Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; RAHISI HAINA THAMANI…

By | December 29, 2020

Watu wengi wanahangaika kutafuta njia rahisi na za mkato za kupata mafanikio makubwa. Na hilo huwapeleka kufanya vitu ambavyo ni rahisi na vinavyofanywa na kila mtu. Matokeo yake ni hawafanikiwi, kwa sababu kile kinachofanywa na kila mtu hakithaminiwi. Jamii itakuthamini kama unafanya kitu ambacho inakihitaji sana, lakini hakuna mwingine anaweza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FUATA USHAURI WAKO MWENYEWE…

By | December 28, 2020

Bila shaka umeshatoa ushauri kwa watu wengi kwenye hali mbalimbali wanazopitia. Labda ni mtu alipata msiba na kumpa ushauri kwamba aliyefariki amepumzika pema. Au ni mtu aliyepata hasara au kupoteza kitu na ukamshauri kwamba kwa kuwa bado yuko hai, basi anaweza kupoteza chochote alichopata. Cha kushangaza sasa, wewe ukiwa kwenye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JUKUMU LAKO KUU NI WATU…

By | December 27, 2020

“People are our proper occupation, our job is to do them good and put up with them.” – Marcus Aurelius Jukumu lako kuu kwenye maisha ni watu. Wajibu wako mkubwa ni kuwatendea vyema na kuweza kuendana nao bila ya kujali wakoje. Kila kazi au biashara unayofanya, inawalenga watu. Hivyo unapofanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; INAANZIA NYUMBANI…

By | December 25, 2020

“Virtue and charity start at home. If you have to go some where to display it, then it is not virtue.” – Leo Tolstoy Upendo, wema na msaada ni vitu ambavyo vinaanzia nyumbani. Kama unavifanya vitu hivi nje lakini huwezi kuvifanya nyumbani, siyo vya kweli. Chochote tunachofanya kinapaswa kuanzia nyumbani, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAANA YA MAISHA NI KUKUA KIROHO…

By | December 24, 2020

“Grow spiritually and help others to do so; it is the meaning of life.” – Leo Tolstoy Maana ya maisha yetu na jukumu kubwa kabisa tulilonalo hapa duniani ni kukua kiroho. Changamoto nyingi tunazokutana nazo kwenye maisha na kutuyumbisha, ni kwa sababu ya uchanga wa kiroho. Unapokua kiroho, unaweza kukabiliana (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KABLA HUJAWEKA JUHUDI…

By | December 23, 2020

“Speed is only useful if you are running in the right direction” – Joel Barker Kabla hujaweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya, hakikisha kwanza ndiyo kitu sahihi kwako kufanya. Maana kama unachofanya siyo sahihi, juhudi zote unazoweka unazipoteza. Kabla hujaweka kasi kubwa kwenye safari uliyonayo, Hakikisha kwanza uko kwenye uelekeo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MOTO HUMEZA KILA KINACHOWEKWA…

By | December 20, 2020

“What’s thrown on top of the conflagration is absorbed, consumed by it—and makes it burn still higher.” – Marcus Aurelius Moto mkubwa na unaowaka kwa ukali, huwa unageuza kila kinachowekwa kwenye moto huo kuwa nishati na kuwaka zaidi. Moto huo hauogopi chochote unachopokea, badala yake unakipokea na kukigeuza moto unaowaka (more…)