Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

Mawazo 10 ya kuongeza mauzo kwenye biashara.

By | July 13, 2021

Mawazo 10 ya kuongeza mauzo kwenye biashara. Mauzo ndiyo injini ya biashara yoyote ile. Bila mauzo hakuna fedha inayoingia kwenye biashara na hapo hakuna biashara. Kila biashara inaweza kuongeza mauzo zaidi ya inavyofanya sasa, hata kama mauzo yako juu kiasi gani. Hapa ni mawazo 10 ya kuongeza mauzo kwenye biashara (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUNUFAIKA NA UNAYOSOMA…

By | July 13, 2021

Watu wengi hawanufaiki na yale wanayosoma, kwa sababu shule zimewaharibu. Shuleni mtu alisoma ili kufaulu mtihani, mtihani ukishapita basi hajali tena yale aliyosoma. Kwenye maisha husomi ili kujibu mtihani, bali unasoma ili kuyafanya maisha yako kuwa bora. Hivyo kwa kila unachojifunza, unapaswa kukitafakari ba kuona jinsi ya kukitumia kwenye maisha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUJIDANGANYA NA KUJIFARIJI…

By | July 12, 2021

Sababu nyingi unazojipa za kwa nini hujaweza kufanya au kupata unachotaka siyo sababu halisi, bali ni visingizio tu. Kwa visingizio hivyo umekuwa unajidanganya na kujifariji, kitu ambacho ni kikwazo kwa mafanikio yako. Kama kuna kitu unajipa kama sababu ya kikwazo, lakini wengine wameweza kuvuka kitu hicho, basi hiyo siyo sababu, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; GEUZA HOFU KUWA FURAHA…

By | July 11, 2021

Jamii imekutengenezs kuhofia mambo yasiyo na tija yoyote kwako. Mfano kuhofia wengine wanakuchukukiaje, kuhofia kukosolewa na hata kuhofia kupitwa na yanayoendelea kwenye mitandao. Hofu zote hizo hazina manufaa yoyote kwako. Ili kuziondoa zisiwe kikwazo, zigeuze kuwa furaha. Furahia pale wengine wanapokupinga au kukukosoa na kama ni watu sahihi jifunze kwao, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USICHANGANYE VIPAUMBELE…

By | July 10, 2021

Mafanikio makubwa ndiyo kipaumbele cha kwanza kabisa kwenye maisha yako, hupaswi kuruhusu kitu kingine kuingilia kipaumbele hicho. Utaona wengine wakihangaika na mambo mbalimbali kwenye maisha na kutamani kufanya kama wao. Lakini jua wengi hawafiki kwenye mafanikio makubwa na sababu kuu ni kuhangaika na mambo mengi badala ya kuweka vipaumbele sahihi. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; CHAGUA KUELEWEKA AU KUFANIKIWA…

By | July 8, 2021

Vyote viwili haviwezi kwenda pamoja. Ukitaka ueleweke na kila mtu huwezi kufanikiwa. Na ukitaka upate mafanikio makubwa, huwezi kueleweka na kila mtu. Wanaofikia mafanikio makubwa wanajali zaidi ndoto zao kuliko wengine wanawachukuliaje. Wanaoshindwa wanajali sana wengine wanawachukuliaje kuliko wanavyojali ndoto zao kubwa. Kipenga kimepulizwa, unachagua upande upi? Ukichagua upande wa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAZINA YA BIASHARA YAKO…

By | July 7, 2021

Ni wateja ambao tayari walishanunua kwenye biashara yako na kuridhika na kile walichokipata. Ukishakuwa na wateja wa aina hii basi biashara yako ina hazina kubwa. Ni wateja ambao ni rahisi kuwashawishi wanunue tena, lakini pia ni wateja ambao wanaweza kuweta wateja wengine. Kila siku pambana kujenga hazina hii kwenye biashara (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WAPE TAARIFA MPYA…

By | July 6, 2021

Kama kuna watu unataka wabadili maamuzi na misimamo yao, usikazane kuwaonyesha kwamba wamekosea, badala yake wape taarifa mpya zinazowapa nafasi ya kufanya maamuzi mapya. Hakuna mtu anayependa kukiri kwamba amekosea, hivyo kuwaonyesha wamekosea kunawafanya wazidi kusimamia maamuzi yao. Lakini unapowapa taarifa mpya ambazo zinawapa mtazamo mpya, wanaamua wenyewe kufanya maamuzi (more…)