Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; WATU WENYE CHUKI…

By | July 19, 2021

Ni watu ambao hupaswi kuwaruhusu wakusumbue kwa namna yoyote ile. Kwa sababu mtu akiwa na chuki na wewe, tayari ana chuki na yeye binafsi. Hakuna namna unaweza kumlazimisha anayekuchukia akupende, maana yeye mwenyewe hajipendi. Watu wanaojipenda hawana muda wa kuwa na chuki kwa wengine. Na watu wenye chuki, hawana manufaa (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa usomaji wa vitabu.

By | July 18, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa usomaji wa vitabu. Kitu kimoja ninachoamini sana ni kwenye zama tunazoishi sasa unaweza kulipwa kwa chochote unachofanya. Miezi michache iliyopita nilinunua simu mpya, wakati naiweka kwenye chaji ukaja ujumbe, ingiza kipato kwa kuchaji simu yako. Mwanzo nilishangaa, lakini baadaye nikajiambia kipi cha kushangaa kutoka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAZURI NA MABAYA…

By | July 18, 2021

Yote huwa yanatokea, na siyo kwa kupenda au kutokupenda kwako, bali ni sehemu ya maisha. Lakini unapoweka mipango yako, huwa unaangalia mzuri yanayoweza kutokea na kuyasahau mabaya. Kinachotokea ni kuumizwa sana pale mabaya yanapotokea. Hupaswi kuruhusu kitu chochote kitokee kwa mshangazo kwako, yaani kitokee bila ya kutegemea kabisa. Tafakari matokeo (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia mawazo yako.

By | July 17, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia mawazo yako. Akili unayo na unaweza kuitumia kuzalisha mawazo mbalimbali. Zipo njia mbalimbali za kuingiza fedha kupitia mawazo yako. Hapa kuna mawazo kumi ya kufanya hivyo. Kuja na mawazo ya kuongeza kipato chako na kuyafanyia kazi. Kuja na mawazo ya kupunguza gharama zako ili (more…)

#TAFAKARI YA LEO; BILA YA NAMBA…

By | July 17, 2021

Maendeleo na hatua zote ambazo tumepiga kama binadamu, ni kwa sababu ya mamba. Uwezo wa kupima na kulinganisha vitu umekuwa msukumo mkubwa kwetu kufanya vitu kwa utofauti mkubwa. Bila ya namba ni rahisi kujidanganya na kuamini unafanya makubwa. Lakini namba hazidanganyi, kama kitu kimefanyika kinaweza kupimika. Weka imani yako kwenye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HITAJI KUU LA MAFANIKIO…

By | July 16, 2021

Unapojifunza kwa wengine waliofanikiwa, haimaanishi uwe kama wao ili ufanikiwe. Njia ya uhakika ya kutokufanikiwa ni kujaribu kuwa kama wengine. Hitaji kuu la mafanikio ni wewe kuwa wewe, kujitambua, kujikubali, kujichagua na kujiamini. Hakuna anayeweza kukushinda wewe kuwa wewe na hapo ndipo ilipo nguvu kubwa kwako ya ushindani na kufika (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia samaki.

By | July 15, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia samaki. Samaki ni moja ya kitoweo muhimu kwenye maisha ya kila siku. Kwa kuwa kadiri watu watakavyoendelea kuwepo wataendelea kula, samaki ni moja ya chakula wanachohitaji. Hapa kuna mawazo kumi ya kuweza kuingiza kipato kupitia samaki. Kufuga samaki na kuwauza kwa ajili ya kula. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; CHAGUA KUWEKEZA VIZURI…

By | July 15, 2021

Muda na nguvu zako ni rasilimali muhimu sana kwako. Namna unavyochagua kutumia rasilimali hizo ni juu yako mwenyewe. Wapo wanaozitumia hovyo na kuzipoteza na wapo wanaozitumia vizuri na kunufaika. Wewe chagua kutumia rasilimali hizo vizuri, kwa kuhakikisha unaziwekeza kwenye kufanya mambo yenye tija kwako na kwa wengine pia. Iwe utachagua (more…)