Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; WAJUE KUHUSU WEWE, ILA WASIKUJUE…

By | July 25, 2021

Mafanikio yana gharama kubwa. Na mafanikio yanapoambatana na umaarufu, yanakuwa na gharama kubwa zaidi. Wengi kabla hawajafanikiwa hutamani sana wapate umaarufu kwani huamini mafanikio yanayoendana na umaarufu ndiyo mazuri. Lakini wakishafanikiwa na kuwa maarufu ndiyo wanagundua jinsi hilo lilivyo mzigo mkubwa. Unapofanikiwa na kuwa maarufu unakuwa lengo la mashambulizi kwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; GIZA HALIDUMU MILELE.

By | July 24, 2021

Giza linapoingia, huwa hatuna wasiwasi kwamba huenda giza hilo likadumu milele. Tunajua kwa hakika kwamba kesho kutakucha, mwanga utakuna na giza kitapotea. Hivyo pia ndivyo maisha yetu yalivyo, kuna nyakati tunapitia magumu mbalimbali. Cha kushangaza huwa tunaona kama magumu hayo yatadumu maisha yetu yote. Ukweli ni hayadumu, ni kitu cha (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha unapokuwa chini

By | July 23, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha unapokuwa chini kabisa. Kuna wakati mtu unakuwa unapitia magumu sana kwenye maisha na kuona kama kila kitu hakiwezekani. Unaweza kukata tamaa na kuona huna cha kufanya. Lakini usiruhusu hilo, yapo mengi ya kufanya. Na kuna njia mbalimbali za kuingiza fedha pale unapokuwa chini kabisa. Fanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HUHITAJI TAARIFA ZAIDI…

By | July 23, 2021

Kwa chochote unachotaka kufanya, huhitaji taarifa zaidi ndiyo uanze. Tayari unazo taarifa za kukutosha kuanza kufanya. Ukijiambia unasubiri mpaka upate taarifa za kutosha, utakuwa unajidanganya. Unachopaswa ni kuanza kwa taarifa ambazo tayari unazo, na kisha kuendelea kujifunza kadiri unavyokwenda. Tunaishi kwenye zama za mafuriko ya taarifa, ni rahisi sana kuzama (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MTU RAHISI KUMDANGANYA…

By | July 22, 2021

Richard Feynman aliwahi kusema jukumu letu la kwanza ni kutokujidanganya kwa sababu ni rahisi mno kujidanganya wenyewe. Hakuna mtu rahisi kumdanganya kwenye maisha yako kama wewe mwenyewe. Kwa vitu unavyotaka na hujapata, utatafuta kila sababu ya kukuridhisha, isipokuwa kuukabili ukweli. Utaangalia nini umekosa au ugumu gani unakabiliana nao. Lakini hutaangalia (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAFANIKIO NI HATUA…

By | July 21, 2021

Mafanikio hayatokei kama ajali au bahati. Bali ni hatua ambazo mtu unapiga, kutoka sifuri, kwenda moja, kisha kumi, mia na kuendelea. Wengi walio sifuri huwa wanataka watoke sifuri mpaka 100, kitu ambacho hakijawahi kutokea. Unatoka sifuri mpaka moja, hapo unajifunza mengi mno. Kisha unatoka moja mpaka 10 ambapo yapo ya (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha bila kuwa na fedha.

By | July 20, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha bila kuwa na fedha. Huwa kuna kauli kwamba unahitaji fedha ili kupata fedha. Ilikuwa sahihi kipindi cha nyuma, ila siyo sasa. Unaweza kuingiza fedha hata kama huna fedha kabisa. Hapa ni mawazo kumi unayoweza kufanyia kazi. Fanya kazi au vibarua ambapo kinachohitajika ni nguvu zako (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MCHANGO WAKO KWENYE CHANGAMOTO…

By | July 20, 2021

Hakuna changamoto unayopitia ambapo wewe mwenyewe huna mchango katika kuisababisha au kuichochea. Kwa kila changamoto au magumu unayopitia, wewe una mchango. Hata kama unaona wengine ndiyo wanaohusika, kuna namna na wewe pia unahusika. Na uhusika wako mkuu huwa ni kukosa umakini kwenye kile unachofanya. Unapoweka umakini wako wote kwenye jambo, (more…)