Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; MAAMUZI YA MAKUBALIANO…

By | May 2, 2021

Maamuzi ya kufanya kwa makubaliano ili kumridhisha kila mtu huwa maamuzi mabovu sana kwako. Maamuzi yoyote yanayofikiwa na kundi kubwa la watu huwa ni maamuzi ya kawaida na hata utekelezaji wake huwa siyo mzuri. Maamuzi yanapaswa kusimama kwenye ukweli na siyo kumridhisha kila mtu. Ili ufanikiwe, lazima uwe tayari kufanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NI MAAMUZI YAKO…

By | May 1, 2021

Pale maisha yako yalipo sasa ni matokeo ya maamuzi ambayo umefanya siku za nyuma. Hata kutokufanya maamuzi ni sehemu ya maamuzi, kwa sababu unakuwa umeruhusu wengine ndiyo wakufanyie maamuzi. Na ukifanya maamuzi halafu usichukue hatua nayo pia ni maamuzi umefanya kutokuchukua hatua na yamekufikisha ulipo sasa. Njia pekee ya kuyabadili (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA HAWAKUELEWI NI SAWA…

By | April 30, 2021

Kama watu wanakulalamikia kwamba hueleweki, hawayaelewi maisha yako hilo lisikusumbue sana. Maana hakuna yeyote anayeiona dunia kwa namna unavyoiona wewe. Imani, mtazamo, fikra na uzoefu ulionao ni wa kipekee, ukiishi kwa kuzingatia hayo, utakuwa tofauti kabisa na wengine. Na kuwa tofauti haimaanishi unakosea, bali inamaanisha unafanya kilicho sahihi kwako. Watu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UTULIVU WA MAISHA…

By | April 29, 2021

Utulivu wa maisha huwa unaanzia kwenye utulivu wa fikra. Kama fikra hazijatulia, maisha pia hayawezi kutulia. Kwa fikra kuzurura hovyo, kunapelekea mtu kupatwa na msongo wa mawazo. Kuzidhibiti fikra zako zikae kwenye kile unachofanya kwa wakati husika ni njia bora ya kutengeneza utulivu wa maisha yako. Anza sasa kudhibiti na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA MAKINI NA UNACHOFANYA…

By | April 28, 2021

Unaweza kuwa bize kweli kweli, kila siku unachoka sana, lakini unayofanya yakawa ni kikwazo kwa unachotaka. Hili ndiyo linazuia wengi wasifanikiwe, wanahangaika na mambo ambayo siyo tu hayawasaidii, bali pia yanawazuia wasipate wanachotaka. Kila unachofanya, jiulize kwanza kama kitakufikisha unakotaka na kuwa na ushahidi kutoka kwa wale ambao wameshafika unakotaka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUPATA UNACHOTAKA…

By | April 27, 2021

Kupata chochote kile unachotaka, kunahitaji ushujaa wa hali ya juu sana, maamuzi ya kwamba lazima utakipata na ung’ang’anizi mpaka ukipate. Kama chochote kinaweza kukuzuia, hutapata unachotaka, lazima uwe ambaye huwezi kuzuiwa na chochote. Ambaye umeamua utapata unachotaka au utakufa ukiwa unapambana kukipata, hakuba chaguo jingine. Ukurasa wa kusoma ni mambo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MWENYE MACHAGUO MENGI NDIYE MWENYE NGUVU…

By | April 26, 2021

Kama mtu ana kitu ambacho watu wengi wanakihitaji na hawawezi kukipata pengine, huyo ana nguvu ya kukiuza kwa namna anavyotaka yeye. Kama watu wanaweza kupata wanachotaka popote, wana nguvu ya kuchagua wakapate wanachotaka wapi. Mwenye machaguo mengi ndiye mwenye nguvu ya kuamua apate kiasi gani kwenye majadiliano yoyote yale. Kama (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KINACHOFANYA MAISHA YAWE MAGUMU….

By | April 25, 2021

Ni kufanya mambo rahisi, kuishi kwa mazoea na kuigiza maisha. Unafanya mambo rahisi kwa sababu hutaki kuchoka, kusumbuka wala kuumia, hutaki pia kushindwa. Unafanya kwa mazoea kwa sababu hutaki kufikiri tofauti na unahofia kujaribu vitu vipya kwa kuwa huna uhakika navyo. Unaigiza maisha kwa kutaka uonekane tofauti na uhalisia wako (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIKUBALI WATU HAWA WAKUBABAISHE…

By | April 24, 2021

Utakapochagua kuishi maisha ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa, watu wanaokuzunguka hawatapendezwa na hilo. Watakupinga, kukukatisha tamaa na hata kukushauri namna unavyopaswa kuyaishi maisha yako. Cha kushangaza sasa, watu hao hawajui hata wanavyopaswa kuyaishi maisha yao, lakini wanaona ni wajibu wao kukupangia wewe jinsi ya kuishi. Kama utawasikiliza watu hao, utakuwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; VUNJA MAZOEA…

By | April 23, 2021

Chochote unachorudia kufanya kwa muda mrefu, huwa unakijengea tabia na kuanza kukifanya kwa mazoea. Inafika wakati unakifanya bila hata ya kufikiria kabisa. Ni vizuri kwa akili yako maana inapunguza mengi ya kufanya, lakini ni mbaya kwa ubunifu na ufanisi. Ukishafanya kwa mazoea huwezi kuja na ubunifu mpya. Kwa kuwa mazoea (more…)