Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA LEO; UPO TAYARI KUTOA NINI?

By | July 5, 2021

Wengi wanapoyaangalia mafanikio, wanachoangalia ni wanakwenda kupata nini. Huo ni upande mbaya wa kuangalia maana ndiyo ambao kila mtu anauangalia na ndiyo maana wengi hawafanikiwi. Wewe angalia kwanza upande wa unatoa nini. Uko tayari kutoa nini ili uweze kufanikiwa? Mafanikio siyo rahisi na ndiyo maana wengi hawafanikiwi. Kikwazo kikubwa ni (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA HAKIKUI, KUNA TATIZO…

By | July 4, 2021

Kama kitu kimezaliwa au kuanzishwa, kinapaswa kukua. Kama hakuna ukuaji maana yakr kuna tatizo, kuna kikwazo kinachozuia kitu hicho kisikue. Wajibu wako ni kujua tatizo au kikwazo kiko wapi, kukifanyia kazi ili kitu kiweze kukua. Na ili ujue kama kitu kinakua au la, lazima uwe na njia ya kukipima. Bila (more…)

#TAFAKARI YA LEO; IFANYE KAZI HII NGUMU….

By | July 3, 2021

Kwa kawaida huwa hatupendi kufanya vitu vigumu, badala yake tunakimbilia kwenye vitu rahisi. Sasa kwa kuwa vitu rahisi kila mtu anafanya, vinakosa thamani na inakuwa vigumu kufanikiwa. Moja ya kazi ngumu ambayo huwa tunaitoroka ni kufikiri na akili zetu huwa zinatafuta kila aina ya sababu ili tu tusifikiri mambo magumu. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNATAKA KUJISIKIA VIZURI AU KUWA BORA?

By | July 2, 2021

Ukitaka kujisikia vizuri, sikiliza uongo, maana huo unakubembeleza na haukuumizi. Ukitaka kuwa bora sikiliza ukweli, huo hakubembelezi na unakuumiza. Walio wengi wanapenda kubembelezwa na kutokuumizwa, ndiyo maana hawapigi hatua kwenye maisha yao. Ni wachache sana walio tayari kuukabili ukweli unaowaumiza na usiowabembeleza, lakini unawafanya kuwa bora zaidi. Kama unataka kufanikiwa, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TUMIA VIZURI KILA UNACHOKUTANA NACHO…

By | July 1, 2021

Kila kitu unachokutana nacho kwenye maisha, ni rasilimali muhimu kwako kufika kule unakotaka kufika. Usikipoteze wala kukitumia vibaya, badala yake kitumie kwa manufaa. Matumizi mazuri ya kitu ni kujiuliza namna ya kukitumia ili kufika kule unakotaka kufika. Matumizi mabaya ya kitu ni kulaumu au kulalamika kwa kukutana nacho. Kila unachokutana (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAATHIRI WENGINE…

By | June 30, 2021

Kila maamuzi unayofanya kwenye maisha yako huwa yana athari kwenye maisha ya wengine. Hiyo ni kwa sababu sisi binadamu tunategemeana sana kwenye maisha. Na chochote unachotaka kwenye maisha yako wanacho wengine, hivyo unachohitaji ni kuweza kuwapa wanachotaka ili nao wakupe unachotaka. Huwezi kufanikiwa peke yako bila kuhusiana na wengine, hivyo (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia

By | June 29, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia ushereheshaji. Watu huwa wanafanya matukio mbalimbali kwenye maisha na kuhitaji washereheshaji (MC) wa kuyaendesha matukio hayo. Hili linatoa fursa kwa mtu kuweza kuingiza kipato kama mshereheshaji. Hapa kuna mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia ushereheshaji; Kuendesha shughuli za sherehe kwa watu binafsi. Kuendesha mikutano (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIRIDHIKE…

By | June 29, 2021

Adui mkubwa wa mafanikio na maendeleo ni kuridhika na kile ambacho mtu ameshapata. Ugunduzi na hatua zote ambazo tumepiga kama wanadamu, ni kwa sababu watu hawakuridhika na kile walichokuwa nacho, japo kilikuwa bora. Iphone ya kwanza kutengenezwa yalikuwa mapinduzi makubwa mno, kila mtu alipenda namna teknolojia ilivyopiga hatua. Leo kuna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KWA NINI MAFANIKIO SIYO RAHISI?

By | June 28, 2021

Kwa sababu yanahitaji umakini mkubwa ambao wengi hawapo tayari kuuweka. Kwa sababu yanahitaji mtu afuatilie kwa kina kila anachofanya kitu ambacho wengi hawakitaki. Kwa sababu yanahitaji juhudi kubwa ambazo wengi hawapo tayari kuziweka. Na kwa sababu hayataki mazoea, kitu ambacho wengi wanakipenda sana. Huwezi kufanikiwa kwa kufanya vile unavyojisikia kufanya (more…)