Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; MATATU YANAYOKUKWAMISHA…

By | March 13, 2021

Kutokujua hasa kile unachotaka, kutokujitoa hasa kupata unachotaka na kuwa na mbadala ni vikwazo vikubwa vitatu kwa mafanikio yako. Kama hujui kile unachotaka, kila mara utayumbishwa na wanayofanya wengine, ukiona wanafanya hiki na wewe unajaribu, wakifanya kile unajaribu pia. Mwisho wa siku unakuta muda umeenda na hakuna cha tofauti umepata. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUNA GHARAMA KUSIMAMIA UNACHOAMINI…

By | March 12, 2021

Mafanikio makubwa siyo rahisi kwa wengi kwa sababu yanahitaji msimamo. Na msimamo una gharama kubwa ambayo mtu anapaswa kuwa tayari kulipa. Je wewe upo tayari kulipa gharama kiasi gani ili kusimamia unachoamini? Maana dunia itatumia kila aina ya ushawishi na mateso kuhakikisha inakuangusha. Lazima uwe umejitoa kweli kweli kama unataka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FANYA MPAKA MWISHO…

By | March 11, 2021

Mafanikio huwa hayaji kwa kuanza kufanya vitu na kuishia njiani, bali huja kwa kufanya vitu mpaka mwisho. Japo haitakuwa rahisi, japo utakutana na vikwazo na changamoto, huwezi kufanikiwa kama utaishia njiani. Chochote unachochagua kufanya, amua kukifanya mpaka mwisho wake, kamwe usikubali kuishia njiani, pambana kwa kila namna uendelee kufanya. Moja (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KIPO UNACHOWEZA KUFANYA…

By | March 10, 2021

Haijalishi unapitia hali gani, kuna kitu unachoweza kufanya. Usikate tamaa na kukosa matumaini kwamba hakuna unachoweza kufanya. Martin Luther King amewahi kusema kama huwezi kuruka kimbia, kama huwezi kukimbia tembea na kama huwezi kutembea tamaa, fanya chochote kuhakikisha unasonga mbele. Hivyo ndivyo unapaswa kukabili kila linalokuja kwenye maisha yako, kwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; LINDA UTULIVU WA AKILI YAKO…

By | March 9, 2021

Watu wakitaka kuyavuruga maisha yako, wanaanza kwa kuvuruga akili yako. Watu wakitaka kukuibia au kukutapeli, wanaanza kwa kuivuruga akili yako. Na hata wale wanaotaka kukutumia kwa manufaa yao, wanahakikisha wamevuruga akili yako kwanza. Akili yako ni rasilimali muhimu na yenye nguvu kubwa ndiyo maana ni kitu cha kwanza kushambuliwa. Kila (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUJIANDAA KUISHI…

By | March 8, 2021

Sehemu ambayo wengi wanayapoteza maisha yao ni kwenye kujiandaa kuishi. Kila wakati mtu anajiambia hajawa tayari, hivyo hafanyi kile anachotaka. Ukiwa shule unasema ukihitimu utaanza kuishi maisha yako. Ukihitimu unasema ukipata kazi utaanza. Ukipata kazi unasema ukimaliza kulea utaanza. Ukimaliza kulea unasema ukistaafu utaanza. Ukistaafu unakuta muda umeshakuacha. Seneca amewahi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NA KWAKO YANAWEZA KUTOKEA…

By | March 7, 2021

Yale unayoona yakitokea kwenye maisha ya wengine, jua na kwako pia yanaweza kutokea. Iwe ni mazuri au mabaya, yana nafasi ya kuja kwako pia. Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi sahihi ya kukabiliana na lolote linalokuja kwako, ili lisikujie kwa mshangazo. Mstoa Seneca alishauri mtu uishi kwenye ile hali unayoihofia kutokea (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HESHIMU THAMANI YAKO…

By | March 6, 2021

Unapaswa kuijua thamani yako na kisha kuiheshimu na kuisimamia, bils kujali wengine wanafanya nini au kukucgukuliaje. Hupaswi kuyumbishwa na maoni ya wengine kuhusu wewe, ijue thamani yako na kuisimamia. Kama ambavyo dhahabu itabaki kuwa dhahabu, hata kama itawekwa kwenye tope au kudharauliwa na wengine. Na kama ambavyo noti ya elfu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NI MSIMAMO…

By | March 5, 2021

Kama unayataka mafanikio makubwa, lazima ujijengee msimamo kwenye kile unachofanya. Hakuna utakachofanya mara moja ukafanikiwa, ila kile unachofanya kwa kurudia rudia ndiyo utafanikiwa. Kuandika makala moja siyo jambo la kishujaa, ila kuandika kila siku kwa muda mrefu kutakufanya mwandishi bora. Kila mtu anaweza kufanya kitu mara moja, ila wanaofanikiwa wanajijengea (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MWILI USITAWALE AKILI…

By | March 4, 2021

Mwili wako huwa haupendi kuchoka wala kuumia, hivyo hutafuta kila mbinu kukwepa kufanya mambo magumu. Hufanya hivyo kwa kuishawishi akili kwamba mambo ni magumu na hayawezekani. Iwapo akili itautii mwili wako, hutaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako. Badala yake akili inapaswa kuusukuma mwili uende zaidi, akili inapaswa kuupa mwili nguvu (more…)