Pesa ni nyenzo inayokuwezesha kupata muda na nguvu zaidi. Kama kuna kitu unafanya mwenyewe kwa masaa 10 kwa siku, ukitumia pesa unaweza kupata wengine wanaokupa masaa hayo kumi na nguvu zaidi. Wengi wamekuwa wanajisifia kwa kuokoa pesa, kabla hawajaangalia ni kuda na nguvu kiasi gani wanapoteza. Mara zote unaookka pesa, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UPANDE WA PILI WA JAMBO…

By | February 13, 2021

Watu wawili wanapogombana au kutokuelewana, jua kila mmoja amechangia kwa namna fulani pale walipofikia. Japo ukisikiliza upande mmoja mmoja, utasikia kila upande ukilaumu upande mwingine na upande huo kuonekana ni sahihi. Lakini utakuwa umefanya makosa makubwa kama utasikiliza upande mmoja pekee, kwa sababu kila jambo huwa lina pande mbili. Kabla (more…)

#TAFAKARI YA LEO; IKABILI HATARI…

By | February 12, 2021

Matatizo mengi kwenye maisha huwa yanaanza wakiwa madogo kabisa, ambayo kila mtu anaweza kuyatatua. Lakini wengi huwa hawayakabili yakiwa madogo, badala yake wanayaficha au kuyapuuza na hilo linayapa nafasi ya kukua na kuwa hatari zaidi. Wewe usifanye hivyo, kama kuna tatizo au hatari, kabiliana nayo, usiifiche wala kuikimbia. Ukurasa wa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UAMINIFU NDIYO USTAARABU…

By | February 11, 2021

Ustaarabu unajengwa kwenye msingi wa uaminifu, pale watu wanapoweka ahadi na kutekeleza ahadi hizo. Uaminifu unapokosekana, watu hawaaminiani na kila mtu anaumia. Unaenda kwa daktari ukiamini atafanya kile chenye manufaa kwako, kadhalika kwa mwalimu, mwanasheria, mhasibu na hata mfanyabiashara. Swali la kujitafakari leo ni je, ahadi gani unawapa watu na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SIYO KINACHOFANYWA, BALI ANAYEKIFANYA…

By | February 10, 2021

Watu hufikiri kuna kazi au biashara ukizifanya mafanikio ni uhakika. Hilo siyo kweli, kwenye kila kazi na biashara, kuna waliofanikiwa na walioshindwa. Kinachowatofautisha watu hao ni sifa zao za ndani. Wale wanaofanikiwa wana sifa za tofauti kabisa na wanaoshindwa. Sifa za mtu zina nguvu na mchango mkubwa mno kwenye mafanikio (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA NA MAONI YAKO MWENYEWE…

By | February 9, 2021

Maoni ni kitu rahisi kila mtu kuwa nacho, lakini wengi walio na maoni hawajayatengeneza wao wenyewe, badala yake wamechukua ya wengine. Wachache wanaotengeneza maoni yenye maslahi kwao, huwa wanayasambaza kwa kasi kama propaganda kwa kuwa wanajua wengi ni wavivu wa kujifunza, kuujua ukweli na kuwa na maoni sahihi. Kwa kuwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAKUNA ANAYEKUFIKIRIA SANA…

By | February 8, 2021

Hakuna anayekosa usingizi kwa kukufikiria wewe, kila mtu anahangaika kujifikiria mwenyewe. Unafikiria wengine wanafikiri nini kuhusu wewe, kumbe na wao wanafikiria wewe unafikiri nini kuhusu wao. Unaweza kuacha kufanya baadhi ya vitu ili kuwaridhisha wengine kumbe hata hawana muda wa kufuatilia nini umefanya na kwa nini umefanya. Kila mtu ana (more…)