Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; KUIFANYA DUNIA IWE UNAVYOTAKA…

By | January 8, 2021

Hicho ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako kabisa. Lakini wengi wamekuwa wakihangaika nacho, wakitaka kuifanya dunia iende wanavyotaka wao na watu wawe vile wanavyotaka. Hilo linaposhindikana wanaumia na kukata tamaa. Mtu pekee unayeweza kumdhibiti na kumbadili hapa duniani ni wewe mwenyewe. Hivyo peleka nguvu zako kwenye kujibadili na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KABLA HUJAWEKA JUHUDI…

By | January 7, 2021

Kabla hujaweka juhudi kwenye chochote unachofanya, hakikisha kwanza hicho ndiyo kitu sahihi kwako kufanya. Kabla hujazidisha mbio, hakikisha uko kwenye uelekeo sahihi. Kwa sababu haijalishi ni juhudi au mbio kiasi gani unaweka, kama unachofanya siyo sahihi, unazidi kujipoteza. Siku zinaanza na kuisha na kila siku unakuwa ‘bize’ na kuchoka kweli (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JIFUNZE KWA KILA MTU…

By | January 6, 2021

Kila mtu unayekutana naye, kuna kitu cha kujifunza kutoka kwake. Inaweza kuwa kitu cha kuanza kufanya au kuacha kufanya. Kuwa tayari kujifunza na utajifunza mengi mno. Unaweza kwenda mahali kupata huduma fulani na kisha ukapata huduma ambayo ni mbovu mno. Badala tu ya kulalamikia huduma mbovu uliyopata, jifunze kutokufanya hivyo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUMUDU KUFANYA KWA MUDA MREFU…

By | January 5, 2021

Ni rahisi sana kuhamasika na kuamua kuchukua hatua kubwa mara moja. Labda umesikia watu wenye mafanikio makubwa wanaamka mapema, saa tisa alfajiri na wewe ukaamua mara moja uanze kuamka saa tisa. Unaamka kwa siku chache lakini baadaye unashindwa. Au unajifunza kuhusu umuhimu wa mazoezi, unahamasika na kuanza mazoezi, siku ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NGUVU NA MUDA NI ULE ULE…

By | January 4, 2021

Kila siku mpya unayoianza, unakuwa na nguvu na muda ambao ni sawa. Unapoimaliza siku hiyo, unakuwa umetumia muda na nguvu ulizoanza nazo. Iwe umefanya mambo mazuri na ya mafanikio au umefanya mambo ya hovyo haijalishi, muda na nguvu vitakuwa vimetumika. Muda na nguvu utakazotumia kuzurura mitandaoni, au kubishana au kufuatilia (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAKOSA YA JANA…

By | January 3, 2021

Kila mtu huwa anakosea kwenye maisha. Unapanga hivi lakini unafanya mengine. Unajua unachopaswa kufanya lakini hukifanyi. Hakuna asiyekosea. Lakini kukosea mara moja siyo kikwazo cha mafanikio, bali kukosea kwa kujirudia rudia ndiyo kikwazo. Makosa uliyofanya jana usiyaruhusu yaendelee leo. Badala yake yatambue na kisha leo chukua hatua sahihi. Wanasema kosa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NAIISHI LEO…

By | January 2, 2021

Wakati pekee ambao nina udhibiti nao ni wakati uliopo. Siku pekee ninayoweza kuitumia kufanya makubwa ni siku hii ya leo. Jana imeshapita, chochote nilochofanya au kushindwa kufanya siwezi kukibadili. Kesho bado haijafika, chochote ninachohofia kuhusu hiyo kesho siwezi kukiathiri. Lakini leo, iko kwenye mikono yangu, ipo ndani ya udhibiti wangu, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAISHA YANGU NI JUKUMU LANGU…

By | January 1, 2021

Maisha yangu ndiyo jukumu langu kuu hapa duniani. Ndiyo wajibu wangu wa kwanza. Kama maisha yangu hayapo vile ninavyotaka, mimi ndiye wa kuwajibika. Sitamwachia mwingine jukumu hili, maana wengine nao wanapambana na maisha yao. Sitalalamika wala kumlaumu yeyote, badala yake nitachukua hatua sahihi kuyaboresha maisha yangu. Kama kuna jambo halipo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KULIPWA ZAIDI, TOA THAMANI ZAIDI…

By | December 31, 2020

Pesa ni zao la thamani. Kiasi cha pesa unachoingiza sasa ni matokeo ya thamani unayozalisha kwa wengine. Kama unataka kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa, toa thamani kubwa zaidi ya unayotoa sasa. Iwe ni kwenye ajira au biashara, zalisha thamani kubwa zaidi kwa wale wanaotegemea unachofanya. Fanya kwa namna ambayo hakuna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JIWEKEE VIWANGO VYAKO NA PAMBANA NAVYO.

By | December 30, 2020

Simba hata awe na njaa kiasi gani, huwa hawindi panya au wanyama wengine wadogo wadogo. Badala yake anapambana mpaka apate kitoweo sahihi kwake, ambacho ni mnyama mkubwa. Moja ya kikwazo cha mafanikio kwa wengi ni kushindwa kujiwekea viwango vya juu na kupambana kuvifikia. Kama unahangaika na kila kitu, hasa vitu (more…)