Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; NIDHAMU…

By | March 23, 2021

Nidhamu ni moja ya misingi muhimu sana ya mafanikio. Ni nidhamu inayokuwezesha kupanga na kutekeleza ili kufanikiwa. Nidhamu binafsi ni kujiheshimu mwenyewe na kutekeleza unayopanga. Nidhamu ya kazi ni kujiwekea viwango vya ufanyaji kazi na kuvifuata kila wakati. Nidhamu ya fedha ni kuongeza kipato, kuweka akiba na kuwekeza. Nidhamu ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNACHOJUA NA UNACHOFANYA…

By | March 22, 2021

Matokeo unayopata sasa kwenye maisha yako, siyo ajali wala bahati, bali ni wewe mwenyewe umeyatengeneza. Umeyatengeneza kutokana na kile unachojua na hatua ambazo umekuwa unachukua. Kama unataka kupata matokeo ya tofauti na unayopata sasa, kwanza jifunze vitu vya tofauti na kisha chukua hatua za tofauti. Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIHANGAIKE NA MENGI…

By | March 21, 2021

Mambo ya kufanya ni mengi ma mengi mno yanawinda umakini wako. Lakini huna muda wala nguvu za kuweza kufanya yote yanayokutaka uyafanye. Kama unataka matokeo mazuri, lazima uweke vipaumbele vyako vizuri, uhangaike na yale ambayo ni muhimu zaidi, ambayo wewe tu ndiye unaweza kuyafanya kwa namna bora unayotaka. Mengine ambayo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TUMIA FIKRA ZAKO VIZURI…

By | March 20, 2021

Fikra zako zina nguvu ya kuumba chochote kile, kiwe kizuri au kibaya. Ni wajibu wako kutumia nguvu hiyo ya fikra kutengeneza ndoto kubwa na nzuri kwako na kuziamini kisha kuzifanyia kazi. Hata kama umefungwa kimwili au mwili unateswa, usiruhusu akili na fikra zako zifungwe au kuteswa. Hata kama unapitia magumu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MARA ZOTE SIMAMA KWENYE UKWELI…

By | March 19, 2021

Hakuna chochote kinachoweza kuhalalisha uongo, iwe unatumika kwa nia njema, matokeo yake huwa ni mabaya. Ni ukweli pekee ulio sahihi na unaomuweka mtu huru. Yeyote anayeweza kutumia uongo mdogo, anaweza kutumia mkubwa pia. Unapotumia uongo kwa sababu unaona ukweli utawaumiza watu, unaishia kuwaumiza zaidi. Ukweli hata ufichwe kiasi gani, haubadiliki, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; DUNIA HAITAKUACHA KIRAHISI…

By | March 18, 2021

Dunia huwa inakuweka kwenye kundi fulani ili iweze kukutumia inavyotaka yenyewe. Ili uweze kufanikiwa lazima uondoke kwenye kundi ambalo dunia inakuweka na uwe wewe, ufanye kilicho tofauti. Na hapo ndipo mgogoro mkubwa wa kimafanikio unapoanzia. Dunia itapambana kukurudisha kwenye kundi ambalo imekuweka huku wewe ukitakiwa kupambana kusimama kwenye kile ulichochagua. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MATATIZO NI YALE YALE…

By | March 17, 2021

Matatizo na changamoto kubwa zinazokusumbua kwenye maisha yako ni chache na zinazojirudia rudia. Matatizo na changamoto zinazowakabili wanadamu ni zile zile ambazo zimekuwepo miaka na miaka. Hivyo usihangaike na matokeo, badala yake tafuta chanzo. Na pia suluhisho bora ni suluhisho la zamani, ambalo limekuwepo miaka na miaka. Usikubali kuendelea kusumbuka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KULIKIMBIA TATIZO…

By | March 16, 2021

Bondia akiwa ulingoni, anaweza kutumia mbinu ya kumkimbia adui ili kujipa muda wa kumsoma adui na kuweka mkakati wake. Lakini lazima amkabili na kumshambulia kama anataka ushindi. Hawezi kushinda kwa kukimbia pekee na akikimbia sana ataishia kuchoka na kushindwa kirahisi. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa matatizo na changamoto mbalimbali za (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIFANYE MAMBO KUWA MAGUMU ZAIDI…

By | March 15, 2021

Mambo yanayokukabili sasa, yanakutosha kupambana nayo, ya nini ujiongezee mzigo kwa mambo ambayo bado hayajatokea? Huwa tunapenda kuhofia mambo ambayo bado hayajatokea, lakini hofu hizo huwa hazisaidii chochote, zaidi ya kuwa kikwazo kwetu kukabiliana na yaliyo mbele yetu. Yakabili yaliyo mbele yako sasa, peleka umakini wako wote hapo na yatakapokuja (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ADHABU YA ASILI…

By | March 14, 2021

Matatizo, vikwazo na changamoto mbalimbali unazopitia kwenye maisha yako, ni asili inakuadhibu. Asili huwa ina sheria zake ambazo huwa haiziweki wazi, lakini unapozivunja, inakupa adhabu kali. Kwa kila gumu unalopitia kwenye maisha, jiulize ni sheria ipi ya asili unaivunja, ijue, ifuate sheria hiyo na utaondokana ba magumu hayo. Asili haina (more…)