Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TuvukePamoja; SHUKRANI.

By | May 16, 2020

Haijalishi unapitia nini, kuna kitu cha kushukuru. Unaposhukuru, unaangalia upande chanya wa maisha yako. Na kwa kuwa akili zetu hutuonesha kile tunachofikiria, Unapokuwa mtu wa shukrani, mambo mazuri zaidi yanakuja kwako. Katika kipindi hiki tunachopitia changamoto, kuwana kijitabu (diary) na kiite kitabu cha shukrani. Kisha kila siku andika yale unayoshukuru (more…)

#TuvukePamoja; CHAGUA KITU UTAKACHOKIFANYA KILA SIKU…

By | May 15, 2020

Katika changamoto hii ya covid 19 tunayopitia sasa, ni rahisi sana kuona mambo hayawezekani. Hilo linapelekea kukata tamaa na kukosa nguvu ya kuendelea na mapambano. Hivyo hicho ni kitu cha kwanza cha kupambana nacho, kuhakikisha kila siku unayo hamasa na nguvu kubwa ya kuendelea na mapambano, bila ya kujali matokeo (more…)

#TuvukePamoja; Maisha na covid 19.

By | May 14, 2020

Kama ambavyo nimekuwa nashirikisha mara kwa mara, na kama ambavyo taarifa mpya zinaonesha, ugonjwa huu wa covid 19 utachukua muda kuondoka. Na mategemeo ya kuondoka kwa ugonjwa huu ni pale dawa au chanjo itakapopatikana, kitu ambacho kinakadiriwa kuchukua siyo chini ya miezi 18. Hivyo tunapaswa kujifunza kuendelea na maisha katika (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; USIMWOGOPE YEYOTE WALA CHOCHOTE…

By | May 14, 2020

“Fear nobody and nothing. That which is the most precious matter in you can be damaged by no one and by nothing.” – Leo Tolstoy Watu wanapotaka kukutawala au kunufaika na wewe, huwa wanaanza na kitu kimoja, hofu. Wanakufanya uwahofie, uone kwamba wanao uwezo wa kuyaharibu maisha yako au kuchukua (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; MWENENDO WA SAA WAKATI WA DHORUBA..

By | May 13, 2020

“Quiet minds cannot be perplexed or frightened but go on in fortune or misfortune at their own private pace, like a clock during a thunderstorm.” — Robert Louis Stevenson Kama kuna dhoruba kali ambayo inaendelea, unafikiri mishale ya saa inaendaje? Je itakwenda haraka au polepole? Jibu unalijua, mishale ya saa (more…)