Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; TEGEMEA UWEZO NA SIYO HURUMA…

By | April 1, 2021

Wafanye watu wakuchague wewe kutokana na uwezo ulionao katika kufanya vizuri kile wanachohitaji na siyo kwa kukuonea huruma. Wakikuchagua kwa huruma wanakuwa wametumia hisia, ambazo huwa hazidumu. Lakini wakikuchagua kwa uwezo, wanakuwa wametumia mantiki, ambayo hudumu wakati wote. Badala ya kutaka uonewe huruma au upendelewe, kazana kujijengea uwezo wako kwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HUDUMA…

By | March 31, 2021

Chochote tunachotaka kwenye maisha yetu, ni wengine wanacho. Hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tubaweza kuwashawishi wengine kutupa tunachotaka. Na njia ya uhakika ya kufanya hivyo ni kutoa huduma kwa wengine. Chochote unachofanya, hakikisha kina manufaa kwa wengine, kinaongeza thamani kubwa kwao na kuyafanya maisha yao kuwa bora. Hakikisha unayagusa maisha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UPENDO…

By | March 30, 2021

Falsafa kuu ya mafanikio inayotuongoza kwenye safari nzima ni upendo. Kwa kujipenda sisi wenyewe tunajikubali tulivyo na kuwa sisi, badala ya kutaka kuwa kama wengine. Kwa kuwapenda wengine tunawakubali na kuwapokea walivyo na kuona njia bora ya kushirikiana nao, bila kutaka wawe tofauti. Kwa kupenda kile tunachofanya hakiwi tena kazi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAZI…

By | March 29, 2021

Kama kuna rafiki mmoja unayemhitaji sana kwenye maisha yako basi ni kazi. Kazi haijawahi kumtupa yeyote anayeipenda na kuiheshimu. Kazi imekuwa inalipa sawasawa na mtu anavyoweka juhudi. Chochote unachotaka kwenye maisha yako, utakipata kupitia kuweka kazi kwa juhudi kubwa. Kuanzia fedha, mafanikio, heshima, afya na hata mahusiano bora. Kila chenye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HEKIMA…

By | March 28, 2021

Kujua pekee haitoshi, bali kufanyia kazi kile unachojua ndiko kunakoweza kukufikisha kwenye mafanikio. Hekima ni kujua na kufanyia kazi kile unachojua. Kwa zama tunazoishi sasa, hakuna uhaba wa maarifa, lakini kuna uhaba mkubwa wa hekima. Watu wamekuwa wanapata maarifa mengi, lakini hawawezi kuyachambua na kujua yaliyo muhimu na kisha kuyatumia (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UTAJIRI…

By | March 27, 2021

Kuna watu wakisikia neno utajiri wanajisikia vibaya, kama vile ni neno baya ambalo ni mwiko kulisema hadharani. Hivyo ndivyo jamii ilivyowatengeneza watu, kuhakikisha hawafikii utajiri ili waendelee kuwa watumwa wa jamii husika. Utajiri ni kitu cha asili, asili huwa haipendi utupu, hivyo hujaza kila aina ya utupu. Fikiria madini ambayo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; AFYA…

By | March 26, 2021

Safari ya mafanikio siyo rahisi, inahitaji mapambano makubwa. Hivyo hitaji la kwanza muhimu kwenye safari hii ni mtu kuwa na afya imara. Afya hiyo inahusisha mwili, akili na roho. Akili inafanya maamuzi, roho inakupa msukumo na mwili unayekeleza. Kwenye afya ya akili unapaswa kuilisha maarifa sahihi, roho inahitaji utulivu mkubwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UADILIFU…

By | March 24, 2021

Uadilifu ni moja ya misingi muhimu sana kwenye mafanikio yako. Ili ufanikiwe, lazima watu wakuamini na watu watakuamini kupitia uadilifu wako. Huwezi kuaminika kama unayosema na unayofanya yanatofautiana. Huwezi kuaminika kama unaahidi vitu na hutekelezi. Huwezi kuaminika kama ukiwa faragha unafanya mambo mengine na ukiwa kwenye hadhara unafanya mambo mengine. (more…)